Tuesday, February 12, 2013

STEPHENI KESHI ABADILI UAMUZI - KUENDELEA KUWA KOCHA WA NIGERIA

Shirikisho la soka la Nigeria limesema leo Jumanne kwamba Kocha wa timu ya taifa Stephen Keshi amebadili uamuzi wake wa kujiuzulu na mazungumzo baina yao na kocha huyo yanaendelea baada ya kocha huyo kuiwezesha Nigeria kushinda ubingwa wa Afrika.

Keshi na Super Eagles, ambayo waliifunga Burkina Faso 1-0 Sunday  na kushinda AFCON 2013, wanatarajiwa kuwasili Nigeria leo huku wakiwa wameandalia sherehe na raisi wa nchi huko mjini Abuja.
    Kujiuzulu kwa Keshi, amabye alitangaza uamuzi wake jana kupitia radio moja huko South Africa, kumeleta aibu kwa utawala wa soka wa nchi hiyo, ambayo imekuwa kiandamwa na skendo za rushwa na utawala mbovu kwa miaka kadhaa sasa.

Shirikisho hilo lilitoa taarifa leo asubuhi kuhusu kujiuzulu kwa Keshi, na kusema kwamba kocha huyo amebadilisha uamuzi wake.

Keshi alisema jana kwamba ameamua kujiuzulu kwake kumekuja kutokana na maofisa wa NFA kumtishia kumfukuza kazi kabla ya mechi ya robo fainali dhidi ya Ivory Coast.

WAJUMBE wapya KAMATI KUU CCM

4 
6ec30
1. WASIRA
2.PINDI Chana
3.Tibaijuka
4. Jerry Slaa
5. Kimbisa
6. Nchimbi
7. Lukuvi


Zanzibar:
1. Nahodha
2. Hussein Mwinyi
3. Prof Makame Mbalawa
4. Dr Salim A.Salim
5. Maua daftari
6. lL. Abuu
7. Samia Suluhu

Spika Anne Makinda apokea sms 600 zenye wito wa kumtaka kujiuzulu na matusi

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda.
Inaripotiwa kuwa Spika wa Bunge, Anne Makinda, amepokea jumbe za maneno 400 na za miito ya simu 200 zenye matusi ya nguoni kutoka kwa watu wakimtaka ajiuzulu. Mtoa habari wa HabariLeo ambaye yupo karibu na Spika Makinda amesemea jumbe hizo zimerekodiwa.Kwamba, Spika alianza kupokea jumbe hizo kuanzia juzi, baada ya viongozi wa CHADEMA kutangaza namba za simu za Spika kwenye mkutano wa hadhara na kuendelea jana ili kutumia ‘nguvu ya umma’, kumlazimisha ajiuzulu.  Sababu ya kutumwa jumbe hizo inaripotiwa kuwa ni baada ya hatua ya Spika Makinda kutangaza mabadiliko ya Kamati za Bunge, yaliyoivunja Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na shughuli zake kuwekwa chini ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) ambapo katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Mwenyekiti wa POAC, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe hakuridhishwa nayo na hivyo kumshitaki Spika Makinda kwa Wananchi ili wamng’oe.
Unaweza kutizama/sikiliza wito huo kupitia audio na video ya chapisho/post ya awali (bofya hapa).
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah, alipozungumza na gazeti hili juzi, alisema uamuzi huo haukufanywa na Spika Makinda peke yake, bali ni baada ya kushauriana na Kamati ya Kanuni za Bunge, ambayo iliridhika na sababu za kuchukuliwa uamuzi huo.
Wajumbe wa Kamati iliyoridhia makubaliano hayo mbali na Spika na Naibu Spika, ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA). Wengine ni Mbunge wa Mbulu, Mustapha Akunaay (CHADEMA), Mbunge wa Kibondo, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi), Mbunge wa Mkanyageni, Mohamed Habib Mnyaa (CUF) na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF). Pia Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Abdallah (CCM), Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM), Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ramo Makani (CCM), Mbunge wa Viti Maalumu, Pindi Chana (CCM) na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM).
Dk Kashilillah alisema mabadiliko hayo hayakuigusa kamati ya POAC peke yake, bali kamati zingine kama ya Sheria Ndogo na ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje, ambayo imegawanywa mara mbili.
Akielezea sababu za kuvunja POAC, Dk Kashilillah alisema lengo lilikuwa ni kuunganisha wizara, taasisi zake na mashirika yaliyo chini ya wizara husika, ili yawe na msemaji mmoja. 
Alisema awali Waziri alikuwa anawajibika PAC, wakati mashirika ya umma yaliyo chini ya wizara yakiwajibika chini ya POAC.
Kwa mujibu wa Dk Kashilillah, kulikuwa na mkanganyiko mkubwa na akaeleza kuwa hatua ya kuunganisha wizara na mashirika yake ya umma, kutafanya sasa Waziri, Katibu Mkuu, Mwenyekiti wa Bodi na watendaji wakuu wa mashirika, kuwajibika kwa kamati moja ya PAC.
Dk Kashilillah alisema sababu nyingine ni kuangalia utendaji katika baadhi ya nchi, ambazo alisisitiza kuwa hazina kamati za mashirika ya umma.
Mwandishi aliwasiliana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ambayo iliweka wazi kuwa hakuna sheria yoyote inayozuia mtu kutoa namba ya simu ya mwingine kwa mtu au watu wengine, bila ridhaa ya mwenye namba ya simu.
Ofisa wa TCRA, ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu si msemaji wa taasisi hiyo, alisema sheria ya kuzuia utoaji namba na taarifa za mtu mwingine, inakataza kampuni za simu kufanya hivyo, lakini haizungumzi kwa mtu binafsi. Ofisa huyo alinukuu sheria hiyo:
 
Taarifa ni siri ya mtu husika, isipokuwa kama mtu huyo ameitoa kwa ridhaa yake.
 
Alisema pamoja na kuwapo na kipengele hicho, mtu yeyote ambaye ana namba ya simu ya mtu mwingine, hazuiwi kutoa namba hiyo kwa watu wengine.Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya   wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, wamesema ingawa namba za simu za viongozi hao zinaweza zikapatikana kwa kila mtu, kuzigawa katika mkutano huo ambao ulikuwa na mtazamo hasi kwa Spika na Naibu wake,  kulikuwa na nia mbaya.
 
Kama ungekuwa mkutano au semina yenye nia njema na Spika, ungesema wamegawa simu kwa nia njema. Lakini mkutano huo ulivyokuwa na kauli mbovu kwa Spika na taasisi ya Bunge, kitendo cha kuwapa watu namba kinamaanisha walitaka hao watu wamtukane pia.
katika mkutano kama huo, kunakuwa na watu wa kila aina wakiwamo wasio na busara. Hivyo viongozi hao wa CHADEMA waliofanya hivyo, wameshindwa kutumia busara.
Mjumbe wa NEC, Juma Killimbah, ambaye aliwahi kuwa Mbunge na kuhadharisha wananchi wasije kujikuta katika mkono wa sheria kwa kutumia namba hizo vibaya kwa kutoa matusi, alisema simu ya kiongozi huyo kujulikana si ajabu na ni jambo la kawaida.
 
Tatizo ni maudhui. Kama kitendo hicho kina lengo zuri hakuna tatizo.
 
Sehemu ya taarifa hii imenukuliwa kutoka kwenye gazeti la HabariLeo. via Wavuti.

Waziri Magufuli azindua Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Ujenzi


 Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akizindua kitabu cha Mwongozo wa Usanifu wa Barabara. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Saidi Amani na kushoto ni Eng. Joseph Nyamuhanga, Mkurugenzi wa Barabara katika Wizara ya Ujenzi.
Msajili wa Bodi ya Wabunifu na Wakadiriaji Majenzi, Arch. Jehad akipokea kitabu cha Mwongozo wa Usanifu wa Barabara kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) mara baada ya kuzinduliwa rasmi. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Saidi Amani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert E. Mrango akipokea kitabu cha Mwongozo wa Usanifu wa Barabara kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, mara baada ya kuzinduliwa rasmi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro,  Eliya Ntandu akipokea kitabu cha Mwongozo wa Usanifu wa Barabara kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) mara baada ya kuzinduliwa rasmi. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Saidi Amani.
Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (wanne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Morogoro.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (Mb), leo amezindua Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi ambalo linakutana kwa siku mbili mjini Morogoro. Wakati akiongea katika uzinduzi wa Baraza hilo linalojumuisha wajumbe kutoka katika taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi,  Mheshimiwa Magufuli amewapongeza watendaji wakuu wa wizara na taasisi zake kwa namna wanavyosimamia utekelezaji wa majukumu yao kwa ufanisi. “Mafanikio yanayoonekana kupatikana kwa upande wa wizara yetu ni matokeo ya usimamizi wenu mzuri” alielezea Waziri Magufuli na kuwataka kutorudi nyuma kwani hiyo ni dhamana waliyopewa na Taifa.
Akizungumzia changamoto zilizopo, Waziri Magufuli alisisitiza kukerwa kwa kuendelea kujitokeza vitendo vya rushwa katika vituo vya mizani na kwenye vivuko.  Mhe. Magufuli amezipongeza hatua zilizokwisha kuchukuliwa na Mtendaji Mkuu wa Tanroads kwa kutangaza ajira za wafanyakazi wa vituo vya mizani na amemtaka kukamilisha mapema ajira za Wahandisi watakaosimamia vituo hivyo. “Hatua hizi tuzimechukua baada ya kubaini kuwa karibu asilimia themanini ya watendaji waliopo katika vituo vya mizani ni wala rushwa” alibainisha Mheshimiwa Waziri Magufuli.
Kwa upande mwingine Wakala wa Ufundi na Umeme  (TEMESA) nao umepewa siku sitini ili kuanza zoezi la ukatishaji tiketi za elektoniki hasa katika kivuko cha Kuvukoni jijini Dar es Salaam. Waziri Magufuli alibainisha baadhi ya mbinu zinazotumiwa na watendaji wasio waaminifu katika vivuko hivyo, kuwa ni pamoja na kujichapishia tiketi kwa siri na wakati mwingine kutochana tiketi wanazozipokea kutoka kwa abiria kwa lengo la kuziuza tena.
Waziri Magufuli hata hivyo amepongeza zoezi la kukamata magari ya Serikali yanayotumia namba za binafsi kinyume na sheria. “Tayari hadi sasa jumla ya magari 1,830 tayari yamekamatwa na kusajiliwa kwa namba za Serikali” alifafanua Mheshimiwa Magufuli..
Wakati huo huo Waziri wa Magufuli pia amekizundua Kitabu cha Mwongozo wa Usanifu wa Barabara. Kitabu hicho kitatumiwa katika utekelezaji wa shughuli za ujenzi na matengenezo ya barabara hapa nchini.
Wakati akizindua kitabu hicho Mheshimiwa Waziri amewapongeza Mameneja wa Tanroads wa mikoa ya Dodoma na Morogoro kwa ubunifu ambao wameuonyesha kwa kutumia fedha wanazotengewa katika bajeti zao. Alielezea kufurahishwa na kazi za upanuzi wa barabara unaoendelea kuanzia eneo la Ihumwa hadi Dodoma Mjini ambao ni matokeo ya jitihada za watendaji wenyewe mkoani. Hapa Morogoro pia kazi hizi za upanizi wa barabara zimeelezwa kuanza kutekelezwa wakati ambapo mkoani Tabora tayari kuna zaidi ya kilometa sita za lami zimejengwa kwa kutumia fedha zilizotengwa katika bajeti ya mkoa. “Ninawaelekeza Mameneja wa Tanroads katika mikoa mingine nanyi muwe na ubunifu na sio kukaa bila ya kuchukua hatua zozote hata pale ambapo tayari kuna bajeti iliyopitishwa” alimalizia Mheshimiwa Magufuli.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...