Mheshimiwa Spika;
Hayo si makusudio yangu. Kinachonileta
mbele ya Bunge lako Tukufu ni kuzungumzia Jumuiya ya Afrika Mashariki
na mustakabali wa Tanzania katika Jumuiya hiyo. Lakini, kwa sababu ya
umuhimu wa masuala hayo niliyoyataja na rai niliyopewa kuwa niyasemee
japo kidogo. Nimeona ni vyema nifanye hivyo.
Mheshimiwa Spika;
Kuhusu mchakato wa Katiba mpya,
napenda kusema kuwa tumefikia hatua nzuri katika utekelezaji wake. Kama
mjuavyo Tume ya Mabadiliko ya Katiba imekamilisha, kwa mafanikio, hatua
ya mwanzo ya kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu Katiba wanayoitaka. Pia
walishatoa Rasimu ya Kwanza ya Katiba na kukamilisha mchakato wa
Mabaraza ya Katiba. Kinachosubiriwa kwa hamu na sisi wote, ni Rasimu ya
Pili ya Katiba ambayo inatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 15 Desemba
2013 au kabla ya hapo.
Friday, November 08, 2013
HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE...!!!
Mheshimiwa Anne Makinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi;
Mheshimiwa Mizengo Pinda, Waziri Mkuu;
Waheshimiwa Mawaziri na Naibu Mawaziri;
Mheshimiwa Freeman Mbowe, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni;
Waheshimiwa Wabunge;
Mabibi na Mabwana;
Nakushukuru sana Mheshimiwa Spika kwa kukubali ombi langu na kutenga muda wenu ili niweze kuzungumza na Wabunge wa Bunge lako Tukufu kuhusu masuala muhimu kwa uhai, ustawi na maendeleo ya nchi yetu na watu wake.
Mheshimiwa Spika;
Nimeambiwa kuwa taarifa ilipotolewa kuwa ninaomba kuja kuzungumza na Waheshimiwa Wabunge, kumekuwepo na dhana mbalimbali. Wapo waliodhani kuwa nakuja kuzungumzia mchakato wa kuunda Katiba mpya na hasa matukio ya wiki chache zilizopita. Wapo waliodhani nakuja kuzungumzia "Operesheni Tokomeza".
Tena wapo waliokwenda mbali na kufikiria kuwa nakuja kuwakaripia Waheshimiwa Wabunge waliotoa maoni yao kuelezea kasoro zilizojitokeza katika utekelezaji wa Operesheni hii muhimu. Na wapo pia waliodhani ninakuja kuzungumzia ushiriki wa majeshi yetu ya Tanzania katika Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa nchini Kongo.
AZAM FC NA KOCHA WAKUBALI KUACHANA, YASEMEKANA JUMA KASEJA AMEJIUNGA YANGA
Taarifa za kipa nyota, Juma Kaseja kutua Yanga zimewachanganya watu wengi. Ingawa zimekuwa hazina uhakika, lakini Salehjembe imepata taarifa za uhakika kwamba mchana wa jana ndiyo amemalizana na Yanga. Lakini bado watu wamekuwa wakihaha kutaka kujua kuhusiana na suala hilo.
Mmoja wa viongozi wa Yanga alisema; "Sitaki kulizungumzia kwa sasa, kama kuna walioandika sawa, lakini kumalizana
kwetu na Juma ni leo (Alhamisi). Tulimpa mkataba, anao yeye, hivyo tutakutana na kumalizana na tumegawanya makundi mawili, moja litakuwa uwanjani katika mechi dhidi ya Oljoro na lingine katika ishu hiyo ya Kaseja."
Na Mahmoud Zubeiry
KOCHA Muingereza, Stewart John Hall ameamua kujiuzulu kufundisha klabu ya Azam FC baada ya kukubaliana na wamiliki wa timu hiyo na jana amewaaga wachezaji wa timu hiyo.
Stewart aliwaaga wachezaji na benchi la Ufundi mara tu baada ya mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya timu hiyo na Mbeya City ulioisha kwa sare ya kufungana mabao 3-3 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
KAMANDA WA M23 AJISALIMISHA UGANDA
Maafisa wa Serikali ya Uganda wanasema
kuwa kamanda wa kijeshi wa wapiganaji walioshindwa katika Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo, DRC, M23, amejisalimisha kwa utawala wa Uganda.
Ripoti kutoka Uganda zinasema kuwa mamia ya wapiganaji wamejisalimisha pamoja na kiongozi wao, Sultani Makenga.
Wapiganaji hao wamejisalimisha katika eneo la hifadhi ya Wanyama ya Pori ya Mgahinga, kwenye mpaka wa Uganda na DRC.
Mnamo Jumanne M23 walisema kuwa
wamesitisha maasi yao ya miezi 20 Mashariki mwa Congo, baada ya
kutimuliwa katika ngome zao Mashariki mwa Congo na wanajeshi wa Serikali
wakishirikiana na askari wa kudumisha amani wa Umoja wa Mataifa.
Hata hivyo serikali za Uganda na DRC hazijaweza kuthibitsha madai haya.
Mapema wiki hii, M23 ilisema kuwa
inamaliza uasi wake wa miezi kumi na tisa masaa chache baada ya majeshi
ya serikali kudai ushindi dhidi ya waasi hao.
Ripoti zinasema kuwa Sultani Makenga
na waasi wengine 1,700, wamesalimisha silaha zao na wanazuiliwa na jeshi
la Uganda katika kambi ya jeshi ya Mgahinga, karibu na mpaka na DRC.
Mapema wiki hii, maafisa wa DRC walisema Makenga alitoroka na kuingia Uganda au Rwanda.
Uganda imekuwa mwenyeji wa mazungumzo ya amani kati ya waasi na serikali ya DRC , ingawa hakuna mkataba wa amani umefikiwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)