Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Suzan Kaganda. PICHA|MAKTABA
WATU wanane wamekufa papo hapo, huku wengine 50 wakijeruhiwa vibaya
katika ajali mbili tofauti zilizotokea Tabora na Morogoro jana.
Katika ajali ya Tabora, basi la Kampuni ya Mohammed Trans likitoka
Mwanza kwenda Dar es Salaam lilipinduka mara nne katika kijiji cha
Makomero, kata na wilaya ya Igunga na kuua watu 5 na kujeruhi 50.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Suzan Kaganda alikiri kutokea kwa
ajili hiyo na kusema jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi wa kujua
chanzo cha ajili hiyo iliyotokea majira ya saa 5:30 asubuhi.
Alilitaja basi hilo kuwa ni aina ya Scania lenye namba za usajili T
738 AAP ambalo lilikuwa na zaidi ya abiria 55. Akizungumza katika eneo
la tukio, mmoja wa majeruhi, Maimuna Mussa (27) aliyekuwa akielekea
Dodoma na mtoto wake mwenye umri wa miaka miwili, alisema walikuwa
kwenye mwendo kasi na alishitukia gari likiacha njia na kupinduka mara
nne.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.