Baraza la
Mitihani la Taifa (Necta), limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la
saba mwaka 2014 yakionyesha kuwa zaidi ya nusu ya wanafunzi waliofanya
mtihani huo Septemba mwaka huu, wamefaulu.
Matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Katibu
Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde yanaonyesha kuwa wasichana
wamefanya vizuri zaidi ya wavulana, huku ufaulu kwa jumla ukiwa
umeongezeka kwa asilimia 6.38 ikilinganishwa na mwaka 2013.
Katika matokeo hayo Shule ya Twibhoki iliyopo
mkoani Mara iliibuka ya kwanza kitaifa kati ya shule 15,867 zilizofanya
mtihani huo ikifuatiwa na Mugini, Peacland na Alliance zote za mkoani
Mwanza.
Shule ya tano ni Kwema ya Shinyanga ikifuatiwa na
St Severine ya Kagera, Rocken Hill ya Shinyanga, Tusiime ya Dar es
Salaam, Imani ya Kilimanjaro na iliyoshika nafasi ya 10 ni Palikas ya
Shinyanga.
Wakuu wa shule vinara wazungumza
Mkuu wa Shule Twibhoki iliyopo Mugumu - Serengeti,
Alphonce Magori alisema siri ya mafanikio hayo ni kila mwalimu kutambua
nafasi yake. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz