Sunday, August 18, 2013

HII NDIO SABABU ILIYOFANYA AGNESS MASOGANGE KUSHTUKIWA NA POLISI NA HATIMAE KUKAMATWA NA UNGA AFRIKA KUSINI

Imebainika kwamba, Baada ya mpango madhubuti uliosukwa na wauza madawa ya kulevya hapa nchini wakishirikiana na baadhi ya watumishi wasio waaminifu wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam wa kuwasafirisha watuhumiwa hao Agnes Gerald maarufu kwa jina la Masogange na mwenzake Melisa Edward, mtandao huo ulikuwa pia umejipanga vyema nchini Afrika Kusini kuwapitisha watuhumiwa hao bila kukamatwa.

Kilichomponza Masogange kukamwatwa ni pale alipochelewa kutoka uwanjani hapo kutokana na kujiremba, kitu ambacho kilisababisha kufanyiwa upekuzi wa dharura na askari ambaye hakujua kuhusu mpango huo. Tembelea http://jambotz8.blogspot.com/ kila siku.

Taarifa zinabainisha kwamba, baada ya Masogange na wenzake kufanikiwa kupita katika maeneo ya ukaguzi ya uwanja wa ndege wa Oliver Tambo nchini Afrika Kusini, mwenzake waliyesafiri pamoja aliyetajwa kwa jina la Mangunga alifanikiwa kuondoka uwanjani hapo na mabegi matatu yenye jumla ya kilo 60 za madawa hayo ya kulevya bila kujulikana.

"Kilichomponza Masogange ni pale alivyokuwa anajiremba baada ya kuruhusiwa kupita katika vizuizi vyote. Kiuhakika hakukamatwa katika mashine, bali ulikuwa ni ukaguzi usio rasmi uliofanywa na Polisi. Nadhani huyu Askari aliyewashika hakujua kuhusu mpango huo." kilisema chanzo kimoja ndani ya jeshi la Polisi kama ilivyonukuliwa katika gazeti la Tanzania Daima la Tarehe 17/8/2013

NEWS OF RWANDA WAANDIKA KUWA RAIS JAKAYA KIKWETE ANAWEZA KUWA NA ASILI YA GITEGA BURUNDI....!!!

Jakaya Kikwete, president of Tanzania, answers questions at a press conference at the United Nations (UN) building in Addis Ababa, Ethiopia, during the 12th African Union (AU) Summit.
Mtandao wa News of Rwanda juzi umeandika makala yenye kichwa cha habari, ‘If President Kikwete is Tanzanian, then most Rwandans being expelled are Tanzanians too’ na kuandika kile linachodai kuwa Rais Kikwete anaweza kuwa na asili ya Burundi.    Kwa mujibu wa wazee wa Burundi waliohojiwa na mtandao huo, umedai Rais Kikwete anaweza kuwa na asili ya Giteka, Burundi.

“They are of Rwandan origin, but speak Kirundi and solely prefer to be viewed as Burundians. By virtual of that country’s laws, they are indeed Burundians,” limeandika. So where did President Jakaya Mrisho Kikwete come from? There are no original residents of Bagamoyo in Tanzania where Kikwete’s parents are traced. Most people from that area are remnants of slaves who were seem as unfit for the market during the slave trade era.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI AUGUST 18, 2013

KIWEWE, MATUMAINI WAOKOKA.....!!!

MSANII wa Kundi la Ze Komedi, Robert Augustino ‘Kiwewe’ na mwenzake Tumaini Martin ‘Matumaini’ wameamua kuacha anasa na kumrudia Mungu kwa kuokoka.
Wakizungumza na paparazi wetu kwa nyakati tofauti, wasanii hao walisema kilichosababisha kuchukua uamuzi huo kwa wakati mmoja ni kutokana na manzingira waliyolelewa tangu wakiwa wadogo, yaani kumjua Mungu.

“Niliamua kufanya uamuzi sahihi ambao naamini utanibadilishia maisha yangu kwa kiasi kikubwa, kwa kufuata mambo yanayompendeza Mungu na siyo starehe za ujana,” alisema Kiwewe huku akiungwa mkono na Matumaini. Wakabainisha kuwa wanasali kwa Mchungaji Josephat Gwajima.
Wasanii hao walisema, ili kuhakikisha wanaungana na Mungu katika kila jambo, wameamua kuanzisha kundi lao la muziki wa Injili, Comedians Gospel linaloundwa na wao pamoja na Mkono.

LIST YA VIGOGO MAFISADI WA ARDDHI HII HAPA....!!!

Getrude Lwakatare

WAMO DEWJI, LWAKATARE, RUTABANZIBWA

WABUNGE Mohamed Dewji wa Singida mjini na Mchungaji Getrude Lwakatare wote wa CCM pamoja na mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam Robery Mugishagwe wametajwa kuwa vinara wa uvamizi na uuzaji wa viwanja jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa, naye ametajwa kumkingia kifua mmoja wa wavamizi wa viwanja kwa kumuwekea dhamana alipofikishwa polisi.

Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Tereza Huviza ndiye aliyewataja vigogo hao jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira, iliyokwenda kutembelea ofisi za Baraza la Mazingira (NEMC).

Huvisa alikuwa akihofia kutaja majina ya vigogo hao, lakini Mwenyekiti wa kamati hiyo, James Lembeli, alimkasirikia na kumhoji ni nani hapa nchini aliye juu ya sheria kiasi cha kumfanya aogope kumtaja licha ya kuvunja sheria.

Lembeli alimtaka Waziri Huvisa kuyataja majina hayo kwani akiendelea kuwahofia watu wa aina hiyo, wataendelea na uvamizi huo na watakapofika 100 wenye tabia hizo nchi haitatawalika.

“Huna sababu ya kuogopa kuwataja watu waovu, kamati hii ina mamlaka kisheria…usihofie chochote, wataje tujue namna ya kuwashughulikia,” alisema Lembeli.

Shinikizo hilo la Lembeli liliungwa mkono na wajumbe wote wa kamati hiyo waliomuhakikishia usalama Waziri Huvisa aliyeonekana kuwa na hofu wakati akiulizwa maswali.


Baada ya kuhakikishiwa usalama, alianza kumtaja Dewji ambaye alisema anashinikiza kupewa eneo la ufukwe karibu na zilipo ofisi za ubalozi wa Urusi hapa nchini huku akijua ni kinyume cha sheria.

YANGA YAILAMBA KIMOJA AZAM, TAIFA JANA... SHUHUDIA MATUKIO YALIYOJILI KATIKA PICHA





Wachezaji wa Yanga wakiiibusu ngao ya jamii waliyotwaa baada ya kuifunga Azam bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa jana.

BIA YA TUSKER YAZINDUA SHINDANO LA 'TUSKER PROJECT FAME'....!!!


Meneja wa Bia ya Tusker kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti, Sialouise Shayo (katikati) akizungumza na wanahabari leo kuhusu  TUSKER PROJECT FAME. Kushoto ni Meneja Masoko Tusker, Anitha Msangi na  msanii mahiri Zahira Zoro.



Kutoka kushoto ni Anitha Msangi,  Sialouise Shayo, Mwanamuziki mahiri Zahira Zorro, na mzao wa Tusker Project Fame, Aneth Kushaba.



Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.

FOOLISH AGE YA LULU KUZINDULIWA MWISHO WA MWEZI HUU NDANI YA MLIMANI CITY


  Msanii mwenye kipaji cha Hali ya juu nchini na Mwenye umri mdogo Elizabeth Michael "LULU"anatarajia kuzindua filamu yake ya Kwanza tokea alipotoka Gerezani, Filamu hii iitwayo FOOLISH AGE ikiwa imetengezwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited itazinduliwa Mnamo tarehe 30 August 2013 Katika Ukumbi wa Mlimani city jijini Dar Es Salaam.

Filamu hiyo inayoelezea Maisha ya LULU ni moja ya filamu nzuri na yenye ubora wa hali ya juu kutokana na Kutengenezwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited Katika Uzinduzi huo wa Filamu hiyo ya Lulu Wasanii mbalimbali akiwemo mwanamuziki Lady Jaydee na Machozi Band anatarajiwa kushusha bonge moja la burudani ya kufa mtu.

ARSENAL YAANZA LIGI KWA KICHAPO, YAPUMZISHWA 3-1, BENTEKE NOMA!, LIVERPOOL, SOUTHAMPTON, FULHAM, WEST HAM ZACHINJA


Neat finish: Arsenal's Olivier Giroud, left, opens the scoringMtaalamu wa kufunga: Nyota wa Arsenal,  Olivier Giroud,  kushoto, akiandika kimiani bao la kwanza kwa Arsenal

 
Kikosi cha Arsenal: Szczesny 4; Sagna 5 (Podolski 90), Koscielny 5, Mertesacker 5, Gibbs 5 (Jenkinson 28, 5); Wilshere 6, Ramsey 5, Rosicky 6; Walcott 6, Chamberlain 6 (Cazorla 46, 5); Giroud 6. 
Wachezaji wa Akiba: Fabianski, Frimpong, Gnarby, Sanogo. Villa: Guzan 7, Lowton 7, Vlaar 7, Baker 6 (Clark 17, 7), Luna 7; El Hamadi 7, Westwood 7, Delph 8; Agbonlahor 7, Weimann 8 (Bacuna 88); Benteke 8

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...