Saturday, August 17, 2013

MUME AFA GESTI AKIWA NA MKE WA MTU...!!!

Mke wa marehemu akisaidiwa kutolewa eneo la tukio

Kwa mujibu wa mtoa habari wetu (jina tunalo), Kipondo na mwanamke huyo, Latifa Suleiman (25), ni wakazi wa Kigogo, Dar ambao walifika   katika gesti hiyo kwa ajili ya kusaliti ndoa zao.

MTU ASIYEJULIKANA AGAWA FEDHA BURE JIJINI DAR....!!!

Bajaji wakiwa kwenye foleni kuwekewa mafuta na mtu ambaye hakutaka kujitambulisha
======  =========
Mwanamme mmoja, ambaye amekuwa akiongozana na maaskari polisi wawili, amekuwa akigawa fedha za bure kwa watu mbalimbali jijini Dar.

Kijana huyo wa makamo, ambaye kwa wiki hii nzima amekuwa akitajwa kwenye radio mbalimbali, aliwalipia bili wagonjwa wote waliokuwa wamelazwa hospitali ya Mwanyamala na Muhimbili, wodi ya wanawake.

Alkizungumza na mwandishi wetu,mmoja wagonjwa wa hospitali ya Muhimbili, Subira Juma alisema kijana huyo alikuja hospitali na kuuliza wangapi wanadaiwa halafu akawalipia bili zao na kisha kuondoka zake bila kujitambulisha.

‘Kwa kweli hata mimi sifahamu kijana huyu katokea wapi, lakini sijwahi kuona mtu akitoa hela bila kujuana, na kisha kuondoka billa kusema lolote’ alisema Subira.

Wakati huo huo, wasafiri wa daladala nao, hasa ziendazo Mbagala nao wametajwa kunufaika na mgawo huo, ambapo wamekuwa wakilipiwa nauli mara kadhaa na mtu huyo.

Mbali na kulipia watu usafiri, kijana huyo pia anatajwa kuwanufaisha maderva boda boda na bajaji kwa kuwawekea mafuta kwenye vyombo vyao vya usafiri.

POLISI FEKI AJITETEA...... ADAI KUWA NJAA NDO ILIMFANYA AJIFANYE TRAFFIC...!!!

 
MKANDA mzima wa askari bandia wa Kikosi cha Usalama Barabarani (trafiki), James Juma Hussein (45)  aliyekamatwa saa 1:30 asubuhi ya Agosti, 14, 2013 maeneo ya Tabata Kinyerezi Mnara wa Voda, jijini Dar es Salaam akiwa ndani ya sare zake za kazi, umepatikana....
 

Kwa nini James alikamatwa? Asubuhi hiyo, afisa mmoja wa trafiki mwenye cheo cha ukaguzi alikuwa akipita eneo hilo kwenda kazini, alipomwona James alisimamisha gari, akashuka kwenda kumsalimia. 


Lakini alishangaa kuviona vifungo vya shati lake ni vya kawaida (vya polisi vinatakiwa kuandikwa police force yaani ‘jeshi la polisi’), akamtilia shaka. 

WAISLAMU MSIKITI WA MTAMBANI 'WAMTEKA' ASKARI POLISI.... !!!


Baadhi ya waumini wa Kiislamu Msikiti wa Mtambani wakiwa wamemzunguka askari Polisi, Jonathan Tossi (katikati aliyeshika kamera) wakimuhoji baada ya kumshikilia kwa muda, hata hivyo walimuachia kwa masharti ya kumtaka afute picha zote alizopiga eneo hilo.
Askari Polisi wakizunguka doria eneo la Msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam kuhakikisha kuna amani.
Askari wa Jeshi la Polisi, Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakizunguka kufanya doria maeneo mbalimbali ya jijini la Dar es Salaam kuhakikisha kuna amani. (Picha kwa hisani ya Gazeti la Jambo Leo.)

TAARIFA YA HARAKATI YA JUMUIYA NA TAASISI ZAKIISLAM TANZANIA KWA VYOMBO VYA HABARI..!!!


Bismillar Rahmanir Rahiim
JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM (T)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA KUCHUKULIWA NA POLISI SHEIKH PONDA ISSA PONDA TOKA HOSPITALI

Jana asubuhi majira ya saa nne na nusu askari wa jeshi la Polisi na watu wanaoaminika kuwa usalama wa taifa walikwenda hospitali ya Muhimbili (MOI) na kumchukua Sheikh Ponda Issa Ponda. Juhudi za Sheikh Mwenyewe, mkewe na waislam waliokuwepo pale hospitali kutaka abaki hospitalini kuendelea na matibabu hazikuzaa matunda. Mpaka Sasa bado tunafuatilia kujua mahali Kiongozi huyo wa Kiislam alikopelekwa.

Tumepokea kwa masikitiko makubwa sana habari hizi na tunashindwa kuamini kama mambo haya yanaweza kufanywa na Serikali inayodai kutawala kwa kufuata utawala bora unaojali sheria, uadilifu, utu na uhuru wa kujieleza.

Kitendo cha kumpiga risasi Sheikh Ponda na kisha kumchukua toka hospitalini na kumpeleka Gerezani kwa kukiuka taratibu ni kinyume cha haki za binadamu, utawala bora na uhuru wa maisha ya mtu. Matibabu ni haki mojawapo kwa binadamu yoyote hata kama kuna wanaomtuhumu. Tuhuma juu ya mtu si sababu ya kukiuka taratibu, kuvunja sheria na hata kumtisha unayemtuhumu kwani njia hiyo haiwezi kutatua tatizo bali inalifanya kuwa kubwa zaidi.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI AGOSTI 17, 2013

.

.

MWAKYEMBE ATIMUA WOTE WALIOHUSIKA KUSINDIKIZA MSAFARA WA MADAWA YA KULEVYA KWENDA SAUZI AFRIKA

Waziri wa Uchukuzi,Mh.Dkt. Harison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari jana  ofisini kwake jijini Dares salaam juu ya hatua zilizochukuliwa na Wizara ya Uchukuzi juu ya sakata la madawa ya kulevya yaliyokamatwa huko Afrika Kusini hivi karibuni.Dkt. Mwakyembe amewafukuza kazi mtandao mzima uliohusika kusaidia kusafirisha madawa hayo, pia Waziri Mwakyembe ameliagiza jeshi la Polisi kuwakamata wafanyakazi hao na kuwaunganisha na wenzao kujibu mashitaka ya jinai.
Waziri wa Uchukuzi,Mh.Dkt. Harison Mwakyembe akionyesha picha ya Msanii Agness Gelard maarufu kwa jina la Masogange mbele ya waandishi wa habari,masogange alikamatwa na madawa ya kulevya huko nchini Afrika Kusini hivi karibuni.
waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Uchukuzi akiwa anafafanua hatua zilizochukuliwa na Serikali kuushughulikia mtandao mzima uliosaidia kupitisha madawa ya kulevya.

ANGALIA PICHA ZA RAIS KIKWETE AKIWASILI NCHINI MALAWI JANA

8E9U4456 8E9U4461 8E9U4487 8E9U4488

WABUNGE 11 WA TANZANIA WANUSURIKA KIFO BAADA YA BUS WALILOKUWA WAKISAFIRI​A KUANZA KUUNGUA


wabunge wakoswa ca547
Wakati msafara wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ukielekea Wilayani Missenyi kukagua sehemu utakapojengwa uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Omukajunguti, gari aina ya Costa lenye namba za usajili T 570 BYU lilowabeba Waheshimiwa Wabunge 11 lilipata hitilafu na kutaka kuungua.
P.T
wabunge tena 5ee72
Ajali hiyo ilitokea eneo la Mwanzo Mgumu kilometa moja kutoka mpakani mwa Wilaya ya Bukoba na Wilaya ya Missenyi ambapo gari hilo aina ya costa lilianza kutoa moshi mwingi kwa upande wa nyuma wakati likiwa kwenye mwendo mkali na kuleta hofu kubwa kwa abiria walikuwemo ndani ya gari hilo.

WAKILI WA PONDA ANENA JUU YA SHEIKH PONDA

Wakili wa Sheikh Ponda

Wakili wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda (54) ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi mpya ya kufanya uchochezi katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Nassor Jumaa, amesema kuwa amesikitishwa na hatua  ya vyombo vya dola kumuondoa Ponda aliyekuwa  amelazwa katika wodi ya Kitengo  cha Taasisi ya Tiba  ya Mifupa  na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu(MOI)  alikokuwa akipatiwa matibabu na kisha kumwamishia katika gereza la Segerea.


Wakili Jumaa alisema amesikitisha na kitendo hicho kwani hakimu Hellen Riwa juzi muda mfupi baada ya wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka kumaliza kumsomea shitaka Ponda, hakimu Liwa alitoa amri ya Ponda aendelee kukaa chini ya ulinzi lakini cha kushangaza leo,wanausalama wamemtoa wodini na kumpeleka katika gereza la Segerea na kwamba atalazimika kurudishwa tena mahakamani siku kesi yake itakapojatwa Agosti 28 mwaka huu, ambapo upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...