Rita
Paulsen aka Madam Rita wa Bongo Star Search na Walter Chilambo tayari
wameshazijibu Salamu za Nay wa Mitego na jana ilikuwa zamu ya Mbunge wa
Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe Kwake
mbunge huyo, Nay ni msanii wa pili wa Hip Hop anayemkubali zaidi
Tanzania baada ya Roma na kwamba anakiheshimu kile alichokisema kwenye
wimbo huo kwakuwa ni kazi ya sanaa. Tazama tweets hizi.
CarolNdosi @CarolNdosi I wonder if @zittokabwe ever listens to hip hop..local or international..
Na Daniel Mbega UHALIFU nchini Tanzania umekuwepo kwa
miaka mingi, lakini katika miaka ya karibuni umeonekana kushika kasi
kuliko ilivyowahi kutokea, kiasi cha kutishia amani kwa Watanzania
kuhusu usalama wa maisha na mali zao. Kati ya Januari 2005 hadi Januari 2006
kulikuwepo na matukio ya uhalifu na ujambazi wa kutumia silaha ambapo
kiasi cha Shs. 16,782,172,419 kiliporwa katika benki kadhaa za maduka ya
kubadilishia fedha nchini. Takwimu zinaeleza kwamba jumla ya
wahalifu 46, wakiwemo raia 12 wa Kenya, walikamatwa katika kipindi hicho
wakihusishwa na matukio mbalimbali ya uhalifu.
Baada ya hapo ikafuatia kasheshe kubwa
ndani ya Jeshi la Polisi, sekeseke ambalo lilifanya iibuliwe orodha ya
maofisa 20 wa jeshi hilo ambao wanashirikiana na majambazi katika wizi
huo.
Lakini wakati huo zilikuja taarifa
mfululizo zikiwatuhumu askari kadhaa ndani ya jeshi hilo ambao wanadaiwa
kujihusisha na vitendo vya uhalifu, huku wakiwa wamechuma mali nyingi
ambazo haijulikani namna walivyozipata kulinganisha na mishahara yao.
Kama nilivyotangulia kusema, vitendo
vya uhalifu hapa nchini vimekuwepo kwa miaka mingi, na kwa kumbukumbu
zangu vitendo hivi vilianza kushika kasi mwanzoni mwa miaka ya 1980.
SERIKALI
imeitaka kampuni ya New Habari 2006, kuacha kuchapisha gazeti la Rai
kila siku na kampuni ya Mwananchi kuacha kuchapisha gazeti la Mwananchi
kwenye mtandao.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Malelezo,
Assah Mwamebene, alitoa onyo hilo ofisini kwake jana na kuongeza kuwa
ameziandikia barua kampuni hizo, zijieleze ni kwanini zinafanya hivyo.
“Tumeona gazeti la Mwananchi baada ya
kufungiwa, limeendelea kuchapishwa kwenye mtandano wa intaneti kinyume
na amri iliyotolewa. Vivyo hivyo kwa Rai ambayo ilikuwa ikichapishwa
mara moja kwa wiki, imeanza kutoka kila siku, tunawataka warejee ratiba
yao,” alisema.
Alisema endapo vyombo hivyo
havitatekeleza agizo hilo na kujieleza katika ofisi yao ifikapo kesho,
Serikali italazimika kuchukua hatua kali zaidi ikiwa ni pamoja na
kuongeza adhabu, ikiwemo kufungia kwa muda usiojulikana na kufutiwa
usajili wake.
“Umma ufahamu kuwa Serikali
haikukurupuka kufungia magazeti hayo, uamuzi ulifanywa baada ya kufuata
taratibu zote za msingi ikiwemo kuwasikiliza wahusika.
Tunasikitika kuwaarifu kuwa kutokana na sababu zisizozuilika, tutashindwa kuendelea kuwaletea habari mpya kupitia tovuti yetu (www.mwananchi.co.tz) na mitandao ya kijamii ya Mwananchi kwa wakati wote ambapo uzalishaji wa gazeti la Mwananchi utakuwa umesitishwa.
Tunasikitika kwa usumbufu wowote utakaosababishwa na hali hii na tunatumaini mtaendelea kuwa nasi wakati wa kipindi
hiki kigumu cha mpito. Tunatarajia kurejea rasmi hewani na habari moto moto wiki ijayo, Ijumaa, tarehe 11 October.
Tunawakaribisha
muendelee kusoma habari zetu za zamani (archives) kwenye tovuti ya
Mwananchi na kurasa zetu za Facebook na Twitter ili mzidi kuhabarika.
Pia tunawakaribisha mtembelee tovuti zetu za www.thecitizen.co.tz na www.mwanaspoti.co.tz ambazo
zitaendelea kufanya kazi kwa ufanisi, zikiwaletea habari za uhakika na
kuaminika kipindi hiki ambapo Mwananchi imefungiwa.
C.E.O wa kampuni ya Endless Fame Film maarufu kma Wema Sepetu ameonekana kuchukizwa na kitendo cha kuchafuliwa kwa jina lake katika moja ya magazeti ya udaku ya hapa nchini. Mapema
asubuhi
ya leo kupitia account yake ya Instagram mwanadada Wema alitupia picha
ya gazeti hilo lililo mchafulia jina kwa kumuandika kuwa "Wema Kunyongwa China Awaomba Watanzania Wamuombee".Pia
dakika
chache zilizopita kupitia account yake hiyohiyo ya Instagram wema
amefunguka zaidi kwa kitendo hicho cha kuchafuliwa jina na kuandika
hivi ...
Mchina aoteshwa pua nyingine kwenye paji
lake la uso. Mchina huyo ambaye anatumia jina moja tu la Xiaolian,
alipata matibabu ya kuunda pua ambayo itakaa badala ya pua yake halisi
ambayo iliathirika na kuharibika.
Taratibu zilifanyika katika hospitali iliyoko Fuzhou huko Fujian
Mwanaume huyo mwenye miaka 22 aliharibu pua yake kwenye ajali ya gari Agosti 2012 lakini alishindwa kupata matibabu.
Matokeo yake pua yake ikaathirika mpaka wale madaktari wakashindwa kuirekebisha.
Hawakuwa na jinsi nyingine yeyote ila
kumuotesha pua nyingine alafu kuiondoa baadae ili iwekwe pale ambapo pua
halisi iliharibiwa.
Pua
hiyo ilitengenezwa kwa kuweka tissue expander za ngozi kwenye paji la
uso la Xiaolian.Ilikatwa kwenye shepu ya pua na ikawa imehimarishwa na
cartilage iliyotolewa kwenye mbavu zake.Madaktari hao wa oparesheni wamesema kuwa pua hiyo imekua vizuri na oparesheni ya transplant itafanyika hivi karibuni
Ila mh! Kweli hii nose job! Mchina ana
pua nyingine kwenye paji la uso kuireplace pua halisi iliyoharibika
kwenye ajali ya gari....!!
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
ametangaza kuwa majeshi ya Kenya yataendelea kukaa Somalia hadi usalama
utakapoimarishwa katika nchi hiyo iliyokumbwa na vita vya miaka mingi. Rais Kenyatta amesema kuwa nchi yake haitashurutishwa na magaidi walioteka jengo la maduka la Westgate kwa siku 4. Rais Kenyatta alihutubia umati
uliokusanyika kwa maombi ya pamoja ya dini mbali mbali, kwa ajili ya
watu 67 waliouawa katika shambulio la Westgate. Shambulio hilo ndio baya zaidi kuwahi kutokea nchini Kneya tangu majeshi yake yaingie nchini Somalia mwaka wa 2011.
''Hawa wauaji waliokuja kutenda
ukatili wao ulio na woga hapa nchini kwetu, walikuwa wanadai kuwa
wanafanya hivyo kwasababu majeshi ya Kenya yapo nchini Somalia. Nataka
niwaeleze bayana kuwa, majeshi yetu yatakaa huko hadi kuwepo amani
katika nchi hiyo.''
Papa John Paul II na John XXIII
wanatarajiwa kutangazwa watakatifu Aprili 27 mwakani, kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa na mkuu wa sasa wa kanisa Katoliki, Papa Francis. Taarifa ya uamuzi huo imetolewa leo
kwenye mkutano wa makadinali unaoendelea mjini Vatican, ikiwa ni hatua
mihimu ya kuthibitisha tangazo lake la Julai mwaka huu kwamba atawapa
heshima viongozi hao wawili wa juu wa Kanisa waliopita katika karne ya
20.
Katika taarifa iliyonakiliwa kutoka
kwenye gazeti la mtandaoni la Daily Mail, alisema wakuu hao wa Kanisa
Katoliki duniani ambao kwa sasa ni marehemu waliweza kutumia karama zao
kwa uamunifu na kuonyesha matendo makuu.
Wachambuzi wa masuala ya Kanisa hilo
alieleza kwamba inaonekana umuzi huo ni wa makusudi ikiwa ni hatua ya
kujaribu kuliunganisha kanisa hilo ambalo lina mkanganyiko kwa sasa.
Kila mmoja ana watu wanaomuunga mkono
na wanaompinga, ambapo kwa sasa Francis anaonekana kuungwa mkono na wote
wa pande zote mbili hivyo kuwa kichocheo cha kuunganisha na kufuta
makovu yaliyolikumba Kanisa hilo kwa miaka ya hivi karibuni.