Siku kama ya leo mwaka
1996, ilikuwa ni vilio kila kona ya nchi, lakini Kanda ya Ziwa
iliathirika zaidi na kuzama kwa meli ya Mv Bukoba na kuteketeza mamia ya
wananchi.
Kuzama kwa Mv Bukoba inaelezwa ni kutokana na kuwa
ubovu. Tukio hilo ambalo haliwezi kufutika vichwani mwa wakazi wa Kanda
ya Ziwa, lakini kilio chao cha kupatiwa meli mpya licha ya Rais Jakaya
Kikwete kuahidi Serikali kununua mwaka 2010, haijanunuliwa hadi sasa.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa ujenzi wa meli hiyo
mpya iliyoahidiwa na Rais Kikwete kwa Ziwa Victoria unatarajia
kukamilika mwaka 2016.
Akizungumza ofisini kwake wiki hii, Ofisa Masoko
wa Huduma za Meli Mwanza Obedi Nkongoki alisema mjenzi wa meli hiyo
Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Denmark (Danida) kwa kushirikiana
na Serikali ya Tanzania.
“Ujenzi huu unahusisha meli nne ingawa Rais
aliahidi tatu; Ziwa Victoria moja, mbili Ziwa Tanganyika na nyingine
Ziwa Nyasa ambazo zinatarajiwa kukamilika 2018, huku ya Ziwa Victoria
ikitarajiwa kukamilika 2016,” alisema Nkongoki. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Alisema meli mpya itakuwa na kasi kwa kutumia saa
tano kwenda Bukoba na kurudi Mwanza, itakuwa ikifanya kazi mchana badala
ya usiku pekee, ikibeba wastani wa abiria ni 500 na tani 56 za mizigo.
Gharama hazitakuwa kubwa zaidi na haitakuwa tofauti na mabasi ila
zitazingatia soko na bei ya mafuta,” alisema Nkongoki na kuongeza:
“2016 itapatikana meli mpya, hapo tutaanza
ukarabati wa meli za Serengeti na Victoria, baadaye tutaifanyia
ukarabati meli ya Umoja, ambao utaziweka katika hali nzuri na
zitakazokwenda na wakati. Tunalenga kujiimarisha kiuchumi kwa nchi za
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo, Uganda, Zambia, Rwanda na
Malawi.”
Alisema meli zinazohudumu zilitengenzwa mwaka 1938
na kwamba, ambayo inaonekana mpya ni ya mwaka 1988, hivyo wamekuwa na
uzoefu wa mabadiliko ya meli kulingana na hali ya hewa.
“Hivyo tuna uhakika wa kuepuka ajali, kwani
tunajitahidi kufanya ukaguzi mara kwa mara. Pia, tunaajiri wataalamu
wenye taaluma ili kuimarisha usalama wa abiria na mali zao,” alisema.
Victoria hivi sasa inabeba abiria 1,200 na tani
200 za mizigo, huku Serengeti ikibeba abiria 593 na tani 350 za mizigo.
Hivyo ujio wa meli mpya na ukarabati wa meli zilizopo unatazamiwa kuwa
ni mkombozi kwa usafiri Ziwa Victoria. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment