MWENYEKITI
wa Kamati ya Mashindano ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga Jumamosi
iliyopita alimtimua mshiriki wa shindano la Redd’s Miss Morogoro 2013, Saphina Chumba (20) jukwaani wakati shindano hilo lilipokuwa likiendelea.
Tukio
hilo lilitokea Jumamosi iliyopita katika Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii
ya Nashera mjini hapa wakati mrembo huyo alipokuwa akiwania kuvaa taji
la mkoa huo.
Kisa cha mrembo huyo aliyevalia namba 5 kutimuliwa ni kukiuka maadili na kanuni za mashindano hayo kwa
kuvaa nusu utupu mbele ya mgeni rasmi ambaye alikuwa Mbunge wa Kilosa,
Mustapha Mkulo na mbele ya Kamati nzima ya Miss Tanzania.
Baada
ya kuona jinsi alivyovaa, Lundenga na kamati yake walikubaliana
kumtimua mshiriki huyo kwa kumwita Jaji Mkuu wa shindano, Alex Niktasi
na kumtaka amuondoe haraka.
Mbali
na Chumba, pia jaji alimtimu mrembo mwingine aliyevalia namba 8, Neema
Joel (20) kutokana na kushiriki shindano hilo mara mbili mwaka huu,
inadaiwa mara ya kwanza alishiriki mkoani Arusha.
Lundenga
alipohojiwa na waandishi wa habari alisema kamati yake inataka kuendeleza
nidhamu tangu ngazi ya chini, hivyo hawawezi kuruhusu utovu wa nidhamu.