Sababu za Watoto Wachanga Kulia Mara kwa Mara na Namna ya Kuwabembeleza
Kwa nini watoto wachanga wanalia .?
Ni
kawaida kwa watoto kulia. Hata watoto wanaozaliwa na afya njema kabisa
wanaweza kulia kwa jumla ya wastani wa kati ya saa moja mpaka matatu kwa
siku. Kwa vile watoto hawawezi kujifanyia chochote wao wenyewe zaidi ya
kutegemea wazazi, walezi ama watu wengine wanaowazunguka katika
kuwapatia chakula, joto, na faraja, kilio ni njia ya mtoto ya
kuwasilisha moja ya mahitaji hayo.
Kama
mzazi mpya, wakati mwingine inakuwa vigumu kutambua mtoto wako
anahitaji nini anapolia. Mzazi anaweza kuwa na maswali kadhaa kichwani
mwake, je, mtoto ana njaa, anasikia baridi, ana kiu, anaumwa ama
amechoka ? Katika siku za mwanzo, hali ya namna hii inawawia vigumu
wazazi wengi, wasijue nini la kufanya.
Hata hivyo, kwa kadiri siku
zinavyopita mzazi mpya ataweza kutambua kuwa kilio cha mtoto wake
kinamaanisha anahitaji nini kutokana na mfumo wake wa kulia.