Friday, March 09, 2018

TRUMP AKUBALI MUALIKO WA KUKUTANA NA RAIS WA KOREA KASKAZINI

Rais Donald Trump wa Marekani amekubali ombi la Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un la kutaka wakutane mapema ndani ya mwezi mei mwaka huu, na hivyo kuweka historia kufuatia kuwa kutokuwepo rais wa Marekani ambaye amewahi kuonana na kiongozi mkuu wa Korea kaskazini.

Hata hivyo mahala watakapokutana viongozi panasalia kuwa siri kwa sasa, na pia Marekani imesisitiza kuwa pamoja na kukubali ombi hilo la rais Kim Jong Un laini bado vikwazo vitasalia pale pale.

Tangazo hilo la kwamba rais Trump amekubali kukutana na Kim Jong Un, limetolewa na viongozi wa juu wa Korea Kusini uliofika mjini Washington kuwasilisha barua ya ombi hilo kutoka kwa Korea Kaskazini.

KENYATTA, ODINGA WAKUTANA IKULU, WAKUBALIANA JAMBO

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekutana na kiongozi wa muungano wa upinzani nchini humo Raila Odinga katika ofisi yake Jumba la Harambee, Nairobi.

Mkutano huo umefanyika muda mfupi kabla ya Bw Kenyatta kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson.

Marekani imekuwa ikihimiza kufanyika kwa mazungumzo na mashauriano kutatua mzozo wa kisiasa uliokumba taifa hilo baada ya uchaguzi uliojaa utata mwaka jana.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...