Mmoja
wa viongozi katika mapinduzi yaliyozimwa nchini Burundi hivi karibuni
ya kumpindua Rais Piere Nkurunziza ameiambia BBC kuwa waasi wao wamekuwa
wakiwapa mafunzo polisi na askari kwa ajili ya jaribio jingine la
kumwondoa rais Pierre Nkurunziza.
Akiwa uhamishoni Generali Leornard Ngenda Kumana amekanusha kuwa walisaidia na mataifa ya nje. Wamekuwa
wakimshutumu Rais Nkurunziza kuwa kusababisha vurugu kaati ya jamii ya
wahutu na watutsi na kuwapa silaha wapiginaji wa vijana waoiunga mkono
serikali ambao wanaonekana wengi ni kutoka jamii ya wahutu.
Zaidi ya watu laki moja wamekimbia nchi hiyo wakihofia vurugu wakati wa uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo.
Wanaompinga wanasema hatua ya kugombea urais kwa muhula wa tatu kwa rais huyo ni kinyume cha katiba. Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.