Sunday, May 18, 2014

MBWANA SAMATA NA THOMAS ULIMWENGU WAJIUNGA TAIFA STARS KIKABILI ZIMBABWE LEO

Samata 
Na Boniface Wambura, Dar es  salaam
Wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wametua Dar es Salaam jana (Mei 17 mwaka huu) mchana, na kujiunga moja kwa moja kwenye kambi ya Taifa Stars kwa ajili ya michuano ya Afrika dhidi ya Zimbabwe (Mighty Warriors).
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza ya michuano hiyo itafanyika leo (Mei 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
Washambuliaji hao wa Taifa Stars wamewasili saa 7.25 mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines wakitokea Khartoum, Sudan ambapo juzi (Mei 16 mwaka huu) timu yao ya TP Mazembe ilicheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal ya huko.
Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mechi hiyo, kwani kimepata mechi za kirafiki na mazoezi ya kutosha kwenye kambi iliyoanzia Tukuyu mkoani Mbeya ambapo kulikuwa na utulivu mkubwa.
Naye Kocha Msaidizi wa Zimbabwe, Kalisto Pasuwa amesema hawaifahamu vizuri Taifa Stars lakini wamekuja kwenye mechi hiyo itakayoanza saa 10 jioni kwa ajili ya kushinda, na kuwataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona kiwango cha timu yake.
Milango kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Ghana wakiongozwa na Joseph Odartei Lamptey itakuwa wazi kuanzia saa 6 kamili mchana, na tiketi zitapatikana katika magari maalumu uwanjani hapo.
Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, kijani na bluu, sh. 10,000 kwa VIP C na B, na sh. 20,000 kwa VIP A. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MEI 18, 2014 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.

.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

RAIA WA UCHINA WAJERUHIWA VIETNAM

Shirika rasmi la habari nchini Uchina Xhinua limesema kuwa serikali imewaondoa zaidi ya raia wake 3000 kutoka nchini Vietnam kufuatia ghasia dhidi raia wa Uchina nchini humo.
Wafanyikazi wawili wa Uchina wameuawa kufuatia ghasia hizo zilizosababishwa na hatua ya Uchina kupeleka meli yake ya kuchimba mafuta katika eneo linalozozaniwa kusini mwa bahari ya Uchina.
Mapema hii leo takriban raia 16 wa Uchina waliojeruhiwa vibaya waliondoshwa nchini humo kupitia usafiri wa ndege maalum.
Serikali mjini Beijing inaandaa safari nyingine za ndege huku naibu waziri wa maswala ya kigeni Liu Jianchao akizuru Vietnam kwa mazungunmzo na mamlaka.
Aidha waziri huyo amewatembelea baadhi ya raia wa Uchina waliojeruhiwa hospitalini.
Wanaharakati nchini Vietnam wameitisha maandamano zaidi dhidi ya raia wa Uchina hii leo licha ya mwito wa serikali wa kutaka kusitishwa kwa maandamano hayo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Chanzo: BBC Swahili

WATU 70 WAUAWA KATIKA VITA NCHINI LIBYA

Mwanamgambo nchini Libya
Maafisa nchini Libya wanasema kuwa idadi ya watu waliofariki katika vita mjini Benghazi imeongezeka na kufikia zaidi ya 70.
Jeshi limetangaza kwamba hakuna ndege itakayoruhusiwa kupaa juu ya mji huo huku spika wa bunge akisema kuwa mtu anayeongoza vita hivyo Khalifa Haftar anajaribu kufanya mapinduzi.
Bwana Haftar amesema kuwa ataendelea na kampeni yake ya kuwaondoa wale aliowataja kama magaidi nje ya mji wa Benghazi huku akiongezea kuwa anaungwa mkono na raia wengi wa mji huo ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini Libya.
Hatahivyo familia nyingi zinahamia magharibi mwa mji huo kufuatia vita vikali kati ya vikosi vya Haftar na wanamgambo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Chanzo: BBC Swahili

ARSENA BINGWA KOMBE LA FA

BAO la dakika ya 109 la Aaron Ramsey limeipa Arsenal ubingwa wa Kombe la FA baada ya kuichapa Hull City 3-2 ikitoka nyuma kwa 2-0 Uwanja wa Wembley.
Ramsey alifunga bao hilo akimalizia kazi nzuri ya Olivier Giroud na kuondoa uwezekano wa mchezo huo kuhamia kwenye mikwaju ya penalti.
Arsenal waliuanza kichovu mchezo huo na kujikuta wanafungwa mabao mawili ndani ya dakika nane, Chester akianza kufunga la kwanza dakika ya nne na Davies akafunga la pili dakika ya nane.
article-2630209-1DF2D11300000578-658_964x520
Santi Cazorla aliifungia Arsenal bao la kwanza dakika ya 17 kwa shuti la mpira wa adhabu kabla ya Koscielny kufunga la pili dakika ya 72 na Ramsey la ushindi dakika ya 108.
Ushindi huo ni furaha kwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye hajatawaa taji lolote kwa miaka tisa.
Mara ya mwisho Arsenal walitwaa taji mwaka 2005, ambalo lilikuwa Kombe hilo hilo la FA wakiendeleza mafanikio ya msimu wa 2003-2004 walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu na Ngao ya Jamii.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Fabianski, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Arteta, Ramsey, Cazorla/Wilshere dk105, Ozil/Rosicky dk105, Podolski/Sanogo dk61 na Giroud.
Hull: McGregor, Chester, Bruce/McShane dk67, Davies, Elmohamady, Livermore, Huddlestone, Meyler, Rosenior/Boyd dk103, Quinn/Aluko dk74 na Fryatt.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

ATLETICO MABINGWA WA LA LIGA

atletico_187be.jpg
Atletico Madrid imenyakua kombe la ligi kuu ya Hispania La liga baada ya kutoka sare ya 1 – 1 dhidi ya Barcelona na hivyo kumaliza ligi ikiwa na pointi 90 huku Barcelona ikishika nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 87.
Real Madrid iliyoshinda mechi yake dhidi ya Espanyol kwa 3 - 1 ikishika nafasi ya tatu kwa kumaliza ligi ikiwa na pointi 87 lakini ikizidiwa na Barcelona kwa tofauti ya goli moja.
Barcelona wana tofauti ya magoli 67 wakati Real Madrid ikiwa na tofauti ya magoli 66.
Katika mechi hiyo ya Barcelona dhidi Atletico Madrid ambayo ilikuwa ni ya kuamua ni timu ipi itanyakua ubigwa wa La Liga msimu huu, Barcelona ndio waliokuwa wa kwanza kuutikisa wavu wa Atletico Madrid kwa goli lililofungwa na Alexis Sanchez katika ya 34 kipindi cha kwanza.
Baadae Atletico Madrid walikuja juu na kuanza kulishambulia goli la Barcelona ambapo Diego Godin katika dakika ya 49 kipindi cha pili aliIsawazishia timu yake kwa goli safi alilolipachikwa wavuni kwa njia ya kichwa na hivyo kufanya mechi hiyo imalizike kwa jumla ya goli 1 - 1 .
Atletico Madrid inakuwa mabingwa wa La Liga tangu baada ya kulikosa kombe hilo tangu mwaka 1996. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...