Wednesday, March 21, 2018
MAMBO 18 YA KUFANYA WAKATI WA MVUA ILI KUHAKIKISHA USALAMA WAKO
Mvua kubwa imekuwa ikinyesha maeneo mengi Afrika Mashariki na kusababisha uharibifu wa mali na vifo. Huko nchini Kenya, watu zaidi ya 10 wamefariki baada ya kusombwa na maji ya mafuriko. Wakati hapa nchini Tanzania mvua hizo zimeleta maafa mbalimbali ikiwa ni pamoja na watu kukosa makazi n.k.
Wataalam wa masuala ya uoakoaji wametoa ushauri ambao unaweza kukufaa sana wakati huu wa mvua.
- Fahamu kwamba wakati wa kiangazi, vumbi, mchanga na taka za aina mbalimbali hurundikana barabarani. Mvua inaponyesha, husababisha barabara kuwa telezi na kwa hivyo ukiwa na gari ni muhimu kutoendesha gari lako kwa mwendo wa kasi kupindukia kwani gari likiteleza utashindwa kulidhibiti gari lako kwa urahisi. Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz
MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA KIGOGO WA SHIRIKA LEO MARCH 21
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (National Housing Corporation – NHC) Bi. Blandina Nyoni.
Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu asubuhi ya leo March 21, 2018 inaeleza kuwa Rais Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (National Housing Corporation – NHC) Bi. Blandina Nyoni kuanzia leo.
Pia taarifa hiyo inaeleza kuwa Rais Magufuli ameivunja Bodi ya shirika hilo la NHC. Uteuzi wa Mwenyekiti mpya na bodi nyingine utafanyika hapo baadaye. Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz
HII NDIO TUZO NYINGINE ALIYOSHINDA CRISTIANO RONALDO
Mshambuliaji Real Madrid Cristiano Ronaldo
Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mwanasoka bora ya mwaka 2017 nchini Ureno.
Ronaldo
alitangazwa kupitia hafla iliyofanyika mjini Lisbon, baada ya
kuwashinda wachezaji Bernardo Silva wa Manchester City na kipa wa
klabu ya Sporting Lisbon Rui Patricio.
Ameshinda tuzo hiyo baada ya kuisaidia Real kushinda mataji yote ya
La Liga na ligi ya mabingwa Ulaya kwa mara ya pili mfululizo mwaka huu
2017.
Naye Kocha wa klabu ya Monaco Leonardo Jardim ameshinda
tuzo ya kocha bora, baada ya kuiongoza timu hiyo ya Ufaransa kushinda
taji la Ligue 1 na kufika hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa
Ulaya, wakati kocha wa Manchester United, Jose Mourinho akishinda tuzo
ya Vasco da Gama kwa kuitangaza vyema soka ya Ureno kimataifa.
TETESI ZA SOKA LEO JUMATANO 21 MARCHI
Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah
Ajenti wa mshambuliaji wa Manchester
United Anthony Martial, 22, hajatoa hakikisho lolote kuhusu uwezekano
wa mchezaji huyo kusalia katika klabu hiyo. Tottenham imejiandaa kumpoteza beki wa ubelgiji Toby
Alderweireld, 29, mwisho wa msimu huu lakini watahitaji kulipwa dau la
Yuro 50m (£44m).
Liverpool imesema kuwa haitamuuza mshambuliaji wake Mohamed Salah,
25, mwisho wa msimu huu na kwamba mchezaji huyo wa Misri hana kandarasi
itakayomruhusu kuondoka katika klabu hiyo wakati wowote. Liverpool
bado haijwasiliana na kipa wa Roma Alisson, 25, lakini raia huyo wa
Brazil hayuko tayari kutia saini kandarasi mpya katika klabu hiyo ya
Itali.
Kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante, 26, amepinga
uvumi kwamba anatakakujiunga na PSG kwa kusema kwamba anahisi kuwa
nyumbani Stamford Bridge. Mchezaji anayelengwa na klabu
ya Manchester United Milan Skriniar, 23, anasema kuwa anafurahia
kusalia Inter Milan. Ria huyo wa Slovakia pia ameivutia Barcelona. The
Slovakian also interests Barcelona.
Subscribe to:
Posts (Atom)