Saturday, November 22, 2014

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOVEMBA 22, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

CHAMA TAWALA ZAMBIA WAMTIMUA KAIMU RAIS CHAMANI

Scott alichukua usukani baada ya aliyekuwa Rais Michael Sata kufariki 
 
Chama tawala nchini Zambia (PF) kimemtimua kaimu rais wa nchi hiyo Guys Scott kutoka chamani na kuvunja utaratibu wa katiba.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa msemaji wa chama hicho.
''Amekuwa akiwaajiri na kuwafuta watu kazi ovyo na pia bila ya kushauriana na kamati kuu ya chama,'' amesema Malozo Sichone.
Bwana Scott, ambaye licha ya hatua hiyo ataendelea kuwa mwanachama wa chama hicho, ataendelea kuhudumu kama kaimu rais hadi uchaguzi utakapofanyika tarehe 20 Januari.
Scott aliteuliwa kuwa kaimu rais kufuatia kifo cha hayati Rais Michael Sata aliyefariki mwezi jana. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MTOTO ALIYEKUFA KWA AJALI AZIKWA UGANDA

wanawake wakiandamana huku wakiomboleza nchini Uganda 
 
Shughuli za mazishi ya mtoto wa miaka miwili zimefanyika nchini Uganda, mtoto ambaye kifo chake kimezua ghadhabu baada ya mtoto huyo kugongwa na gari la halmashauri ya jiji la Kampala ,baada ya mama yake kukamatwa akiuza matunda kinyume cha sheria.
Familia ya Ryan Ssemaganda na wanasiasa wa upinzani walitishia kutomzika mtoto huyo mpaka maofisa hao watakapo wajibika kwa kitendo hicho.Mwili wake ulichukuliwa wakati wakiandamana kuelekea bungeni siku ya alhamisi.
Raia wa Uganda wanaona kuwa halmashauri hiyo inatumia nguvu nyingi kupambana na wachuuzi wa mitaani.
Mama wa mtoto Ryan alikamatwa siku ya jumatatu baada ya kukutwa akiuza matunda huku akiwa hana leseni.
Siku iliyofuata, Bibi wa mtoto huyo alimpeleka katika Ofisi za Mamlaka ya mji wa Kampala ambako mama mtoto alikuwa akishiliwa , nia ilikua kumpa mama mtoto ili amnyonyeshe.
Maafisa wa Ofisi hiyo walikataa na wakati wakijadiliana kuhusu hilo, mtoto alichoropoka kutoka kwa mama yake na kugongwa na gari linalomilikiwa na Mamlaka hiyo.
Siku ya Alhamisi polisi ilizuia kupelekwa kwa mwili katika Bunge, wakisisitiza mwili huo uzikwe ili marehemu apumzike kwa amani, na kuwataka waepuka jambo hilo kushughulikiwa kisiasa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MECHI ZA LIGI KUU UINGEREZA LEO JUMAMOSI

Chelsea
Mechi za Ligi kuu ya Uingereza siku ya jumamosi

Chelsea v West Brom18:00
Everton v West Ham18:00
Leicester v Sunderland18:00
Wakufunzi wa timu kuu nchini Uingereza
Man City v Swansea18:00
Newcastle v QPR18:00
Stoke v Burnley18:00
Mchezaji wa Manchester United
Arsenaly v Man Utd 20:30
Mechi zote kuchezwa saa za Afrika Mashariki. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WENGER: TULIJARIBU KUMSAJILI MESSI


Arsene Wenger asema alijaribu kumsajili nyota wa Barcelona Lionel Messi 
 
Mkufunzi wa kilabu ya Arsenal Arsene Wenger amethibitisha kuwa kilabu hiyo ilijaribu kumsajili nyota wa kilabu ya barcelona Lionel Messi kama mpango wa kutaka kuwanyakua wachezaji watatu wachanga wa kilabu hiyo.
Messi alikuwa na miaka 15 wakati huo na mwenzake Gerrad Pique pamoja na aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal Cess fabregas.
Wenger:''Tulitaka kumchukua Fabregas,Messi na Pique,lakini tukafanikiwa kumpata Fabregas pekee''.
Fabregas aliichezea kilabu ya Arsenal kwa miaka minane kabla ya kurudi Barcelona ,huku Pique akijiunga na Manchester United mwaka 2004.
Wachezaji Cess fabregas na Lionel Mesi wakiwa katika kilabu ya Barcelona.
Messi mwenye umri wa miaka 27,ameichezea timu ya Barcelona kwa muda wote na kuisadia kushinda mataji sita ya La liga pamoja na kombe la vilabu bingwa mara tatu baada ya mpango wa kujiunga na Arsenal kugonga mwamba.
Hatahivyo ,Wenger amepinga madai kwamba mpango huo ulifeli kutokana na makaazi ya Messi na familia yake.
Mchezaji huyo wa timu ya Argentina pia angelazimika kuwa na kibali cha kufanya kazi nchini Uingereza.
Wenger aliongezea:''Nadhani Messi mwenyewe hakutaka kujiunga nasi''. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...