Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeomba
kuongezewa muda wa mwezi mmoja kutokana na ugumu wa kazi ya uchambuzi wa
maoni yaliyotolewa na wananchi na asasi mbalimbali.
Tume hiyo inayoongozwa na Jaji Joseph
Warioba ilitakiwa kufanya kazi kwa miezi 18 kwa mujibu wa Sura ya 83 ya
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Maana yake ni kuwa Tume hiyo iliyoanza kazi Mei 1, mwaka jana ilitakiwa kukamilisha kazi yake Novemba 1, mwaka huu.
Ikiwa maombi hayo ya Tume yatakubaliwa ina maana watatakiwa kukabidhi ripoti yake Desemba 1, mwaka huu.
Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji
Augustine Ramadhan aliliambia gazeti hili kwa simu jana kuwa wamepeleka
serikalini maombi ya kuongezewa muda wa kufanya kazi.