Friday, May 03, 2013
SHILOLE......... "BILA CONDOM HUWEZI KULIFAIDI PENZI LANGU HATA UKINIHONGA MABILIONI"
Mwigizaji na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Zena Mohamed, maarufu kwa jina la shilole
amedai kuwa anaweza kufanya ujinga wowote humu duniani lakini
linapokuja suala la mapenzi kamwe hawezi kwenda pekupeku ( bila condom
) ....
Akiongea
kwa kujiamini ,Shilole alisema kuwa hata mtu awe vipi, au awe wa dini
gani au awe na pesa kiasi gani kamwe hawezi kumvulia nguo kama hana
kondom mkononi.....
Msanii
huyo alienda mbali zaidi na kuzilaani kauli za baadhi ya
watu zinazosema eti ukitumia "CONDOM" ladha ya mapenzi inapungua.Yeye
anadai kuwa ni mdau wa "GEMU" hilo na huwa anatumia NDOM
kama kawa na hufurahia kama kawaida...
WOLPER "NAJUTA KUJIINGIZA KWENYE MAPENZI"...!!
DIVA
wa kiwango cha juu cha filamu hapa Bongo, Jacqueline Wolper,
ameonekana kujutia historia yake ya kimapenzi baada ya kufungukia
kitendo cha yeye kumuanika kila aliyekuwa akimpenda kwamba kimemtibulia
na sasa amejifunza kutokana na makosa.
Jacqueline Wolper.
Akizungumza
na Ijumaa hivi karibuni, Wolper alisema kuwa, kwenye maisha yake ya
huko nyuma ameshajianika akiwa na wapenzi tofauti lakini sasa
atakayempa nafasi kwenye moyo wake hatamuanika ila hilo litakuja
baadaye sana kwani sasa hivi kaweka pembeni kwanza mambo ya mapenzi.
“Sitaki
yajirudie yaliyotokea katika maisha yangu ya huko nyuma, hata hivyo
sasa hivi niko bize sana na kazi, mambo ya wanaume nimeamua kuyaweka
pembeni kwanza,” alisema Wolper na kuongeza:
“Sitaki itokee kama
ilivyokuwa kwa Dallas ambapo kila mtu alijua alikuwa ni mtu wangu, kwa
sasa nimeamua kutulia kwanza na hata nikimpata mwingine watu hawatamjua
hadi wakati wa ndoa.”
BREAKING NEWZZZZZZZZZZZZZ!!!! : MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 KUSAHISHWA UPYA,
MCHUMBA WA MTU ATUPWA JELA KWA KUJIUZA...........!!!
Na Richard Bukos
MREMBO
Brandina Barthon (24), Jumatatu iliyopita alihukumiwa kwenda jela miezi
6 baada ya kupatikana na hatia kwenye kesi ya ukahaba iliyokuwa
ikimkabili katika Mahakama ya Sokoine Drive (Jiji) jijini Dar.
Brandina
alisomewa hukumu hiyo na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, William
Mutaki ambaye alisema kutokana na ushahidi uliothibitika, mahakama hiyo
inamhukumu kwenda jela miezi 6, ili liwe fundisho kwa wengine.
Hukumu
hiyo ilimfanya mrembo huyo kuchanganyikiwa na kuangua kilio lakini
mheshimiwa hakimu aliamua kukazia hukumu yake bila ya kupepesa
macho.
Wakati
mwanamke huyo akiangua kilio, afande wa Jeshi la Magereza alimfikia na
kumchukua kwa ajili ya kumpeleka kwenye Karandinga kuelekea Gereza la
Segerea kuanza maisha ya jela.
Mbali
na Brandina, mwanaume aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wa mtuhumiwa huyo
aliyekuwa akifuatilia kesi hiyo naye alimwaga machozi baada ya kutolewa
hukumu hiyo.
HII NDIO LIST KAMILI YA VIONGOZI WA TANZANIA NA WA KIMATAIFA WALIOJIUNGA FREEMASONS
Siri ya List za Viongozi wa Tanzania Yatajwa (Secret Society), Freemason, imedaiwa kuwa na siri nzito na viongozi wakuu wa nchi yetu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
MWINYI NA ANDY CHANDE
| |
Andy ChandeKikubwa kinachodaiwa ni kuwa Chande anatumiwa na Freemason kuhakikisha kwamba kila kiongozi wa nchi hii anakuwa karibu na jamii hiyo ya siri.
Inazidi kudaiwa kuwa Freemason inafanya njama za hali ya juu kujiweka karibu na Ikulu, ikiwa na mpango wao wa muda mrefu wa kusimika rais ambaye ni memba wa jamii hiyo katika awamu zinazokuja.
Uchunguzi umeonesha kuwa Chande amekuwa karibu na Ikulu tangu Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na amedumu kujiweka karibu na viongozi wa nchi mpaka awamu hii ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete.
NEEMA YAWASHUKIA WALIOFELI .... MATOKEO YA KIDATO CHA NNE KUPANGWA UPYA
TUME ya kuchunguza sababu za kufeli kwa kiasi kikubwa kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliofanya mitihani ya kuhitimu mwaka 2012 imekamilisha kazi yake na taarifa za uhakika zilizolifia gazeti hili zinasema , upangaji alama zao utafanyika upya.
Kama ambavyo gazeti hili lilivyobaini katika uchunguzi wake wa kiuandishi kwamba kulifanyika mabadiliko ya utoaji alama kwa ajili ya mitihani waliyofanya wanafunzi mwaka huo (2012) bila maandalizi kwa wadau, tume hiyo imependekeza alama zipitiwe upya (regrading).Katika alama za awali, alama D anapoyopewa mtahiniwa baada ya mtihani wake kusahihishwa ilikuwa ni kuanzia alama 21 kwenda mbele na F ilikuwa 20 kushuka chini lakini katika mabadiliko yaliyoleta ‘maafa’ ya kufeli kwa watahiniwa wa mwaka jana, alama D ilianzia 35 na kuendelea, wakati ile ya kufeli (F) ilianzia alama 34 kushuka chini.
Subscribe to:
Posts (Atom)