Msanii/Mtangazaji
Soggy Doggy ameacha mzigo pande za redio Uhuru na leo rasmi ameondoka Dar es
salaam nakwenda Iringa ambapo atakuwa akifanya kazi katika kituo kingine cha
Redio kinachoenda kwa jina la Ebony Fm.Soggy Doggy ashawahi kufanya kazi katika
vituo vya redio mbalimbali hapa nchini kama Arusha na Mwanza.
Friday, March 01, 2013
Mtendaji mkuu TAZARA Bw. Akashambatwa Mbikusita-Lewanika aachia ngazi.
Mtendaji
Mkuu wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Bw. Akashambatwa
Mbikusita-Lewanika,(Pichani) hatimaye ameachia ngazi baada ya kuendesha
kampeni kali ya miezi kadhaa kutaka aendelee kuongoza Mamlaka hiyo kwa
miaka mingine mitatu.
Hatua
hiyo ya kuachia ngazi imekuja baada ya Bodi ya Wakurugenzi na Baraza la
Mawaziri la Mamlaka hiyo kuonyesha dhahiri kutotaka Mzambia huyo
aendelee na uongozi wa TAZARA kutokana na utendaji wake mbovu na uongozi
mbaya uliowabagua wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kwa misingi ya utaifa
wao.
Habari
za ndani za Mamlaka hiyo zimesema Bw. Akashambatwa ambaye kipindi chake
cha uongozi kiliisha tarehe 22 Januari, 2013 kiliongezwa kwa maombi
maalum ya Serikali ya Zambia kwamba Serikali hiyo ilihitaji muda mrefu
kidogo kumpata mbadala wake, licha ya Serikali ya Tanzania
kutoridhishwa na utendaji wake.
Katika
kikao chake cha tarehe 20 Februari, 2013 jijini Lusaka, Zambia, Baraza
la Mawaziri lilijadili kwa siri na kwa kirefu suala la mtendaji Mkuu
huyo ambaye inasemekana aliombewa tena na Serikali ya Zambia kipindi cha
nyongeza, ombi ambalo inadaiwa lilipingwa vikali na ujumbe wa Serikali
ya Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe.
Taarifa
za uhakika ndani ya Wizara ya Uchukuzi zinasema Serikali ya Tanzania
haikumtaka Mtendaji Mkuu huyo kwa sababu kadhaa zikiwemo :uwezo mdogo,
ubadhirifu, kuchochea ubaguzi kati ya Watanzania na Wazambia, ukaidi na
uchochezi. Inadaiwa kuwa Mtendaji Mkuu huyo alizuia kuanzishwa kwa mradi
wa usafiri jijini Dar es Salaam bila sababu yoyote ya msngi na kuishia
kusambaza taarifa za uongo na uchochezi Zambia na magazeti mbalimbali
nchini.
Tarehe
25 Februari, 2013 Gazeti la kila siku la Zambia, Zambia Daily Mail,
liliripoti tukio hilo la kuachia ngazi kwa kiongozi huyo ambaye
anajulikana sana nchini Zambia kama mfanyabiashara na kiongozi wa kimila
(chief),
Gazeti
hilo lilinukuu barua ya Bw. Akashambatwa ya tarehe 22 Februari, 2013
kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Ujenzi, Ugavi na
Mawasiliano ya Zambia, akielezea kuwa hakuna faida ya kuomba kurefushwa
kwa mkataba wake wakati vyombo vikuu vya uongozi vya TAZARA, Bodi ya
Wakurugenzi na Baraza la Mawaziri, havionyeshi kumkubali.
Kuondoka kwa Bw. Akashambatwa kwenye uongozi wa TAZARA kunatarajiwa kupokewa na wafanyakazi wa TAZARA kwa nderemo na vifijo.
Google Waja na Miwani Inayopiga na Kurekodi Picha kwa Maelekezo.
TEKNOLOJIA waliyotumia
Google kutengeneza miwani ambayo ina uwezo wa kumpiga picha mtu au
kurekodi bila muhusika kujua (google glass) sio mpya ila Kampuni ya
Google ndio wakwanza kuja na teknoloji hiyo, ili kila mtu aweze kutumia
na inakadiriwa huwenda bidhaa hii ikafanya vizuri sana katika mauzo.
Google
glass ni rahisi sana kutumia, kama unataka kupiga picha unachotakiwa
kusema ni “OK Glass, take a picture.” upo kwenye foleni unaona fujo
unataka kuchukua video, mwambie Google Glass naye atakusaidia kuchukua
video. Hii ndio kali, unataka kuwaonyesha ndugu na marafiki kitu
unachokiona wakati huo huo? Google glass inafanya yote hayo, inakuja na
kitu kama “Skype-style video chat”.
Umesafiri
kwenda kuchukua mzigo China? Google glass itakusaidia kuchukua
kutafsiri lugha. Umeenda Zanzibar kutembelea majengo ya kitalii na
unabaki kushangaa shangaa, uliza Google glass na itakupa tour guide.
Google
glass ni kifaa ambacho unaweza kutumia kurekodi video, kupiga picha,
kutafuta habari katika Google, kutafsiri lugha, na unaweza fanya yote
haya bila kutumia mikono yako (hands free). Tatizo ni kwamba, ukishavaa
hiki kifaa kama miwani, watu hawajui kama unawarekodi kwenye video au
vipi, na kwa wabongo walivyo wanavyojua kujihami kupigwa picha au
kurekodiwa kwenye video, ukivaa Google glass unaweza tolewa baa.
Kwa
nchini Tanzania kifaa hiki ambacho kitakuwa na wastani wa bei ya sh.
mil 2. 2 ($1500). Hata hivyo kifaa hicho kinachovaliwa kama miwani,
sijui kama utaweza kutembea nacho hata hatua kumi kabla ya vibaka
kukuvaa baada ya kujua thamani yake. Tusubiri Google wakiwezeshe kifaa
hiki kiweze elewa kiswahili ndio na sisi tutakifaidi zaidi kwani hapa
hamna kubonyeza bonyesha ni kuongea tu. Je ukipata Google glass utatumia
kifaa hiki cha kisasa kufanyia nini? Acha maoni yako.
*Imeandaliwa na www.thehabari.comRais Kagame wa Rwanda akanusha kuwa na nia ya kugombea tena urais kwa awamu ya tatu.
Rais
Paul Kagame wa Rwanda amesema hana mpango wa kugombea tena muhula wa
tatu madarakani baada ya muhula wake wa sasa kumalizika mwaka 2017.
Akizungumza
mjini Kigali, rais Kagame amevishutumu vyombo vya habari kuanzisha
mjadala juu ya iwapo ataibadili katiba ili aweze kuwania muhula
mwingine.
Mjadala
huo ulifuatia hatua ya rais huyo mapema mwezi huu kuunda kamati katika
chama chake, kutafakari mwelekeo wa nchi baada ya muda wake madarakani
kumalizika.
Chama
cha upinzani cha FDU-Inkingi, kimetoa tangazo kikilaani njama zozote za
kuifanyia marekebisho katiba ili kuruhusu muhula wa tatu kwa rais.-DW
Hivi ndivyo Chadema walivyotikisa Mbeya jana
Mapokezi makubwa ya Mh. Freeman Mbowe katika viwanja vya Rwanda Nzovwe jijini Mbeya.
Burudani mbalimbali pia zilikuwepo
Mh. Mbowe pia alimtaka waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi kujiudhuru pamoja na naibu waziri wa wizara hiyo kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne na kusema kuwa katika siku 14 alizozitoa zimebaki siku tatu za wao kuendelea kuwepo madarakani na kuongeza kuwa wasipofanya hivyo wataitisha maandamano ya nchi nzima kushinikiza waondolewe katika nafasi hizo. Mara baada ya kauli hiyo Mbowe aliwataka wananchi kuchangia fedha kwaajili ya wahanga siku ya maandamano ambapo zilichangishwa fedha kiasi cha sh. 3, 267, 550/=
Wakichangisha
fedha kwaajili ya wahanga wa maandamano yatakayofanyika pindi mawaziri
wataposhindwa kujiudhuru picha ya kwanza ni Mh. Sirinde, inayofuata ni
Mh. Msingwa na ya mwisho ni Mh. Mbowe.
Picha na Keny Pino
JOKETI KUPAMBA UZINDUZI KAMPENI YA UNYANYASAJI
Na Mwandishi
wetu
MWANAMITINDO
nyota nchini, Joketi Mwegelo, anatarajiwa kunogesha uzinduzi wa kampeni ya kupinga
unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto kike, unaotarajiwa kufanyika
keshokutwa, ambapo shughuli mbalimbali na mada zitatolewa.
Joketi, ambaye anawika katika tasnia mbalimbali nchini ikiwemo urembo, mitindo, muziki na filamu, atashiriki kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo ijulikanayo kama Okoa Mtoto wa Kike Tanzania utakaofanyika katika Kata ya Nyamongo wilayani Tarime, Mara.
Taarifa ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyumbani Kwanza Media Group iliyoandaa kampeni hiyo, Mossy Magere, imesema kuwa maandalizi yote muhimu yamekamilika na Joketi atawasili wilayani Tarime kesho tayari kwa kushiriki na atatoa mada ya masuala ya ujasiriamali kwa washiriki wa tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa.
Mossy alisema kuwa mbali na Joketi, wasanii mbalimbali watashiriki kutoa burudani wakiwemo wasanii nyota wa bongo fleva na wale wa asili wanaotamba mkoani Mara.
'Maandalizi yote ya msingi yamekamilika na kinachosubiriwa ni muda wa uzinduzi ufike, Joketi anatarajiwa kuwasili hapa kesho tayari kwa kushiriki nasi. Atapata fursa ya kutoa mafunzo na mbinu
za
kimaisha kwa washiriki ambao wengi ni wanafunzi wa shule mbalimbali wilayani
hapa,' alisema Mossy.
Kampeni hiyo ambayo itadumu kwa kipindi cha miezi sita, itazinduliwa rasmi keshokutwa na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, ambaye ameshirikishwa kwa karibu na Kampuni ya Nyumbani Kwanza.
Alisema mchakato wa uundwaji wa klabu za wapinga unyanyasaji katika shule mbalimbali za sekondari wilayani Tarime ambapo kampeni hiyo inaanzia umekamilika na wanafunzi wamevutiwa na kujiunga kwa wingi kwenye klabu hizo ambazo zitakuwa kichocheo cha kuendeleza kampeni hiyo.
Mossy aliongeza kuwa, uundwaji wa klabu hizo unalenga kukiwezesha kizazi cha sasa na kijacho kuwa mstari wa mbele kukataa vitendo vya unyanyasaji.
“Kila jambo jema huanzia ngazi za chini, kwa sasa tunaendelea kuunda klabu za wapinga unyanyasaji ambazo zitakuwa zikipewa mafunzo na mbinu mbalimbali ili kuwajenga kufahamu madhara wakiwa wangali wadogo shuleni.
Subscribe to:
Posts (Atom)