Friday, December 27, 2013
HII HAPA NDIO SIRI YA PINDA KUNUSURIKA
*Katibu Umoja wa Wanawake aadhirika kikaoni
*Wabunge 178 waomba kikao na Kinana
KATIKA
hali isiyo ya kawaida, Ijumaa iliyopita Waziri Mkuu Mizengo Pinda
aliponea chupuchupu kung’olewa uenyekiti wa kikao cha wabunge wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM).
Kikao hicho (party caucus) kilifanyika baada ya hali ya hewa bungeni kuchafuka baada ya kuwekwa hadharani bungeni ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliyosomwa na Mwenyekiti wake James Lembeli.
Ripoti hiyo ilihusu tathmini ya upungufu kadha wa kadha uliojitokeza wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili, upungufu ulioibua mjadala mzito bungeni, na kusababisha mawaziri wanne kujiuzulu.
Mawaziri hao ni Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na David David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi). Hata hivyo habari zilizopatikana zilisema mawaziri hao waling’olewa kwa amri ya Rais Jakaya Kikwete.

Subscribe to:
Posts (Atom)