JIJI la Arusha limeendelea kujijengea sifa ya kuwa moja ya maeneo yenye vituko, kufuatia kijana mmoja mkazi wa eneo la Phillips, kata ya Sekei jijini humo, Hamad Rashid (32) kukamatwa leo akiiba kiti (stuli) kinachotumika kuwekea mwenge wa Uhuru wakati mwenge ukiwa katika mbio zake mkoani Arusha.
Tukio la kuiba na kisha kukamatwa limetokea jana saa 11 jioni katika eneo la Sanawari Mataa eneo lililopangwa kwaajili ya mkesha wa mwenge huo baada ya kukamilisha mbio zake na kazi ya kuweka mawe ya msingi na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas ameithibitishia Nkoromo Blog kutokea tukio hilo na kwamba mtuhumiwa huyo alikamatwa na polisi waliokuwa wakiulinda mwenge pamoja na kiti hicho.