Friday, May 31, 2013

DIAMOND AMPIGIA MAGOTI JOKATE NA KUMUOMBA MSAMAHA

MKALI wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, ameibuka na kuelezea kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake zilipendwa, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ambaye ni mwigizaji na modo moto wa kuotea mbali Tanzania.


Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.

Akizungumza kwa uhakika kabisa, Diamond alisema inampasa amuombe radhi Jokate kwa sababu katika uhusiano wao, Jokate hakuwahi kumkosea ila yeye ndiye tatizo na chanzo cha kuachana kwao.
Diamond alisema hayo kwenye mahojiano na Mtangazaji Zamaradi Mketema katika Runinga ya Clouds kwenye Kipindi cha Take One, kilichorushwa juzi Jumanne usiku kituoni hapo.

DIAMOND ANAFAFANUA
“Inanipasa nimuombe radhi Jokate. Ni kweli nilimtenda vibaya wakati wa mapenzi yetu. Hakukosea sana maana hakuwahi kufanya jambo lolote kinyume. Sijui niseme nini lakini nataka kueleza wazi kuwa mimi ndiyo sababu ya kuachana kwetu na ilitokea tu.


Diamond na Jokate wakicheza.

“Naamini hilo jambo lilimuuma sana, maana nakumbuka wakati ule, baada ya mimi kurudi kwa Wema (Sepetu), watu walimwandama sana kwa maneno na alionekana msaliti lakini ukweli ni kwamba nilimpenda sana lakini ndiyo hivyo, siwezi kufafanua zaidi.
“Kutoka moyoni mwangu, namuomba msamaha Jokate, kama hatanisamehe nitaendelea kumuomba mpaka naingia kaburini. Sina raha kabisa kutokana na jambo hilo. Lazima niwe mkweli.”

JACQUELINE WOLPER
Diamond alikwenda mbali zaidi na kuwazungumzia baadhi ya wasichana aliowahi kutoka nao kimapenzi akiwemo mwigizaji Jacqueline  Wolper ambaye alisema ni mwanamke aliyempenda sana, ndiyo maana alimtungia wimbo wa Mawazo.

PENNY SASA
Kwa upande wa mpenzi aliye naye sasa, Mtangazaji wa Runinga ya DTV, Penieli Mungilwa ‘Penny’ alisema ni mwanamke mtulivu na sahihi kwake kwa sababu anatambua majukumu yake kwake, pia anamheshimu.

“Huyu kwa kweli ana karibu sifa zote alizonazo Wema ila uzuri wa Penny ananiheshimu sana. Hafanyi mambo yake hadharani. Unajua wakati nikiwa na Wema hata kama akifanya mambo yake siku mbili au tatu baadaye nayaona kwenye magazeti, tofauti na Penny ambaye kwangu mimi naona ananiheshimu, hata kama anafanya mambo yake ni kwa siri.”

BREAKING NEWZZZZZZZZZZZ...!!! NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA (ACSEE 2013)


Matokeo ya kidato cha 6 yametangazwa. Ufaulu umeongezeka mara dufu zaidi ya wanafunzi 90% wamefaulu. Shule zilizoongoza ni
    1. Marian Girls
    2. Mzumbe

f Matokeo ya kidato cha sita (ACSEE) 2013 - Link 1

f Matokeo ya kidato cha sita (ACSEE) 2013 - Link 2

TANGAZO MUHIMU KWA UMMA KUTOKA BENKI KUU YA TANZANIA

 
 Benki Kuu inapenda kuutahadharisha umma kuwa katika siku za karibuni kumekuwepo
na mtandao wa matapeli unaotumia TOVUTI ifuatayo www.jakayafoundation.wapka.mobi/index.html

Mtandao huo unajidai kuwa ni Taasisi ya Fedha ijulikanayo kwa jina la Jakaya foundation ambayoinamilikiwa na Benki Kuu chini ya utawala wa bodi kuu ya mikopo inayotolewa na serikali kupitia sekretariat ya Utumishi wa umma ofisi ya Rais. 


Matapeli hao wanaeleza kwamba Taasisi hiyo inatoa mikopo ndani ya masaa 24 kwa Mtanzania yeyotemwenye umri kuanzia miaka 18 endapo atajiunga kwa kulip a ada ya shilingi 37,000/=.BENKI KUU INAUARIFU UMMA KUWA HAIITAMBUI NA WALA HAIHUSIANI KWA NAMNA YOYOTE ILE NA TAASISI INAYOELEZWA KWENYE TOVUTI HIYO.


Kwa taarifa hii, Benki Kuu inatoa tahadhari kwa Wananchi kutojihusisha na Taasisi hiyo ya kitapeli kwa ajili ya kupata huduma za mikopo kama ambavyo inadai.
 

IMETOLEWA NA
IDARA YA UHUSIANO NA ITIFAKI
BENKI KUU
YA TANZANIA
DAR ES SALAAM.
29/5/2013

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MAY 31, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS HAYA HAPA

14 b3187

1 1c845

HAWA NDIO WADADA WALIO FUNGA NDOA YA JINSIA MOJA

Mashoga hao wakifungishwa ndoa kwenye ofisi ya msajili nchini Uingereza.
Wanawake wawili raia wa Pakistan wameweka historia kama Waislamu wa kwanza wa jinsia moja kufunga ndoa nchini Uingereza.

Rehana Kausar, miaka 34, na Sobia Kamar, miaka 29,wameweka historia pale walipofunga pingu za maisha katika sherehe iliyofanyika kwenye ofisi ya msajili, kisha haraka wakaomba hifadhi ya kisiasa baada ya kuwa wamefunga ndoa, wakidai kwamba maisha yao yatakuwa hatarini kama wakirejea kwenye nchi yao ya asili.
Wakishuhudiwa na wasimamizi wao na marafiki wawili, wanandoa hao walivalia mavazi meupe asilia ya ndoa pale walipofunga ndoa mjini Leeds, West Yorkshire.
Wawili hao, kutoka mikoa ya Lahore na Mirpur ya Pakistan, walisema walipokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa wapinzani nchini Pakistan - ambako mahusiano ya jinsia moja ni kinyume cha sheria na kuchukuliwa ni kusaliti Uislamu.
Na tangu habari za ndoa yao mapema mwezi huu kuzagaa, wanandoa hao walidai kupokea vitisho vya kuuawa hata kutoka nchini Uingereza 
Kabla ya zoezi hilo, hata msajili aliwashauri wawili hao kufikiria kwa makini kuhusu uamuzi wao wa kufunga ndoa sababu ya mtazamo wa baadhi ya Waislamu kuhusu mahusiano ya jinsia moja.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...