Saturday, March 23, 2013

MAKALIO YANGU HUNIFANYA NIKOSE AMANI MTAANII".....AGNESS MASONGANGE



VIDEO Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ambaye muda mwingi amekuwa akiishi Afrika Kusini ameelezea jinsi maisha ya Bongo yalivyomchosha huku usumbufu anaopata kutokana na makalio yake makubwa ikiwa moja ya sababu. 

Akipiga stori mwandishi wetu, Masogange alisema umbile lake hilo limekuwa likimfanya akose amani anapokatiza mitaani, tofauti na Sauzi ambako wanawake wengi wamefungashia huku yeye akionekana ‘cha mtoto’.

“Muda mwingi niko Sauzi, Bongo miyeyusho na hili umbo langu nimekuwa nikisumbuliwa sana na wanaume lakini Sauzi hili langu la kawaida, wengi wamefungashia ile mbaya, kwa hiyo muda mwingi nitakuwa huko, huku nitakuwa nakuja na kuondoka,” alisema Masogange.

HATIMA YA HUKUMU SHEIKHE PONDA KUJULIKANA APRIL 18 MWAKA HUU.


Dar es Salaam. 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Aprili 18, mwaka huu inatarajiwa kutoa hukumu katika kesi inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda (55) na wenzake 49.

Mbali na kupangwa kwa tarehe ya hukumu hiyo, Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa jana aliutaka upande wa mashtaka na utetezi kuwasilisha hoja zao kama washtakiwa hao watakuwa na hatia ama la, Aprili 3, mwaka huu.
Juzi wakati Sheikh Ponda akijitetea aliieleza mahakama hiyo, kuwa yeye hana nyaraka za umiliki wa Kiwanja cha Malkazi Chang’ombe bali historia ya eneo hilo inawafanya wao kuwa wamiliki.
Sheikh Ponda na wenzake hao 49, wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kuingia kwa jinai, kuvamia ardhi inayomilikiwa na Kampuni ya Agritanza Ltd kwa nia ya kujimilikisha isivyo halali, wizi wa mali yenye thamani ya Sh 59.6 milioni na uchochezi.
Akijitetea dhidi ya mashtaka hayo, Sheikh Ponda, akiongozwa na wakili wake, Juma Nassoro, alidai kuwa awali kiwanja hicho kilikuwa kinamilikiwa na Taasisi ya Jumuiya ya Kiislamu ya East African Muslim Welfare Society (EAMWS) ambayo ilivunjwa na Serikali mwaka 1958 na Serikali kuunda chombo kingine kilichosajiliwa kama Bakwata.
Alidai kuwa Bakwata iliundwa ili kusimamia shughuli zilizokuwa zikiendeshwa na Taasisi ya Jumuiya ya Kiislamu ya East African Muslim Welfare Society na siyo mali kama majengo, viwanja na hata shule.
“Tulitumia njia ya mazungumzo ya kidiplomasia kurejesha kiwanja cha Malkazi Chang’ombe kwa kuzingatia kuwa itatatua mgogoro huo katika njia nyepesi” alidai Sheikh Ponda.
Alidai Sheikh Ponda.Nyerere sasa tusilete mijadala isiyokuwepo.”
Hata hivyo, Sheikh Ponda alikubali kuwa yeye ni miongoni mwa watu waliohusika kutoa taarifa kwa maimamu wa misikiti mbalimbali kuwaeleza waumini wao kushiriki kujitolea katika ujenzi wa msikiti wa muda uliojenga katika eneo la Malkazi Chang’ombe Oktoba 11 na kukamilika Oktoba 14, mwaka jana.
Alidai kuwa walijenga msikiti huo baada ya kufanya makubaliano na mmoja wa wamiliki wa Kampuni ya Agritanza Ltd, Hafidhi, na kukubaliana kuweka alama ambayo kila Muislamu akiiona ataiheshimu na kutofanya shughuli zake binafsi katika eneo hilo na kupendekeza kujenga msikiti huo wa muda.
Kuhusu kukamatwa kwake.
Sheikh Ponda alidai kuwa yeye alikamatwa Oktoba 16, 2012, nyakati za saa 4 kasoro usiku alipokuwa akijiandaa kuingia katika Msikiti wa Tungi Temeke , akipanda ngazi alitokea mtu mmoja aliyekuwa kwenye gari nyeusi aina ya Toyota Harrier akimtaka amfuate.

MIKATABA 17 KUSAINIWA NA RAIS WA CHINA WAKATI WA ZIARA YAKE HAPA NCHINI

Na Eeuteri Mangi na Hussein Makame - Maelezo
Rais wa Jamuhuri ya watu wa China Xi Jinping anataraija kuanza ziara ya kihistoria nchini tangu kuapishwa  kwake kuitumikia  nchi hiyo ambapo katika ziara hiyo atasaini mikataba 17 ya ushirikiano wa  kiuchumi kati ya Serikali za Tanzania na nchi hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe alisema kuwa  ziara hiyo ni ya kwanza barani Afrika  kwa Rais huyo mpya wa China baada ya kuchaguliwa kuliongoza taifa hilo Machi 14 mwaka huu.
Lengo la ziara hiyo ambayo itaanza tarehe 24 hadi 25 Machi mwaka huu ni kukuza uwekezaji  na biashara baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.
Baadhi ya Mikataba hiyo itahusiana na uboreshaji wa sekta ya viwanda, kilimo hasa cha tumbaku ikiwemo kuwatafutia soko wakulima kutoka mikoa ya Tabora na Ruvuma ili waweze kuuza zao hilo katika soko la China.
Waziri Membe alisema kuwa; “Mikataba mingine ni ya kulipatia Shirika la Utangazaji Tanzania zana za kufanyia kazi na kuandaa mazingira ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo itakayounganishwa na reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), reli ya kati na barabara”.  
Rais Xi Jinping pia atazindua na kukabidhi rasmi kituo cha Mikutano cha  Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere  chenye ghorofa tatu na kumbi nne za mikutano  zenye uwezo  kupokea washiriki zaidi ya 1800 kilichogharimu dola za kimarekani milioni 29.7 zilizotolewa na Serikali ya China kwa lengo la kumuenzi Mwalimu Nyerere.
Waziri huyo alisema kuwa baada ya kufika nchini Rais Xi Jinping atazungumza na mwenyeji wake Rais Dk. Jakaya Kikwete pamoja na Viongozi Waandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadaye atahudhuria dhifa ya kitaifa Ikulu Jijini Dar es salaam.
Siku ya pili ya ziara yake Rais Jinping  atazungumza rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Ali Mohamed Shein pamoja na ujumbe wa viongozi waandamizi kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri Membe aliongeza kuwa Rais Jinping atatoa hotuba maalumu kwa Tanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla na  kuzungumzia sera ya Serikali mpya ya China kwa bara la Afrika ambayo itahudhuriwa na watu kutoka kada mbalimbali ikiwemo Viongozi na Maafisa Waandamizi wa Serikali, Wahadhiri wa Vyuo Vikuu,Wabunge, Viongozi wa Dini na Asasi za Kiraia na Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali.
“Hotuba hiyo ya Rais wa China ataitoa kwa lugha ya Kichina na kutafsiriwa  kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili ili iweze kuifika dunia nzima, hivyo tunaviomba vyombo vya habari nchini vichukue fursa hiyo kuwa vya kwanza kuutangazia Ulimwengu” alisema Waziri Membe.
Ziara hiyo ya Rais wa Jamhuri ya Watu wa China  ni muendelezo wa uhusiano mzuri kati ya nchi hiyo na Tanzania ulioasisiwa na viongozi  wa mataifa hayo mawili, yaani Mao Zedong wa China na  Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania.
Rais Jinping ataondoka nchini Machi 25 saa 10:40 jioni kuelekea nchini Afrika Kusini kuhudhuria mkutano wa tano wa Wakuu wa Nchi zinazokuwa kwa kasi kiuchumi ambazo ni Brazil, Urusi, India, China na Afrika ya Kusini (BRICS). 

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA MBEYA IMEPIGA MARUFUKU MAANDAMANO YALIYOPANGWA NA CHADEMA TAREHE 25 MACHI MWAKA HUU

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dk. Norman Sigalla




KAMATI ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya limepiga marufuku maandamano yoyote kufanyika Mkoani hapa yenye lengo la kushinikiza Raisi Kikwete kumfukuza kazi Waziri wa Elimu kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne.
  
Maandamano hayo yalipangwa kufanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA)  Machi 25, Mwaka huu, ambayo yamepangwa kuhusisha Mikoa yote ya Nyanda za Juu Kusini na kufanyika Jijini Mbeya kwa lengo hilo.
Akitoa taarifa ya Kamati hiyo kwenye Mkutano wa ushauri wa Mkoa (RCC),Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dk. Norman Sigalla amesema kamati hiyo ilikaaa Machi 19, mwaka huu na kuamua kuwa hakuna mantiki ya kufanyika kwa maandamano hayo.
  
Amesema sababu iliyoonekana ni kwamba tayari tume imeshaundwa kuchunguza madai hayo hivyo hamna sababu ya watu kuandamana kushinikiza waziri kujiuzulu ili hali kamati itakuja na majibu juu ya kile kilichosababisha matokeo kuwa mabaya.
  Sigalla amesema kamati ya Ulinzi na Usalama imeona kuwa kuendelea kufanya maandamano soyo ufumbuzi wa matatizo bali yataathiri shughuli za kujitafutia kipato kwa wananchi wa kawaida pamoja na usalama wa mali.
  
Ameongeza kuwa usalama wa Wananchi wa Mkoa wa Mbeya utaathirika kutokana na wanaotarajiwa kufanya maandamano hayo wamehamasishwa kutoka mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma  ambako kutajaza idadi kubwa ya watu.

Amesema kamati pia inaamini kuwa maandamano ya aina hiyo yanaweza kusababisha  uvunjifu wa amani hivyo kamati inapiga marufuku maandamano ya aina yoyote kufanyika Mkoani Mbeya na kuongeza kuwa yapelekwe maeneo mengine.
  
Aidha ametoa rai kwa vikundi vya kisiasa, kijamii na vikundi vya dini kuweka mbele maslahi ya wananchi kwa kuhimiza kujitafutia vipato kutokana na fursa za maendeleo zilizopo.
  
Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa kamati ya Ulinzi na Usalamaya Mkoa ameviagiza vyombo vyote vya Ulinzi na usalama kuendelea kuhakikisha kwamba Mkoa wa Mbeya unaendelea kuwa tulivu na amani ambayo itawezesha wananchi kuendelea na shughuli za kujiongezea kipato bila bugudha yoyote.
Maandamano hayo yamepangwa kufanyika Machi 25, Mwaka huu kufuatia Mkutano wa Hadhara uliofanyika hivi karibuni wa Chadema katika Viwanja vya Shule ya Msingi RuandaNzovwe Ilomba Jijini Mbeya Februari 28, Mwaka huu, ambapo Mwenyekiti wa Chama hicho taifa Freeman Mbowe aliagiza kufanyika kwa maandamano hayo kwa namna yoyote ile.
  Pia katika kuhakikisha dhana hiyo inatimia Mwenyekiti huyo pia alichangisha zaidi ya Shilingi Milioni Tatu ambazo alidai kuwa zitasaidia wakati wa maandamano katika kununulia maji ya kunawa baada ya kupigwa na mabomu pia kununulia dawa za huduma ya kwanza kwa watakaoathirika na maandamano hayo.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...