SIKU
MOJA baada ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF)
kuwatembezea wadau na wanachama wake katika nyumba za mradi wa nyumba za
makazi ambazo zimejengwa na Shirika hilo eneo la Buyuni kata ya Majohe
Chanika Wilayani Ilala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Naibu
Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene nae ametembelea na kujionea nyumba
hizo na kuumwagia sifa Mfuko huo kwa ubunifu na kuwajali wananchama
wake.
Mbene
pia alitembelea Ujenzi wa jingo la Kitegauchumi la Ghorofa 35
linalojengwa na Mfuko huo katikati ya jiji la Dar es Salaam. Pichani ni
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akiangalia mchoro wa Jengo
la Kitega Uchumi cha Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF)
ambalo linajengwa katikati ya jiji la Dar es Salaam na litakuwa na
Ghorofa 35. Ndani ya jingo hilo la kutakuwa na Ofisi, maduka na nyumba
za kulala.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF),
Bwana Adam Mayingu akimpa maelezo Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo
Mbene juu ya muundo kamili wa Jengo hilo la ghorofa 35 ambalo linajengwa
na PSPF jijini Dar es Salaam na litakuwa na maduka, makazi na Ofisi.
Meneja Mradi wa Ujenzi
wa Jengo hilo la PSPF Tower, Ghazi Al Shamali (kushoto) akitoa maelezo
kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma
(PSPF), Bwana Adam Mayingu juu ya hatua zilizofikiwa hadi sasa katika
ujenzi huo.
Naibu
Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akiangalia thamani za ndani
katika moja ya vyumba katika nyumba zilizopo ndani ya jengo hilo la PSPF
Tower ambalo ujenzi wake bado unaendelea na pindi zitakapo kamilika
zitauzwa kwa watumishi wa Serikali pamoja na Wanachama wa Mfuko huo.
Naibu
Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko
wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu
wakiongozana kuteremka ngazi zilizopo katika moja ya nyumba (apartment)
zilizopo katika jingo hilo la PSPF Tower ambalo linaendelea kujengwa.
Naibu
Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akitembezwa ndani ya jengo hilo
na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma
(PSPF), Bwana Adam Mayingu.
Watumishi wa PSPF wakizungumza jambo ndani ya Jengo
hilo.
Awali Naibu Waziri wa
Fedha, Janet Zebedayo Mbene alipata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi
wa nyumba 491 za Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF)
zinazojengwa Buyuni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na ambazo
zimekamilika ujenzi wake na kuanza kuuzwa kwa Wanachama wa mfukjo huo.
Pichani mbele kutoka kushoto ni Gabriel Silayo, Mkurugenzi wa Uwekezaji
wa PSPF, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, Naibu Waziri wa
Fedha, Janet Mbene na Mkurugenzi wa Fedha wa PSPF, Masha Mshomba
wakimtembeza Kiongozi huyo katika nyumba hizo.
Nyumba hizo
zikiwa zimekamilika ujenzi wake na kusubiri wateja tu.
Naibu Waziri wa Fedha,
Janet Mbene akiwa na Mkurugenzi wa Fedha wa PSPF, Masha Mshomba
akimtembeza ndani ya moja ya nyumba hizo.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu akifafanua jambo kwa Naibu Waziri
wa Fedha, Janet Mbene nje ya moja ya nyumba ambazo zimejengwa na PSPF,
kwaajili ya kuwauzia wanachama wake kwa gharama nafuu.