Aliyekuwa
Waziri Mkuu Edward Lowassa
SIKU moja baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kumuonya aliyekuwa
Waziri Mkuu Edward Lowassa, kwa tuhuma za kukiuka Katiba na kuanza
kampeni za Urais kabla ya muda, kiongozi huyo ameibuka na kudai kuwa
hana njia ya kuwazuia watu wasimuombe agombee Urais.
Pia Lowassa ametumia nafasi hiyo na kuwaomba wale wote ambao bado
wana nia ya kumshawishi agombee nafasi hiyo ya urais, wasubiri kwanza
hadi pale chama chake hicho kitakapotoa maelekezo.
Akizungumza na vijana 60 wa bodaboda kutoka wilaya ya Mbarali, Mbeya
waliokwenda pia kumshawishi agombee nafasi hiyo, mjini Dodoma jana,
alisema si vyema kwa maofisa wa chama kuzungumzia masuala ya wanachama
wao kwenye vyombo vya habari wakati kuna vikao vya chama.
Alisema watu waliojitokeza na kumshawishi kuchukua fomu za kuwania
nafasi hiyo ya Urais, hajawaita wala kuwalipa chochote kama inavyodaiwa
na kwamba walikuwa wakifuata maneno ya Rais Jakaya Kikwete aliyoyatoa
mkoani Ruvuma katika sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya Uhuru.
Alisema katika siku hiyo, Rais Kikwete aliwataka watanzania
wawashawishi viongozi wanaoona wanafaa ili wajitokeze kugombea nafasi
hiyo ya Urais. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.