Friday, December 20, 2013

WANAUME HUPENDA KUOA MWANAMKE WA AINA HII

 https://www.facebook.com/jambotz

Leo nitazungumazia juu ya aina ya wanawake ambao wanaume wengi hupendelea kuoa. Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha.
Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.
Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa. Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtakiwa kwamba anataka kumuoa.

Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke na ikiwezekana waweze kupata watotoa ambapo watoto mara ndio wamekuwa furaha ya ndoa. Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga.

BREAKING NEWZZZZZZZZZZZZ...!!! RAIS KIKWETE KUTENGUA UTEUZI WA MAZIRI WANNE...!!!

https://www.facebook.com/jambotz
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda amesema kwamba Rais Kikwete amekubali kutengua nyadhifa za mawaziri wanne kufuatia ripoti ya 'Operesheni Tokomeza' iliyotolewa mapema leo bungeni.
Mawaziri hao waliotenguliwa nyadhifa zao ni: Mhe. David Mathayo David wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki wa Maliasili na Utalii, Mhe. Emmanuel Nchimbi wa Mambo ya Ndani na Mhe. Shamsi Vuai Nahodha wa Ulinzi.

Mhe. Kagasheki alitangaza kujiuzulu mapema kabla uamuzi huo uliotangazwa na Waziri Mkuu.
Endelea kutembelea blog hii ya Jambo Tz kwa habari zaidi. Pia usisahau ku-like page yetu ya facebook click neno Jambo Tz

RAIS KIKWETE ASAINI MUSWADA KUPINGA NA KUONDOA KODI YA SIMU...!!!



Rais Jakaya Kikwete ametia saini hati ya dharura (Certificate of Urgency) ili Muswada wa Fedha wa Mwaka 2013 ufanyiwe marekebisho ya kuondoa tozo ya kodi kwa kadi za simu.
             

Bunge la Bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2012/13 lilipitisha kodi ya Sh1,000 kwa kila kadi ya simu, hatua ambayo ilipingwa na wabunge wengi.


Ingawa wasemaji wa Ikulu hawakupatikana jana kuzungumzia suala hilo, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba alisema jana kuwa Rais Kikwete alitia saini hati hiyo juma hili.


Ingawa wasemaji wa Ikulu hawakupatikana jana kuzungumzia suala hilo, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba alisema jana kuwa Rais Kikwete ametia saini hati hiyo juma hili.


“Maana yake ni kuwa, muswada huo unatakiwa urudi bungeni haraka ili uweze kufanyiwa marekebisho hayo,” alisema Makamba. Alisema kabla ya kufikiwa kwa hatua hiyo, Rais alishawaagiza wadau wanaohusika na sekta hiyo wakae na kujadili suala la kodi hizo... “Mazungumzo hayo bado yalikuwa yanaendelea mpaka katikati ya juma hili.”

DIAMOND PLATNUMZ AFANYA PATI YA UFUSKA..!!! NAY, CHEGE, OMMY DIMPOZ WAHUDHURIA

 
Diamond Platnumz akimmwagia manoti Halima Kimwana.

KUFURU ya kufunga mwaka! Dogo anayejua kuzitumia vyema fursa muhimu, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ amefanya yake kwa mara nyingine, safari hii amefanya pati iliyojaa ufuska. 

 
Burudani zikitolewa na Kundi la Kibao Kata.
Msanii huyo kwa ‘kolabo’ ya swahiba wake mkuu ndani ya anga la muziki Bongo, Omari Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ alifanya tukio hilo lililoacha watu midomo wazi mwanzoni mwa wiki hii ndani ya Ukumbi wa Business Park uliopo Kijitonyama, Dar.
Pati hiyo ilikuwa ya kumpongeza mtu wake wa karibu katika Wasafi Classic Baby (WCB), Halima Haroun ‘Halima Kimwana’.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA DESEMBA 20, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...