Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
amesikitishwa sana na uharibifu wa mazingira unaoendelea katika machimbo
ya mchanga Donge.
Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara Visiwani Unguja na jana alikuwa na ziara katika mkoa wa Kaskazini Unguja. Makamu wa Rais amesema hatua za haraka zichukuliwe ili kuokoa mazingira yasiendelee kuharibiwa.
Makamu wa Rais pia amewataka Viongozi
wote wa CCM kuhakikisha kuwa Chama kinajitegemea kwenye maeneo yao,
Makamu wa Rais aliyasema hayo mara baada ya kukagua shughuli za kiuchumi
za CCM katika ufukwe wa Nungwi ikiwa sehemu ya ziara yake aliyoifanya
kwenye mkoa wa Kaskazini Unguja.
Makamu wa Rais pia alifungua ofisi
mbili za CCM moja ikiwa ya jimbo la Donge na nyingine ikiwa Ofisi ya CCM
mkoa wa Kaskazini ambapo inahistoria ya kipekee kutokana na kuwekwa
jiwe la msingi mwaka 1986 na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere.