Hofu
kubwa imetanda Kaskazini mwa nchi ya Kenya,baada ya kuwepo kwa taarifa
kwamba kundi la wapiganaji wa Al shabaab Limeviteka vijiji kadhaa katika
mpaka wa Kenya na somalia.
Mamia ya wakaazi wameyatoroka makaazi yao kufuatia taarifa za kuwepo kwa wapiganaji wa Alshabaab wapatao thelathini.
Shule nne zinaripotiwa kufungwa.
Naibu
kamishna wa kaunti ya Mandera amenukuliwa akisema kwamba wamepokea
ripoti za kuwepo kwa wapiganaji hao na watawaandama na kulidhibiti eneo
hilo. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.