Thursday, December 22, 2016

UWEZO WA WANAWAKE KUPATA MIMBA WASHUKA TANZANIA

Viwango vya wanawake kuweza kupata mimba nchini Tanzania vimepungua hadi 5.2 kwa kila mwanamke nchini Tanzania mwaka 2015/2016 kutoka 6.2 kwa kila mwanamke miaka ya 1991/92, kulingana na utafiti wa afya nchini humo

Kulingana na gazeti la The Citizen la nchini Tanzania, utafiti huo uliofanywa na kutolewa na Afisi ya kitaifa ya Takwimu nchini humo NBS wiki iliopita unaonyesha kushuka kwa viwango vya uwezo wa kushika mimba miongoni mwa wanawake .

Kwa mfano mwaka 1996 ripoti hiyo inaonyesha watoto 5.8, mwaka 2004/05} ni watoto 5.7 mwaka 2010 ni watoto 5.4.

WAJUMBE WAIDHINISHA USHINDI WA TRUMP

Wajumbe wa jopo la wateule wanaoamua ushindi wa rais wa Marekani, wamemwidhinisha Donald Trump kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Novemba 8, mwaka huu.

Hatua hiyo imezima juhudi za dakika za mwisho za kutaka kumzuia Trump kuingia ikulu ya White House Januari 20.

Baada ya ushindi huo, Trump ameahidi ‘kufanya kazi kuunganisha nchi yake na kuwa rais wa Wamarekani wote’.

RAIS WA GAMBIA ASEMA HANG'ATUKI MADARAKANI NG'OO............!!!

Rais wa Gambia Yahya Jammeh ameonya kuwa atakataa jaribio lolote la viongozi wa kieneo kumlazimisha kuondoka madarakani licha ya kushindwa katika uchaguzi na mfanyibiashara Adama Barrow.

Akihutubia wanachama wa muungano wa Bar Afrika nchini humo Bw Jammeh alisema: ''Waje wajaribu kuniondoa.wanasubiri nini? mimi ni mtu mpenda amani lakini haimaanishi kwamba sitalitetea taifa langu, kwa ujasiri na uzalendo na kuibuka mshindi''.

Amesema kuwa alikataa wito wa muungano wa viongozi wa mataifa ya Magharibi ECOWAS akiwemo rais Muhammadu Buhari wa Nigeria na Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia kuondoka nchini Gambia.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...