Friday, August 09, 2013

JAJI MUTUNGI AANZA KUTUMA SALAMU ZA UTENDAJI KAZI WAKE ....!!!



Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman akimpongeza Francis Mutungi baada ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Jaji wa Mahakama Kuu katika hafla iliyofanyika Ikulu, Juni 19,2012. Jaji Mutungi jana aliteuliwa kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa. Picha na Maktaba. 
********
Dodoma. Msajili mteule wa Vyama vya Siasa nchini,  Jaji Francis Mutungi amewataka Watanzania kutulia na kusubiri utendaji wake atakapokabidhiwa rasmi jukumu hilo jipya alilopewa na Rais Jakaya Kikwete.
Mutungi aliteuliwa kushika wadhifa wa msajili wa vyama vya siasa kuchukua nafasi ya John Tendwa ambaye amestaafu. Tendwa aliiongoza taasisi hiyo kwa miaka 13.
Mutungi alisema: “Ninafahamu nina majukumu mazito mbele yangu, lakini siwezi kusema chochote kwa kuwa sijakabidhiwa rasmi ofisi. Ninachotaka kusema ni kwamba nitakuwa mtumishi wa kila mmoja.”

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI SWALA YA SIKUKUU YA IDDI KITAIFA MKOANI TABORA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa salamu maalum za Sikukuu ya Iddi baada ya Swala iliyofanyika Kitaifa Mkoani Tabora katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi leo.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa sita kutoka kulia), akishiriki na waumini wa dini ya Kiislamu katika Swala ya Sikukuu ya Iddi, iliyoswaliwa Kitaifa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora leo.

SIMBA KUADHIMISHA SIMBA DAY KESHO TEREHE 10.

KESHO, Jumamosi tarehe 10 Agosti mwaka 2013, klabu ya soka ya Simba itaadhimisha kile kinachoitwa Siku ya Simba (SIMBA DAY) katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 
Utaratibu wa kuwa na Simba Day ulianzishwa na klabu kwa lengo la kuwa na siku ambapo wapenzi, wanachama, viongozi, wachezaji wa zamani na wa sasa pamoja na watu wengine mashuhuri, hukutana kwa pamoja na kusherehekea klabu ambayo imewafanya wawe wamoja pamoja na tofauti nyingi walizonazo.
 
Mwaka huu, shughuli hiyo itafanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine, Simba SC inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki na klabu ya soka ya Sports Club Villa kutoka nchini Uganda.
Katika kusherehesha tukio hilo, wasanii maarufu kama vile Juma Nature, Tunda Man na Snura maarufu kwa jina la ‘Mama Majanga’ watatumbuiza uwanjani hapo.

MUME WA JOYCE KIRIA, HENRY KILEWO AWALIZA WATU KWENYE MKUTANO MABIBO SAHARA

Leo akiwa anawahutubia wakazi wa mabibo-Sahara kwa mara ya kwanza toka atoke jela huko gereza la uyui- Tabora ktk mkutano ambao mgeni rasmi alikua John Mnyika, aliwaliza baadhi ya wananchi waliofika katika mkutano huo. Hii kutokana na kuguswa na hotuba ya kamanda Kilewo ambayo ilikua inaudhunisha kutokana na simulizi ya namna alivyokamatwa na huko jela namna ya watu waliofungwa pasipo na hatia.

kiukweli inasikitisha, lakini bado alisisitiza kwa kusema 'hakuna dhambi kubwa hapa duniani kama uoga' na ' watatupiga kwa mabomu na watatu ua kwa risasi lakini na wao watakufa kwa presha ya dhambi

WANYARWANDA 520 WATII AGIZO LA RAIS KIKWETE LA KUONDOKA NCHINI

044 2423a 
Zikiwa zimesalia saa 48 kabla ya kumalizika kwa muda uliotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa wahamiaji haramu kuondoka nchini au kuhalalisha ukaazi wao na wenye silaha kuzisalimisha, makundi ya wahamiaji hao, yameanza kuondoka kwa hiari.
Wastani wa wahamiaji haramu 150 wanaendelea kujiandikisha kuvuka mpaka katika Kituo cha Rusumo, Ngara mkoani Kagera kutekeleza agizo hilo.

Ofisa Uhamiaji wa Kituo cha Rusumo, Samweli Mahirane alisema mpaka sasa Wanyarwanda 520 wameshaondoka katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Ngara na kurejea makwao huku Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fabian Massawe akisema silaha 17 za aina mbalimbali zimesalimishwa.
Mahirane alisema wahamiaji hao wanatokea katika vijiji vya Wilaya za Ngara, Karagwe, Kyerwa, Biharamulo na Geita pamoja na Runzewe na wamekuwa wakiishi katika maeneo hayo bila vibali halali. (HM)

"Kuondoka kwa hiari kwa wahamiaji haramu, kutahitimishwa Jumatatu Agosti 12 na baada ya tarehe hiyo, vyombo vya dola vitaanza kufanya kazi kama agizo la Rais Kikwete lilivyoelekeza katika Mikoa ya Kagera na Kigoma," alisema.
Aliwahakikishia wahamiaji hao usalama katika mataifa yao kwani hivi karibuni Serikali ya Rwanda ilikubali kuwapokea hata walio na mifugo kwa masharti kuwa ndani ya kipindi kifupi wataipunguza kwa kuiuza na kuboresha maisha yao.

"Rwanda wanahitaji mifugo michache, hivyo walio na mingi wanatakiwa kuipunguza kwa kuuza na kujenga makazi bora ikiwa ni pamoja na kuhifadhi ama kulinda mazingira ya nchi hiyo," alisema Mahirane. Chanzo: mwananchi

MOURINHO: HATUTAKATA TAMAA MPANGO WA KUMSAJILI ROONEY...!!!

jose 13f47
Jose Mourinho amesisitiza kwamba atapigana mpaka siku ya mwisho katika jaribio lake la kumsaini Wayne Rooney. (HM)

Chelsea tayari walishatuma ofa mbili ambazo zimekataliwa na Manchester United, ofa ya mwisho inayotajwa kuwa ni zaidi ya paundi million 25 ilitumwa jumapili. Lakini Mourinho alisema: "Hatuna kizuizi cha muda kwenye suala hili.

'Tumemuona Rooney kama ni mchezaji ambaye tungependa kuwa nae. Tumefanya kila kitu katika utaratibu unaopaswa na tutafanya hivyo mpaka siku ya mwisho ya usajili. Tunafnya kila kitu tukizingatia sheria, kutoa ofa rasmi kwa klabu moja kwa moja.
 

'Hakujawahi kuwepo kwa mawasiliano na mchezaji, hakijatokea kitu kama hicho. Tusubiri tuone kama mambo yatabadilika.'

Rooney inaaminika kwamba amemwambia kocha wake David Moyes kwamba anataka kuondoka, lakini United imekuwa ikisisitiza kwamba hauzwi. Chanzo: shaffihdauda

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...