Saturday, November 02, 2013

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, HAYA HAPA......!!!

Matokeo ya Darasa la Saba yametangazwa leo na mwaka huu ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 30.72 mwaka jana mbaka asilimia 50.61 mwaka huu kutokana na wanafunzi walio fanya mtihani mwaka huu wa darasa la saba wamefaulu zaidi ukilinganisha na wanafunzi wa mwaka jana.
Kaimu mtendaji wa Baraza la Mtihani Charles Msonda amesema ufauru katika masomo yote umepanda kwa asilimia kati ya 6.01 na 28.06 ukilinganisha na mwaka 2012 Mwaka huu watainiwa wamefahulu zaidi katika somo la Kiswahilin kwa asilimia 69.06 na somo walilio faulu kwa kiwango kidogo zaidi ni somo la Hisabati wamefaulu kwa asilimia 28.62 Msonda amesema jumla ya watahiniwa 427,606 kati ya 844,938 walio fanya mtihani huo wamepata alama ya 100 kati ya alama ya 250 idadi hiyo nisawa na asilimia 50.61

ANGALIA MATUKIO KATIKA PICHA: MBEYA CITY FC YAIBAMIZA ASHANTI UNITED GOLI MOJA BILA.

Timu ya Ashanti United ikiwa katika picha ya pamoja kabla ya Mpira  kuanza 
 Timu ya Mbeya City Fc ikiwa katika Picha ya Pamoja Kabla ya mpira kuanza 

KIONGOZI WA TALIBAN NCHINI PAKISTAN, AUAWA

131102043401_hakimullah-mehsud_2d5a2.jpg
Kiongozi wa kundi la wapiganaji la Taliban nchini Pakistan, Hakimullah Mehsud, ameuawa kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani, hii ni kwa mujibu wa afisaa mmoja mkuu wa kundi hilo.
Shambulizi hilo lililenga gari alimokuwa anasafiria Mehsud, Kaskazini Magharibi mwa Waziristan.
Watu wanne waliokuwa wanasafiri na Mehsoud wakiwemo walinzi wake wawili waliuawa katika shambulizi hilo.
Marekani pamoja na Pakistan zimewahi kudai siku za nyuma kumuua Mehsoud ingawa madai yao hayakuwa na ukweli.
Serikali ya Pakistan imetoa taarifa kulaani vikali mashambulizi ambayo Marekani inafanya kwa kutumia ndege zisizo na rubani, ikisema kuwa mashambulizi kama hayo yanakiuka uhuru wa taifa hilo.
Shambulizi hilo lililofanywa siku ya Ijumaa, lililenga gari la Mehsud.
Afisaa mmoja mkuu wa ujasusi nchini Marekani, aliambia shirika la habari la Associated Press kuwa Marekani ilipokea taarifa muhimu kuthibitisha kifo cha Mehsoud.
Hata hivyo msemaji wa baraza la usalama wa kitaifa la Marekani, alisema kuwa hawawezi kuthibitisha taarifa hizo lakini ikiwa ni kweli basi ni pigo kubwa sana kwa Taliban.
Hakimullah Mehsud alijulikana sana mwaka 2007 kama kamanda wa mwasisi wa kundi hilo Baitullah Mehsud, alipowakamata wanajeshi 300 wa Pakistani .

MASHABIKI SIMBA WATAKA WACHEZAJI WAKONGWE WARUDISHWE


mashabiki_wa_simba_wakifurahia_ushindii_dc4d7.jpg
MASHABIKI WA SIMBA 
Mashabiki Simba wamepiga kelele na kutala benchi lao la ufundi libadilike na kuwarudisha wachezaji wakongwe.
Zaidi ya mashabiki waliotuma ujumbe mfupi kupitia barua pepe na wale waliopiga simu ya mkononi ya SALEHJEMBE, wamemtaka Kocha Mkuu, Abdallah Kibadeni na wasaidizi wake kufikiria na kugeuza misimamo waliyonayo.
"Kweli Kibadeni anatuangusha, ni kocha mkongwe lakini anaonyesha hana msimamo, ninahisi anaburuzwa na watu wengine maana anatoa uamuzi ambao unaonyesha kuna chuki. Wakongwe warudishwe," alisema Mohammed Kassim.
Juma Mroki, Thomas Mapunda waliojitambulisha wanaishi Dar es Salaam na Songea, walisema wakongwe ndiyo tatizo la timu hiyo.
"Angalia tumeongoza hadi dakika ya 90, lakini tumeshindwa kujilinda. Uzoefu pia ni jambo muhimu, wakongwe wasidhalauriwe eti kwa kuwa tuna vijana."
Baadhi ya wachezaji wakongwe wa Simba ambao wameshushwa kikosi cha pili ni Henry Joseph na Ramadhani Chombo 'Redondo'.
Lakini mshambuliaji mwenye kasi, Haruna Chanongo, naye ameshushwa kikosi cha pili kwa kuwa tu alishindwa kucheza vizuri mechi moja dhidi ya Yanga!
Mashabiki Simba, jana walifanya vurugu baada ya timu yao kushindwa kulinda bao na Kagera wakasawazisha katika dakika za nyongeza.
Walifanya vurugu na kuvunja viti huku baadhi yao wakiumia baada ya askari polisi kupambana nao wakati wakijaribu kuzuia vurugu hizo.
Simba imekuwa ikisonga kwa mwendo wa kusuasua na kusababisha kuendelea kuporomoka na sasa iko katika nafasi ya nne baada ya Yanga walioshika usukani jana, Azam FC na Mbeya City.
Chanzo: salehjembe

JELA MAISHA KWA UBAKAJI

kana_mbakaji_512x288_bbc_nocredit_fc7c2.jpg
Johannes alikiri kumbaka Anene lakini alikanusha madai ya kumuua
Mwanamume mmoja nchini Afrika Kusini aliyepatikana na hatia ya ubakaji na mauaji ya msichana mwenye umri wa miaka 17 amepewa hukumu mbili za maisha jela na mahakama moja viungani mwa mji wa Cape Town.
Viongozi wa mashitaka walitaka mshukiwa Johannes Kana afungwe jela maisha bila dhamana.
Marehemu Anene Booysen alifariki mwezi Februari , masaa kadhaa baada ya kuuawa kinyama katika kesi ambayo imewaghadhabisha wengi.
Afrika Kusini ni nchi mojawapo yenye visa vingi vya ukatili wa kijinsia duniani.
Mwandishi wa BBC Nomsa Maseko aliyefika katika mahakama ya Swellendam, umbali wa kilomita 220 kutoka mji wa Cape Town, anasema kuwa mjombake Kana alishanga kwa kupiga makofi na hata kuangua kicheko jaji alipotoa uamuzi wake.
" Hiki ni kichekesho ," alisema huku akiongeza kuwa mfumo wa sheria hauna haki
Lakini wengi waliohudhuria kesi hiyo walihisi kama haki imetendeka
Bi Booysen alitendewa ukatili na mwili wake kutupwa karibu na nyumba yake Bredasdorp lakini alifariki baadaye hospitalini mjini Cape Town
Wakati huohuo, Rais Jacob Zuma alitaja mauaji hayo kama ya kushtua na ya kinyama.
Ametoa wito kwa majaji kutoa adhabu kali sana kwa wanaofanya vitendo vya uhalifu wa kijinsia.
Wakati wa kesi dhidi ya Kana, madaktari waliomtibu Bi Booysen walisema kuwa majereha aliyoyapata yalikuwa mabaya zaidi kwake kuwahi kuyashuhudia.
Kabla ya kifo chake alisema kuwa karibu wanaume watano au sita walihusika na shambulizi dhidi yake , lakini washukiwa watatu walikamatwa baadae ingawa ni mmoja tu aliyehukumiwa.
Kana alikiri kosa la ubakaji ingawa alikana kuwa alimuua.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...