Afisa elimu mkoa wa Shinyanga Bi. Eva M. Lopa
Na Steven Kanyeph
Afisa elimu mkoa wa Shinyanga Bi. Eva M. Lopa ametoa takwimu ya ufaulu
kwa elimu ya msingi na sekondari kwa muda wa miaka mitatu kwa mkoa wa
shinyanga katika kikao cha taarifa ya elimu kwa mkoa wa Shinyanga
kilichofanyika katika ukumbi wa Mkoa uliopo mkoani Shinyanga , siku ya
jana.
Akitoa takwimu hizo kwa elimu ya msingi Bi. Lopa amesema
kuwa matokeo ya elimu ya msingi yamekuwa ya yakipanda mwaka hadi
mwaka , na kwa mwaka 2010 yalikuwa ni asilimia 42.5 wakati mwaka 2009
yalikuwa asilimia 31.9 mwaka 2011 matokeo yalikuwa asilimia 44.2 hivyo
kuwepo na ongezeko la asilimia 1.7% kwa mwaka 2009 hadi 2011 wakati
mwaka 2012 wanafunzi waliofauru ni asilimia 56.1% sawa na ong ezeko la
asilimia 11.9
Afisa elimu huyo ameainisha sababu zilizopelekea
ongezeko la ufaulu huo kwa mwaka 2012 kwa elimu ya msingi kwa mkoa wa
Shinyanga kuwa ni pamoja na ufuatiliaji wa karibu wa viongozi wa elimu
ngazi za wilaya na mkoa , ufuatiliaji wa ufundisha ji, ongezeko la
walimu kutoka uwiano wa 1.74 hadi 1.54 na ongezeko la vitabu kwa
wanafunzi kutoka uwiano wa f1.6 hadi 1.4