Wednesday, October 01, 2014

BUNGE LA KATIBA: WALIOPIGA KURA YA HAPANA WATISHIWA MAISHA


Wahudumu  wa Bunge Maalumu la Katiba wakiwa wamebeba masanduku ya kura za wajumbe waliopiga kura za siri kwa Sura ya 11 hadi 19 ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, mjini Dodoma jana.

Baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba waliopiga kura za hapana wamelazimika kuondoka Dodoma na kurudi Zanzibar kwa madai ya vitisho walivyopata kutoka kwa wenzao.

Mmoja wa wajumbe hao, Salma Said alisema jana jioni kuwa yeye na wajumbe wenzake wamekataa kuitikia wito wa Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta kwenye Kamati ya Mashauriano ili kuhojiwa kuhusu kura hiyo na kutokana na vitisho wanavyopata kutoka kwa wajumbe wenzao wameamua kuondoka Dodoma.

Vitisho hivyo vimeripotiwa muda mfupi baada ya Sitta kuunda Kamati ya Mashauriano ya watu tisa inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti, Samia Suluhu Hassan kushughulikia kura hizo zilizopigwa na wajumbe saba zinazoweka njiapanda uwezekano wa kupatikana akidi ya kupitisha Katiba inayopendekezwa.

Wajumbe waliopiga kura za wazi za hapana kwa ibara zote ni Adil Mohamed Adil, Dk Alley Soud Nassor, Fatma Mohamed Hassan, Jamila Ameir Saleh, Salma Hamoud Said, Mwanaidi Othman Twahir na Ali Omary Juma. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WALIODHURIKA KWA TOGWA SONGEA WAFIKIA 340...!!!


 

Idadi ya watu waliolazwa hospitalini kwa kunywa togwa inayosadikiwa kuwa na sumu katika Kijiji cha Litapwasi, Kata ya Mpitimbi mkoani Ruvuma imeongezeka kutoka 270 hadi 340.

Tukio hilo lilitokea Jumapili baada ya watu kushiriki sherehe ya Kipaimara ambako walikula, kunywa pombe na togwa na baadaye wale waliokunywa togwa walianza kuumwa matumbo, kuhara na kutapika.

Hadi jana, watu 102 walikuwa bado wamelazwa katika Zahanati ya Lyangweni, Hospitali ya St. Joseph Peramiho na Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma.

Tayari watu watano wanashikiliwa na Polisi kwa upelelezi kuhusiana na tukio hilo, akiwamo Baba Mzazi wa mtoto Dickson aliyepata kipaimara, Enes Nungu (47). Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATANO OKTOBA 01, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MKE WA MUGABE KUSHITAKIWA...!!!

Grace Mugabe kulia
Muungano wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Zimbabwe al maarufu Zinasu, umesema kwamba unawasilisha kesi mahakamani hii leo kutafuta ufafanuzi zaidi wa namna mkewe rais Grace Mugabe alivyopata shahada ya udaktari wa falsafa.
Mwanafunzi mmoja mwanaharakati amesema kuwa ni muhimu kwa taifa hilo kuhifadhi hadhi yake ya elimu.
Baadhi ya watu wamehoji kasi aliyosomea shahada hiyo huku wengine wakidai ni njama za kumuandaa kwa urithi wa kiti cha rais baada ya rais Mugabe.
Gazeti moja linalomilikiwa na serikali , the Herald limechapisha kuwa Bi Grace Mugabe alipata shahada hiyo kwa utafiti wake juu ya mabadiliko ya mfumo wa kijamii na miundo ya familia. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

DRC: WAPIGANAJI WA ZAMANI WAFA NJAA

Wapiganaji hao wa zamani wamekuwa wakila chakula kutoka kwa mashamba ya wakulima
Shirika moja la kimataifa la kutetea haki za binadamu linasema kuwa zaidi ya watu mia moja wamefariki kutokana na njaa pamoja na maradhi katika kambi moja ya kijeshi katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Shirika hilo Human Rights Watch, limesema kuwa watu hao ambao walikuwa wapiganaji wa zamani na wake zao pamoja na watoto walihamishwa katika kambi nyingine iliyotengwa Kaskazini mwa DRC.
Ilikuwa baada ya wao kujisalimisha kutoka kwa kundi la wapiganaji Mashariki ya nchi.
Walipokea chakula kidogo na huduma ya afya baadhi wakiponea kifo kwa kuiba chakula kutoka kwa mashamba ya wakulima.
Serikali ya DRC inasema kuwa inachunguza ripoti hiyo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

UCL: MATOKEO YA CHELSEA VS SPORTING LISBON

IMG_7653.PNG
Usiku wa jana watu wawili waliowahi kuwa vipenzi vya nchi ya Ureno – Jose Mourinho na Nemanja Matic walirejea nchini humo katika jiji la Lisbon lakini safari hii wakiwa kama wapinzani.
Huku Mourinho akionekana kuchukua ‘attention’ yote ya vyombo vya habari ndani ya jiji Lisbon, Nemanja Matic alikuwa kasahaulika.
Lakini katika dakika ya 34, mchezaji huyo wa zamani wa Benfica aliifungia goli pekee Chelsea katika mchezo huo.
Matic alifunga goli hilo kwa kichwa baada ya kuachwa bila kukabwa vizuri na mabeki wa Sporting Lisbon.
Mchezaji wa zamani wa Manchester United Luis Nani alikuwa akiitumikia Sporting jana na hakuwa kwenye kiwango kizuri katika kipindi cha kwanza – kipindi cha pili alijitahidi lakini akashindwa kubadili matokeo ya mwisho dhidi ya vijana wa Jose Mourinho.
Takwimu na timu zilizopangwa
Sporting (4-3-3): Patricio 7; Cedric 6, Mauricio 5.5 (Oliveira 63, 6), Sarr 5, J.Silva 5; Mario 6, Carvalho 6, A.Silva 6 (Montero 81); Carrillo 6.5 (Capel 81), Slimani 6, Nani 6.
Subs not used: Marcelo, Jefferson, Martins, Rosell.
Bookings: Carvalho, Mario, Cedric, Mauricio
Manager: Marco Silva
Chelsea (4-2-3-1): Courtois 6; Ivanovic 6, Cahill 6, Terry 6, Luis 6.5; Matic 8, Fabregas 7; Schurrle 5 (Willian 57, 6), Oscar 7.5 (Mikel 71, 6), Hazard 7 (Salah 84); Costa 6.
Subs not used: Cech, Zouma, Azpilicueta, Remy.
Bookings: Ivanovic, Hazard, Luis Filipe, Fabregas
Manager: Jose Mourinho.

UCL: MATOKEO YA MAN CITY VS AS ROMA

IMG_7652.PNG
Mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya Manchester City imeendelea kutopata matokeo chanya katika michuano ya ligi ya mabingwa wa ulaya kwa mara ya pili mfululizo msimu huu.
Wakicheza kwenye uwanja wao wa Etihad dhidi ya AS Roma ya Serie A, Sergio Aguero aliipatia timu yake goli katika dakika ya 4 kupitia mkwaju wa penati.
Lakini dakika 19 baadae Francisco Totti ‘Mfalme wa Roma’ akaifungia goli la kusawazisha Roma na kuandika historia ya mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kufunga goli kwenye michuano ya ulaya.
Man City sasa inakuwa imeshindwa kupata matokeo chanya katika mechi 2 za kwanza cha UCL – wiki mbili zilizopita walifungwa na Bayern Munich.
Timu zilipangwa hivi
Manchester City: Hart 7; Zabaleta 6.5, Kompany 6, Demichelis 5.5, Clichy 6; Navas 5 (Milner 46, 6), Toure 5.5, Fernandinho 6, Silva 7; Aguero 6.5 (Jovetic 84), Dzeko 6 (Lampard 57)
Subs (not used): Caballero, Sagna, Kolarov, Mangala
Goals: Aguero (Pen, 4)
Booked: Zabaleta
Roma: Skorupski 6; Maicon 6 (Torosidis, 89), Manolas 6, Yanga-Mbiwa 6.5, Cole 6; Pjanic 7.5, Nainggolan 6.5, Keita 6.5; Florenzi 5.5 (Holebas 83), Totti 7 (Iturbe 72, 6), Gervinho 7.
Subs (not used): Curci, Ljajic, Destro, Paredes
Goals: Totti (23)
Booked: Maicon, Nainggolan
Referee: Bjorn Kuipers (Holland) 7
Star man: Miralem Pjanic
Attendance: 37,509

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...