Wednesday, May 21, 2014

MELI YA KIKWETE KUKAMILIKA 2016

http://jambotz8.blogspot.com/
Siku kama ya leo mwaka 1996, ilikuwa ni vilio kila kona ya nchi, lakini Kanda ya Ziwa iliathirika zaidi na kuzama kwa meli ya Mv Bukoba na kuteketeza mamia ya wananchi.
Kuzama kwa Mv Bukoba inaelezwa ni kutokana na kuwa ubovu. Tukio hilo ambalo haliwezi kufutika vichwani mwa wakazi wa Kanda ya Ziwa, lakini kilio chao cha kupatiwa meli mpya licha ya Rais Jakaya Kikwete kuahidi Serikali kununua mwaka 2010, haijanunuliwa hadi sasa.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa ujenzi wa meli hiyo mpya iliyoahidiwa na Rais Kikwete kwa Ziwa Victoria unatarajia kukamilika mwaka 2016.
Akizungumza ofisini kwake wiki hii, Ofisa Masoko wa Huduma za Meli Mwanza Obedi Nkongoki alisema mjenzi wa meli hiyo Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Denmark (Danida) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.
http://jambotz8.blogspot.com/
“Ujenzi huu unahusisha meli nne ingawa Rais aliahidi tatu; Ziwa Victoria moja, mbili Ziwa Tanganyika na nyingine Ziwa Nyasa ambazo zinatarajiwa kukamilika 2018, huku ya Ziwa Victoria ikitarajiwa kukamilika 2016,” alisema Nkongoki. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MEI 21, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.


.

.

.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

VIFO VYA BOMU NIGERIA VYAFIKIA 118

Maafisa nchini Nigeria wamesema kuwa wamepata maiti 118 kufuatia shambulio la bomu katika mji wa Jos.
Mabomu mawili yalilipuka mojawepo ikiwa imefichwa ndani ya gari na kulipuka katika soko moja kubwa. Dakika 20 baadaye mlipuko wa pili ulitokea karibu na hospitali.
Inahofiwa kuwa kuna maiti zaidi zilizonaswa kwenye vifusi vya majengo yaliyo poromoka kutokana na shambulio hilo.
Kufikia sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo lakini wengi wanaamini kuwa Kundi la wapiganaji wa kiislamu la Boko Haram lilihusika.
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amejitokeza kukemea mashambulio hayo na kusema kuwa amejitolea kuangamiza kabisa ugaidi. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Na BBC Swahili

JESHI LA KENYA LAWASHAMBULIA AL-SHABAAB

Wanajeshi wa Kenya wanaendelea kukabiliana na Al Shabaab Somalia
Jeshi la Kenya limeishambulia ngome ya Al Shabab ya Jilib huko Somalia.
Katika mahojiano na BBC, msemaji wa Jeshi la Kenya Willy Wesonga amesema kuwa oparesheni hiyo kutoka angani imefaulu kuwaangamiza baadhi ya wakuu wa Al Shabab.
Ngome hiyo inadaiwa kuwa eneo ambapo wapiganaji hao wa kiislamu wanafanya mazoezi na mikutano yao.
Kikosi cha Kenya kinadai kuishambulia ngome hiyo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wakaazi wa wilaya hiyo ya Jilib.
Wapiganaji wa Al shabab wamezidisha mashambulio nchini Kenya tangu nchi hiyo iingize wanajeshi wake ndani ya Somalia kuwasaka wapiganaji hao haramu mwaka wa 2011
Wesonga anasema jeshi la Kenya linalishambulia Al shabaab kama sehemu ya vita vikuu duniani dhidi ya ugaidi, na pia kuwazuia wafuasi wa kundi hilo kutekeleza mipango yao, yanayohatarisha usalama wa kieneo.
Hayo yanajiri wakati kundi la Al Shabab likidai kufanya shambulizi huko Mandera na kuwaua maafisa wa usalama wa Kenya. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Na BBC Swahili

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...