Shirika
rasmi la habari nchini Uchina Xhinua limesema kuwa serikali imewaondoa
zaidi ya raia wake 3000 kutoka nchini Vietnam kufuatia ghasia dhidi raia
wa Uchina nchini humo.
Wafanyikazi
wawili wa Uchina wameuawa kufuatia ghasia hizo zilizosababishwa na
hatua ya Uchina kupeleka meli yake ya kuchimba mafuta katika eneo
linalozozaniwa kusini mwa bahari ya Uchina.
Mapema hii leo takriban raia 16 wa Uchina waliojeruhiwa vibaya waliondoshwa nchini humo kupitia usafiri wa ndege maalum.
Serikali
mjini Beijing inaandaa safari nyingine za ndege huku naibu waziri wa
maswala ya kigeni Liu Jianchao akizuru Vietnam kwa mazungunmzo na
mamlaka.
Aidha waziri huyo amewatembelea baadhi ya raia wa Uchina waliojeruhiwa hospitalini.
Wanaharakati
nchini Vietnam wameitisha maandamano zaidi dhidi ya raia wa Uchina hii
leo licha ya mwito wa serikali wa kutaka kusitishwa kwa maandamano hayo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment