Monday, May 05, 2014

LUIS SUAREZ KAFNYA YAKE TENA

Screen Shot 2014-05-05 at 3.48.52 PM 
Wiki mbili baada ya kutangazwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya England kupitia chama cha wanasoka wanaocheza EPL mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay Luis Suarez ambae ni miongoni mwa mastaa wa soka waliowahi kumiliki headlines kwa kipindi kirefu, amechaguliwa tena kuwa mwanasoka bora wa England na chama cha waandishi wa habari za michezo Uingereza.
Suarez mwenye umri wa miaka 27 aliwashinda kwa kura nyingi wachezaji wengine akiwemo nahodha wa Liverpool na England Steven Gerrard.
article-2620532-1D69BE9B00000578-539_306x423 
Magoli 30 aliyofunga msimu huu kwenye EPL yameiweka Liverpool kwenye nafasi ya kutwaa ubingwa wa Premier League baada ya miaka 24.  Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Hii ndio listi ya washindi wa tuzo hiyo tangu mwaka 1990 mpaka leo
1989–90     John Barnes          
1990–91     Gordon Strachan
1991–92     Gary Lineker
1992–93     Chris Waddle
1993–94     Alan Shearer
1994–95     Jurgen Klinsmann
1995–96     Eric Cantona
1996–97     Gianfranco Zola
1997–98     Dennis Bergkamp
1998–99     David Ginola
1999–00     Roy Keane
2000–01     Teddy Sheringham
2001–02     Robert Pires
2002–03     Thierry Henry
2003–04     Thierry Henry
2004–05     Frank Lampard
2005–06     Thierry Henry
2006–07     Cristiano Ronaldo
2007–08     Cristiano Ronaldo
2008–09     Steven Gerrard
2009–10     Wayne Rooney
2010–11     Scott Parker
2011–12     Robin van Persie
2012–13     Gareth Bale

MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 05, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAPIGANO MAKALI YAANZA TENA SUDAN KUSINI

Wanajeshi wa Sudan Kusini
Mapigano makali yamekuwa yakiendelea katika mji wa Bentiu nchini Sudan Kusini ambapo vikosi vya serikali vinajaribu kuurejesha mji huo uliotekwa na waasi.
Mwandishi wa Habari wa BBC aliyeandamana na kikosi cha Umoja wa Mataifa nje ya mji huo anasema amesikia milio ya bunduki na silaha nzito nzito ambapo pia ameona kikosi cha majeshi ya serikali kikijipanga.
Hata hivyo amesema bado haijajulikana ni kundi gani kwa sasa linaloshikilia mji huo wa wenye utajiri wa mafuta.
Kwa upande serikali nchini Sudan kusini inasema majeshi yake yameudhibiti mji wa huo na ngome ya waasi ya Nasir.
Baadhi ya wakimbizi wa Sudan Kusini waliokimbia makazi yao hivi karibuni kutokana na vita
Mjumbe wa Umoja wa mataifa mjini humo anasema mji huo umedhibitiwa upya na kikosi cha serikali katika operesheni kubwa iliyoanza hapo jana Jumapili.
Shambulio hilo linajiri siku mbili baada ya rais Salva Kiir kumwambia Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry, kwamba yupo tayari kufanya mazungumzo ya amani ya moja kwa moja na kiongozi wa waasi, Riek Machar. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Chanzo BBC

HUKUMU YA WANAJESHI WABAKAJI DRC LEO

Wanajeshi wa serikali ya DRC
Hukumu inatarajiwa kutolewa baadaye leo kwenye kesi inayowahusu wanajeshi 39 wanaotuhumiwa kuendesha ubakaji na uhalifu wa kivita nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.
Wanajeshi hao wanatuhumiwa kusababisha machafuko yanayoendelea kwenye mji mdogo wa Minova ulio mashariki mwa nchi hiyo mwaka 2012.
Waasi wa M23 ambao wanadaiwa nao kujihusisha na vitendo vya ubakaji
Wakati wa machafuko hayo maelfu ya wajeshi wa serikali walikuwa wakirudi nyuma baada ya kupoteza mji wa Goma kwa waasi wa M23 .
Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa wanajeshi hao waliwabaka karibu wanawake na wasichana 135.
Matukio ya ubakaji yameenea katika eneo la mashariki mwa Congo na yanaidiwa kufanywa na askari wa pande zote mbili waasi na wale serikali. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...