Meja Jenerali Godefroid Niyombareh
amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati
maalum ya kuiokoa Burundi
Raia wa Bujumbura wakishanilia tangazo la generali Niyombareh
Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu
wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa
Nkurunziza.
Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi
februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani
mbali na sheria za kimataifa.
Polisi wameamrishwa kuondoka mabarabarani
Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.
Tayari wanajeshi wameshika doria nje ya makao makuu ya runinga ya taifa.
Maafisa wa polisi wamekuwa wakipambana na waandamanaji wanaopinga hatua ya Rais Nkurunzinza kuwania awamu ya tatu