Saturday, April 13, 2013

ANGALIA PICHA IKIWAONYESHA ODINGA AKIWA NA KENYATTA IKULU NA WALIOKUA WAGOMBEA WENZA WAO

Picture
Picha: L-R: Uhuru, Ruto, Raila, Kalonzo katika Ikulu ya Nairobi leo, Aprili 13, 2013
RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta na na Naibu wake William Ruto, leo wamekutana na kushauriana na wakuu wa chama cha CORD Raila Odinga na Kalonzo Musyoka waliowatembelea Ikulu Nairobi kuwatakia heri.

PADRI ALIYEOA KWA SIRI AFUNGWA JELA MIEZI 6 ...!!!

KUSHOTO: Padri William akimbusu mkewe, Beverley. KULIA: Kanisa la Mt. Clara ambamo Padri huyo alibambwa akifanya uchavu wake kwa binti wa miaka 17.

Padri mmoja wa kanisa Katoliki ambaye alifunga ndoa kwa siri amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela jana kwa kumsumbua msichana mdogo kwa kile jaji alichoelezea 'uvunjifu mkubwa wa uaminifu'.


William Finnegan, akifahamika kama 'Fadha Bill', alimpapasa binti huyo mwenye miaka 17 chini na kulazimisha kumbusu kwa nguvu katika Kanisa Katoliki la Mt Clara mjini Bradford siku ya Jumapili ya Pasaka mwaka jana.

Jaji Roger Thomas alisema kwamba Padri huyo mwenye miaka 60, alikiri wakati wa kesi hiyo kwamba alifunga ndoa kwa siri miaka 14 iliyopita.

Pia alitumia maneno makali kwa wanaparokia wa Finnegan ambao walikuwa upande wake licha ya mashitaka hayo, akisema: "Pengine baadhi yao wanaweza kuamini kesho jua litachomoza magharibi kesho kama akisema hivyo."

YUSUPH MLELA AMTUNDIKA MIMBA MWANAFUNZI NA KUMLAZIMISHA AITOE....!!

STAA wa filamu za Kibongo, Yusuph Mlela amedaiwa kumtundika mimba mwanafunzi aliyefahamika kwa jina moja la Salha, mkazi wa Zanzibar ambaye anasoma katika chuo cha ITF, Tandika, jijini Dar.

Kwa mujibu wa chanzo kimoja  kilichopo chuoni hapo, Mlela alidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na denti huyo kwa muda mrefu ambapo mashosti wote wa Salha, walikuwa wakimtambua kama shemeji yao hadi alipodaiwa kumpa kibendi.

 “Unajua shemeji yetu (Mlela) alikuwa anakuja sana hapa chuoni lakini baada ya kuambiwa yule Salha ana ujauzito wake, aliruka viunzi na kusema hahitaji mtoto, atoe mimba.


“Salha alipokataa ndipo Mlela alipoamua kukata mguu kabisa, tukawa hatumuoni,’’ kilisema chanzo hicho.


Alipotafutwa Mlela kuhusiana na ishu hiyo, alimkana mwanafunzi huyo na kusema hamtambui na wala chuo  anachosoma hakijui.


“Huyo msichana simjui hata hicho chuo chenyewe cha Tandika sijawahi kufika huko,  kama huyo binti ana ushahidi auweke hadharani,’’ alisema Mlela.

MWENYEKITI WA CHADEMA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA JELA KWA WIZI WA MIL. 1.2


Mwenyekiti wa chadema, mtaa wa Isamilo kaskazini B wilayani Nyamagana Philbert Bulinjiye amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kujipatia shs milioni 1,250,000 kwa njia ya udanganyifu.

Hukumu hiyo, imetolewa na hakimu Vaineth Mahizi wa mahakama hiyo, kufuatia kesi ya jinai namba 196/2012, iliyofunguliwa na Vedasto Mavubhi ambaye alimtuhumu mwenyekiti huyo kuchukua kwake kiasi hicho cha fedha, kwa ajili ya kumuuzia kiwanja. 

Hakimu Mahizi katika hukumu yake, alidai ameridhika na ushahidi uliotolewa na upnade wa mlalamikaji, mashahidi pamoja na wazee wa baraza hivyo kumhukumu mwenyekiti kwenda jela.
Alisema mwenyekiti huyo pamoja na Balozi Robert Byagaye wanastahili kutumikia kifungo hicho cha mwaka mmoja jela kutokana na kutiwa hatiani. 

"kitendo kilichofanywa na viongozi hawa, kuwaibia raia wanaowaongoza kiutapeli kwa kuwadanganya kuwauzia kiwanja na kisha kutafuta mtu bandia kwa madai kuwa kiwanja hicho kiko katika mtaa wanaouongoza, ni udanganyifu" Alisema hakimu na kuongeza kuwa Mwenyekiti huyo amehukumiwa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa viongozi wengine matapeli.

SHAA AJILINGANISHA NA AKINA DIAMONDA & OMMY DIMPOZ

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Sara Kaisi ‘Shaa’ amejinasibu kuwa kiwango alichonacho sasa hakina tofauti na wasanii wengine wakali kama Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ na Nassib Abdul ‘Diamond’.
                                                     Shaa akifanya vitu vyake.
Shaa aliyabainisha hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akifanya mahojiano na mwandishi wa habari hii aliyekuwa akitaka kufahamu kiwango cha fedha anachokipata katika shoo zake mbalimbali anazofanya.

“Hivi sasa kama mtu anaweza kumchukua Ommy ama Diamond kwa dau hilo analowapa, basi anaweza pia kunichukua mimi kwa shoo zake kwa kiwango cha nyota hao wawili, kwani uwezo ninao,” alisema.

Aliongeza kuwa ili kudumu katika fani ya muziki wa kizazi kipya, kunatakiwa kuongeza ubora wa kazi kwa kufanya kazi na wadau mbalimbali wa muziki wa ndani na nje ya nchi.
Shaa alisema kwa sasa wimbo wake wa ‘Lover Lover’ unaendelea kufanya vema katika vituo mbalimbali vya redio hapa nchini na Afrika Kusini, ambako video ya wimbo huo inachezwa zaidi.

MBUNGE ATAKA KILIMO CHA BANGI KIHALALISHWE TANZANIA

MBUNGE wa Nkasi,Ally Kessy (CCM) ametoa mpya bungeni baada ya kuuliza swali la kuitaka serikali ihalalishe kilimo cha bangi ili kujipatia fedha za kigeni.

Akiuliza swali la nyongeza jana, Kessy alisema kwa kuwa zao la tumbaku limekuwa likipigwa marufuku dunia nzima, lakini limendelea kulimwa na kuchangia pato la mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania, kwanini serikali isihalalishe kilimo cha bangi kama ilivyo kwa tumbaku ili kuchangia pato la taifa?
Swali hilo liliibua vicheko kwa wabunge wote, akiwemo Spika na Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula, Adam Malima.

Hata hivyo, Waziri Malima akijibu swali hilo alisema kuwa pingamizi dhidi ya zao la tumbaku duniani limepungua na zao hilo sasa ni moja ya mazao makubwa ya biashara.
Kuhusu bangi kuhalalishwa kuwa zao la biashara, Waziri Malima alisema kuwa katika nchi zingine imeruhusiwa kuwa moja ya zao la biashara na linachangia pato la taifa.

“Hapa nchini bado bangi haijaruhusiwa kuwa zao la biashara, lakini kama utafiti utafanyika na kubaini kama linaweza kupata soko la kuingizia pato taifa, tutaliangalia hilo,” alisema.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRILI 13, 2013

.

.
.
.
.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...