Na
Eeuteri Mangi na Hussein Makame - Maelezo
Rais wa Jamuhuri ya watu wa China Xi Jinping
anataraija kuanza ziara ya
kihistoria nchini tangu kuapishwa kwake kuitumikia nchi hiyo ambapo
katika ziara hiyo atasaini mikataba 17 ya ushirikiano wa kiuchumi kati
ya
Serikali za Tanzania na nchi hiyo.
Akiongea
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje
na
Ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe alisema kuwa ziara hiyo ni ya
kwanza barani Afrika kwa Rais huyo mpya wa China baada ya kuchaguliwa
kuliongoza taifa hilo Machi 14 mwaka huu.
Lengo
la ziara hiyo ambayo itaanza tarehe 24 hadi 25 Machi mwaka huu ni kukuza
uwekezaji na biashara baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya
Watu wa
China.
Baadhi
ya Mikataba hiyo itahusiana na uboreshaji wa sekta ya viwanda, kilimo
hasa cha
tumbaku ikiwemo kuwatafutia soko wakulima kutoka mikoa ya Tabora na
Ruvuma ili
waweze kuuza zao hilo katika soko la China.
Waziri
Membe alisema kuwa; “Mikataba mingine ni ya kulipatia Shirika la
Utangazaji
Tanzania zana za kufanyia kazi na kuandaa mazingira ya ujenzi wa bandari
ya
Bagamoyo itakayounganishwa na reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), reli
ya kati
na barabara”.
Rais
Xi Jinping pia atazindua na kukabidhi rasmi kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere chenye ghorofa tatu na kumbi
nne za mikutano zenye uwezo kupokea washiriki zaidi ya 1800
kilichogharimu dola za kimarekani milioni 29.7 zilizotolewa na Serikali
ya
China kwa lengo la kumuenzi Mwalimu Nyerere.
Waziri
huyo alisema kuwa baada ya kufika nchini Rais Xi Jinping atazungumza na
mwenyeji wake Rais Dk. Jakaya Kikwete pamoja na Viongozi Waandamizi wa
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadaye atahudhuria dhifa ya
kitaifa
Ikulu Jijini Dar es salaam.
Siku
ya pili ya ziara yake Rais Jinping atazungumza rasmi na Rais wa
Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Ali Mohamed Shein pamoja na
ujumbe
wa viongozi waandamizi kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri
Membe aliongeza kuwa Rais Jinping atatoa hotuba maalumu kwa Tanzania,
Afrika na
Dunia kwa ujumla na kuzungumzia sera ya Serikali mpya ya China kwa bara
la Afrika ambayo itahudhuriwa na watu kutoka kada mbalimbali ikiwemo
Viongozi
na Maafisa Waandamizi wa Serikali, Wahadhiri wa Vyuo Vikuu,Wabunge,
Viongozi wa
Dini na Asasi za Kiraia na Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali.
“Hotuba
hiyo ya Rais wa China ataitoa kwa lugha ya Kichina na kutafsiriwa kwa
lugha ya Kiingereza na Kiswahili ili iweze kuifika dunia nzima, hivyo
tunaviomba
vyombo vya habari nchini vichukue fursa hiyo kuwa vya kwanza kuutangazia
Ulimwengu” alisema Waziri Membe.
Ziara
hiyo ya Rais wa Jamhuri ya Watu wa China ni muendelezo wa uhusiano
mzuri
kati ya nchi hiyo na Tanzania ulioasisiwa na viongozi wa mataifa hayo
mawili, yaani Mao Zedong wa China na Mwalimu Julius Nyerere wa
Tanzania.
Rais
Jinping ataondoka nchini Machi 25 saa 10:40 jioni kuelekea nchini Afrika
Kusini
kuhudhuria mkutano wa tano wa Wakuu wa Nchi zinazokuwa kwa kasi kiuchumi
ambazo
ni Brazil, Urusi, India, China na Afrika ya Kusini (BRICS).
No comments:
Post a Comment