Friday, May 23, 2014

BIBI ANASWA AMEBEBA 'UNGA' UWANJA WA NDEGE DAR...!!!


“Huyu ni mzee, lakini tumeshangaa kuona bado ana nguvu za kutosha na tulishangaa baada ya kutoa kete 20 kwa mara moja katika awamu ya kwanza, jambo hili si rahisi kutokana na umri wake,” .PICHA|MAKTABA 



Dar es Salaam. Bibi mmoja raia wa Nigeria, Olabisi Ibidun Cole (65) amevunja rekodi ya umri wa watu wanaokamatwa wakiwa na dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Cole alikamatwa Jumatatu akiwa amemeza kete 82 aina ya heroini zilizokuwa zimefungwa kwenye karatasi zinazofanana na ganda la sigara, ambazo si rahisi kuonekana katika mitambo.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Alfred Nzowa zimesema pamoja na mbinu zake na kujiamini, mwanamke huyo alikamatwa kutokana na ushirikiano wa vitengo mbalimbali vya uwanja wa ndege.

Kamanda wa Polisi wa Uwanja wa Ndege, Hamisi Selemani alisema mwanamke huyo alikamatwa Mei 19, mwaka huu saa tisa alasiri akijiandaa kwenda Paris, Ufaransa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.

Selemani alisema raia huyo aliwasili nchini Mei 15, mwaka huu na alikaa muda wote bila ya kuwa na shughuli yoyote, jambo ambalo lilitiliwa shaka na kumkamata. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

KAKA WA MTOTO ALIYEFUNGIWA KWENYE BOKSI NAYE 'APOTEA'

 Rashid Mvungi  akimuangalia mtoto wake Nasrah Rashid (4) ambaye ni mlemavu wa viungo aliyefungiwa chumbani na kufichwa kwenye boksi bila ya kufanyiwa usafi tangu akiwa na umri wa miezi tisa.  

Morogoro. Zimeibuka taarifa kwamba mtoto aliyekuwa amefungiwa kwenye boksi kwa miaka minne na mama yake mkubwa, Nasra Rashid (4) alikuwa na kaka aliyefahamika kwa jina la Nasoro ambaye hadi sasa hajulikani mahali halipo.

Wakati polisi ikisema imefurahi kupata taarifa hizo na kwamba itazifanyia kazi, habari zilizopatikana jana kuhusu hali ya Nasra zimesema atafanyiwa vipimo 18 ili kubaini hali ya afya yake. Vipimo vya awali, vimebaini kuwa amevunjika mifupa ya mikono na miguu na kwamba atapelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Kuhusu kaka yake, baadhi ya majirani wa nyumba aliyokuwa anaishi mama mzazi wa Nasra enzi za uhai wake walidai kuwa Mariamu alikabidhiwa watoto wawili kuwalea baada ya mama yao kufariki dunia.

Mmoja wa majirani hao, Ramadhani Mansuri alisema wakati mama mzazi wa Nasra akiishi eneo la Mjimpya alikuwa na watoto wawili akiwamo Nasoro ambaye aliachwa akiwa na umri kati ya miaka 14-15.

Vipimo

Ofisa Ustawi wa Jamii, Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungamtitu alisema taarifa alizopata kutoka kwa madaktari zinasema kuwa mtoto huyo atafanyiwa vipimo 18 ili kubaini hali ya afya yake.

Akizungumzia matokeo ya vipimo vya awali, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Dk Rita Lyamuya alisema haijafahamika sababu za kuvunjika kwa mifupa hiyo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 23, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.

.

.
.
.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

DAVID MOYES AZUA BALAA, AMPIGA DOGO MMOJA BAADA YA KUMTUKANA KWA KUPOTEZA KAZI MAN UNITED

Investigation: Moyes was present at the bar in Clitheroe at the time of the assault
Incident: Joshua Gillibrand claims he was attacked at just after 10pm on Wednesday night
 Tukio: Joshua Gillibrand anadai alishambuliwa majira ya saa 10:00 usiku wa jana jumatano.
 
Inasemekana Moyes alikerwa na kijana huyo mlevi aliyemtukana kocha huyo baada ya kufukuzwa kazi hivi karibuni na kumuita ‘s*** (hatujaona haja ya kutafsiri kimaadili), akimaanisha hajawahi kushinda kombe, alisema shahidi.
Baada ya maneno hayo vurugu ziliibuka mezani ambapo glasi zote zimeanguka chini.
Mr Gillibrand, alikula vibao na alichubuka kwenye bega kutokana na ugomvi huo, lakini hakuhitaji kwenda hospitali kupata matibabu zaidi.
Leo polisi walithibitisha kufungua uchunguzi juu ya tukio hilo na wanatarajia kuongea na kocha huyo wa zamani wa Everton.
Location: The Emporium wine bar in Clitheroe, Lancashire, where the alleged assault took place

BOKO HARAM NI MAGAIDI WA KIMATAIFA - UN


Baraza la Usalama la UN
Baraza la usalama la umoja wa mataifa hatimaye limeidhinisha kuwekewa vikwazo kundi la Boko Haram baada ya utekaji nyara wa takriban wasichana 300 wa shule katika eneo la Chibok Nigeria.
Kundi hilo limeshutumiwa kuwaua maelfu ya watu nchini Nigeria katika miaka michache iliyopita.
Nigeria ni mwanachama wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa kwa kipindi cha miaka miwili. Kwa nafasi hii imeweza kushinikiza baraza hilo kuimulikia tochi.
Hatua ya baraza hilo kuiorodhesha Boko Haram miongoni mwa magaidi wa kimataifa, wakipishana au hata kuhusishwa moja kwa moja na AL Qaeda, huenda isionekane kama hatua kubwa. Lakini hii ina maana kuwa sasa jamii ya kimataifa italichukulia kwa uzito mkubwa zaidi kundi hilo.
Baraza hilo limeidhinisha pia vikwazo kuwekewa kundi hilo, viongozi wake na yeyote anayehusishwa nalo. Hii ina maana kuwa hata mali zao zitazuiliwa na akaunti zao zote zinazojulikana kufungwa. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...