Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila. PICHA|MAKTABA
Mbunge wa Kigoma Kusini
(NCCR-Mageuzi), David Kafulila ameeleza namna alivyoibua sakata la
uchotwaji wa Sh306 bilioni kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow na kudokeza
kuwa kitendo cha baadhi ya watuhumiwa kugoma kujiuzulu, kinaonyesha kuna
watu zaidi wanahusika.
Kafulila (32), ambaye alikuwa akiulizia suala hilo
kila mara bungeni hadi uamuzi wa kulijadili ulipofikiwa, amesema
ataendelea kulifuatilia hadi aone mwisho wake.
Akaunti hiyo ilifunguliwa Benki Kuu ya Tanzania
(BoT) kuhifadhi fedha za malipo ya tozo ya ufuaji umeme baada ya Tanesco
kuingia kwenye mgogoro na Kampuni ya IPTL na suala hilo kupelekwa
mahakamani.
Kwa mujibu wa masharti ya uendeshaji wa akaunti za
escrow, fedha hizo zilitakiwa zitolewe baada ya Mahakama kutoa uamuzi
wa mgogoro huo, lakini wakati ilitaka pande hizo mbili zikutane na
kukokotoa viwango vya tozo hizo, fedha hizo zilitolewa na kulipwa kwa
mmiliki mpya wa Kampuni ya Pan African Power Solutions (PAP), jambo
lililosababisha kuibuka kwa kashfa hiyo. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz