Sunday, May 19, 2013
SIMBA NA YANGA ZAINGIZA MILIONI 500
Na Boniface Wambura,
IMEWEKWA MEI 19, 2013 SAA 6:20 MCHANA
MECHI ya watani wa jadi Simba na Yanga la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, iliyochezwa jana (Mei 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa mabingwa wapya Yanga kushinda mabao 2-0 imeingiza sh. 500,390,000.
Mechi hiyo namba 180 ambayo ilikuwa kati ya saba la kuhitimisha ligi hiyo msimu wa 2012/2013 ilishuhudiwa na watazamaji 57,406 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Kila klabu imepata mgawo wa sh. 123,970,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,330,677.97.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 19,039 na kuingiza sh. 95,195,000 wakati kile cha sh. 7,000 kiliingiza watazamaji 17,647 na kupatikana sh. 123,515,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 63,036,064.81, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 37,821,638.88, Kamati ya Ligi sh. 37,821,638.88, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,910,819.44 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 14,708,415.12.
"WANAOCHOCHEA VURUGU ZA KIDINI NI WATU WALIOTUMWA NA MATAIFA YA NJE"..... RAIS KIKWETE
Rais Jakaya Kikwete amebainisha kuwa vurugu za kidini na kisiasa zinazotokea nchini, zina uhusiano na watu wa nchi za nje.
Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi kwenye ibada hiyo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu.
“Wanaohamasisha vurugu hizo ni watu wenye uhusiano ya karibu na watu wa nje ambao mambo yakiharibika nchini watakuwa wa kwanza kupanda ndege, ilhali wakiendelea kutoa matamko ya uchochezi wakiwa nje ya nchi wakati wengine wakiendelea kuumia,” alisema Kikwete.
Ibada hiyo ilifanyika chini ya ulinzi wa polisi na askari wa usalama, na ilihudhuriwa na Askofu Mkuu wa Anglikana duniani, Justin Welby.
Rais Kikwete alisema amekuwa akichukizwa na vurugu za kidini zinazofanywa na baadhi ya watu wasioitakia mema Tanzania, huku wakijua kuwa amani ikitoweka ni gharama kubwa kuipata.
JACQUILINE WOLPER ATAJWA KWENYE LIST YA WASANII AMBAO NI FREEMASONS...!!
Inawezekana kila kitu kina wakati wake, kuna muda watu walikuwa wakisikia neno ‘Freemason’ ama ‘Illuminate’ kama inavyojulikana nchini Kenya wengi walikuwa wanaiona ni habari kubwa, lakini kwa sasa hivi inaweza kuchukuliwa kama sio big deal.
Sababu ni ile ile kuwa wengi wanaoendelea kwa haraka ama kuwa juu katika kile wanachokifanya basi utasikia huyo ni member wa Freemason, kwa upande wa Marekani wanasema ‘he/she just sold her/his soul to the devil’. Japo kwa upande wa Marekani wapo wanaokiri kufanya hivyo kweli, ila kwa Africa Mashariki hakuna msanii aliyewahi kukiri.
Lakini yote hayo ni kama yanakanganya na kuonekana kama hayana mantiki hasa pale ambapo vithibitisho vya kinachoongelewa huwa havileti mantiki ya moja kwa moja. Pengine watu wanatafuta pesa kwa bidii na kumuomba Mungu lakini kwa kuwa kwenye mstari wa juu wanajikuta wanahisiwa kuwa member wa secret society (Freemason). Oh..au labda ndo vile kwa upande mwingine lisemalo lipo na kama halipo laja !
Tunathubutu kuziita blaa blaa kwa upande mwingine, lakini tukiweka kwenye mabano kuwa inaweza kuwa na ukweli, who knows!
Mtandao wa malimwengu wa nchini Kenya huenda ukawa na mfano mzuri wa kile nilichokitaja hapo juu, mtandao huo kupitia mwandishi wake imetaja majina ya wasanii wa Tanzania na Kenya wanaosemekana kuwa ni wafuasi wa Freemason, lakini kizuri zaidi ni kwamba mtandao huo umejaribu kuonesha vithibitisho na kushindwa kupata jibu la moja kwa moja kwa nini wasanii hawa wamekumbwa na hili. Inabaki hivyo hivyo kuwa tetesi tu.
Hawa ni wasanii waliotajwa na maelezo yanayowahusu:
TANZANIA:
1.Naseeb Abdul Jumaa (Diamond Platinum)
Picha aliyopiga mwaka jana akiwa na mzungu anaeaminika kuwa ni moja kati ya viongozi wa Freemason wakiwa wameweka pozi na kuonesha ishara inayooaminika kuwa ni ya Freemason, na kwamba alipoulizwa yeye alisema hakufahamu kama alikuwa anaelekezwa kupiga picha kwa pozi la ki-freemason. Kwa mujibu wa mwandishi anaona inaweza kuwa kweli kwa sababu anaonekana kuenjoy!
HAYA NDIO MAJIBU YA HALIMA MDEE KUHUSU STORY ZA YEYE AKUJIHUSISHA NA MAPENZI YA JINSIA MOJA
Kupitia season mpya ya Clouds Fm, ndani ya so so fresh na fetty, Mh Halima Mdee jana amefunguka juu ya swali aliloulizwa kuhusu story zilizosambaa kuwa anashiriki mapenzi ya jinsia moja.
aah unajua huwezi kuzuia watu kusema, na mimi huwa sihangaiki na watu wanasema nini, lakini ukitaka kumjua Halima unaweza ukamchunguza kirahisi sana, kwa kumuangalia alipotoka, historia yake na mahusiano yake, ambayo mengine ni wazi sana watu walikuwa wanayajua,
watu wanapenda ku speculate pale ambapo wanaona kitu ambacho hawati kuona, sasa hilo swala lilishaandikwa sana, nadhani walioandika baadae wakaja kuomba radhi kwasababu waligundua wameandika kitu kisicho sahihi, probably kutokana na sauti yangu you know, probably kutokana na tembea yangu, kwasababu mimi nimekulia kwenye familia ya wanaume watupu umeona eeh, mimi nimekuwa ni mpambanaji tokea utotoni, kwasababu nimezungukwa na jeshi la kibabe, thats who iam, lakini mtu anaetaka kumjua Halima na ana uhuru tu, hata akitaka niwatajie list ya watu wangu i can do that, lakini sidhani kama is their damn business, cause ma life is personal, na wakitaka kuchunguza wachunguze kwa mpango wao na watapata taarifa, kwa uhuru tu, na wanaweza wakatoa tangazo kwamba jamani watu waliowahi kuwa na uhusiano na huyu if any wajitokeze, watajitokeza kama wapo upande huo, watajitokeza kwasababu sasa hivi si dunia huru bana
Ufaransa yakubali ndoa ya jinsia moja
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, ametia saini sheria yenye utatanishi, inayohalalisha ndoa kati ya watu wa jinsia moja.
Ufaransa sasa imekuwa nchi ya 14 duniani kuruhusu ndoa kama hizo.
Makundi ya watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja nchini Ufaransa yamefurahi kuwa hatimaye sheria hiyo imepitishwa.
Wanasema kuna marafiki kadha wanaosubiri kufunga ndoa na maelfu ya watoto wanaolelewa na watu wa jinsia moja
ambao sasa watapata hifadhi kisheria.
Wanaopinga sheria hiyo wamehamaki.
Wanaona kuwa Rais Hollande ameshughulika mno na ndoa kati ya jinsia moja kwa sababu ameshindwa katika maswala muhimu zaidi - kama swala la uchumi wa nchi.
Maandamano mengine ya kupinga ndoa kati ya jinsia moja yanapangwa kufanywa tarehe 26 May.
Yanaweza kuwa makubwa na ya fujo kama yaliyopita.
Sababu ni upinzani dhidi ya ndoa za jinsia moja umechanganyika na malalamiko mengine ya mrengo wa kulia dhidi ya serikali.
Na hali nchini sasa ni tete.
Lakini kwa kweli vita vimemalizika.
Watu wa jinsia moja sasa wataanza kufunga ndoa nchini Ufaransa.
Baadhi ya wanasiasa wa mrengo wa kulia wataahidi kuwa watabatilisha sheria hiyo wakipata madaraka, lakini historia inaonesha kuwa kufuta mabadiliko kama haya katika jamii ni shida sana.
Subscribe to:
Posts (Atom)