Nay akiwa na bastola yake
Sunday, April 28, 2013
GARI JIPYALA MILIONI 35 ALILONUNUA NEY WA MITEGO PAMOJA NA BASTOLA HAPA
Mwaka 2013 ni mzuri kwa rapper Nay wa Mitego.
Licha ya kuwa na hit single hewani, Muziki Gani aliyomshirikisha
Diamond, rapper huyo amenunua ndinga mpya aina ya Mark X yenye thamani
ya shilingi milioni 35. Kama hiyo haitoshi, hitmaker wa Nasema Nao,
amejihami pia kwa kununua bastola.
Nay ameshare picha hizo kwenye Instagram na Facebook ambapo miongini mwa
picha za gari lake ameandika, ‘My new car. Mark X, Zic z wat I nid.”
Mwaka huu Nay ametumiwa kwenye show nyingi za Airtel na Vodacom ambazo
huenda zimemwingizia mkwanja wa kutosha.
MBUNGE LEMA AZUILIWA KUPIGA MSWAKI WALA KUNYWA CHAI AKIWA MAHABUSU...... !!
Lema ambaye bado anaendelea kusota rumande siku ya tatu baada ya kunyimwa dhamana, ameanza kufanyiwa vituko na Jeshi la Polisi baada ya jana asubuhi mkewe kuzuiliwa asimpe mswaki wala chai.
Mbunge huyo alikamatwa kutokana na amri ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, aliyedai kuwa aliwachochea wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha kumzomea kiongozi huyo na kupopoa gari lake kwa mawe.
Hata hivyo, siku moja kabla ya kukamatwa Lema aliwaonesha waandishi wa habari ujumbe mfupi wa simu ya kiganjani aliyotumiwa na Mulongo akimtishia kuwa atamfungulia kesi yoyote anayoitaka.
“Umeruka kihunzi cha kwanza, nitakuonesha kuwa mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi,’’ ulisomeka ujumbe huo uliotumwa kupitia simu namba 0752 960276 ambayo Lema alidai ni ya Mulungo.
MSANII SIZE NANE ALILIA BIKRA YAKE HADHARANI...!!
Mwanamuziki aliyeitikisa vilivyo Kenya kabla ya kuokoka na
kuachana na muziki wa kidunia, mwanadada Size 8 sasa ameanza
kufunguka katika interview kwenye vituo mbali mbali vya redio na Tv kuhusiana na maisha mapya ya kidini.
Kati ya mambo yote ambayo Size 8
amekuwa akiyaongelea, ni moja tu ambalo amekuwa akilitilia mkazo kwa
kumaanisha kuwa linamsikitisha zaidi .....Jambo hilo ni lile la kupoteza
BIKRA YAKE.....
Size 8 ameziambia media kuwa "Najutia
sana kupoteza bikra yangu. Ninaamini kuwa kijana anatakiwa kujilinda
na kujizuia kufanya ngono katika ujana wake wote mpaka atakapo pata
kibali toka kwa Mungu."
KIONGOZI WA KANISA AZIKWA AKIWA HAI
Msaidizi
wa zamani wa Padri (Katekisita) katika Kigango cha Kanisa Katoliki
Kijiji cha Mkwajuni, Florian Mwamosi (70) amekufa baada ya kuzikwa akiwa
hai katika kaburi moja na mtu anayedaiwa kumuua kwa njia ya
kishirikina.
Tukio hilo limetokea katika Kitongoji
cha Maweni kijijini hapo wilayani Chunya mkoani Mbeya.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani alikiri kutokea kwa tukio hilo
akieleza kuwa lilitokea saa 9:00 mchana katika kijiji hicho cha Maweni
Mkwajuni wilayani Chunya.
"Marehemu
aliuawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa na mawe kwa tuhuma za
kuhusika na uchawi na kusababisha kifo cha Peter Robert," alisema.
Kamanda Athumani alisema kuwa
uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea na kwamba wahusika wote wa
tukio hilo wamekimbia na kuzihama nyumba zao, hivyo polisi wanaendelea
na msako wa kuwatia mbaroni watuhumiwa na kwamba tayari kaburi hilo
limefukuliwa jana kutenganisha maiti hizo.
BEYONCE AWAPIGA MKWARA WAPIGA PICHA, HIKI NDO ALICHOKISEMA
Baada
ya kukerwa na picha alizopigwa wakati wa tamasha la SuperBowl ambazo
anaona zilimdhalilisha, mwanamuziki Beyonce amefikia maamuzi magumu ya
kuwakataa wapiga picha
Kwa
mujibu wa barua pepe iliyotumwa kwenye ukurasa wa facebook wa Umoja wa
Wapiga picha za Muziki imeeleza kuwa mwanamuziki huyo haitaji tena
wapiga picha katika shoo za ziara yake ya sasa ya Ulaya
Badala
yake amekuwa akitoa picha rasmi zilizopigwa kutoka katika shoo na
wapiga picha maalum aliowakodisha.
Mawaziri, wabunge CCM warushiana 'makombora'
Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM), jana walishambuliana huku waliokuwa mstari wa mbele kuikosoa serikali katika vikao vya bajeti vinavyoendelea mjini Dodoma wakituhumiwa kukiua chama na kukipa nguvu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Kikao hicho ambacho kilikuwa chini ya Mwenyekiti wake, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kilifanyika katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa mjini Dodoma.
Pinda alianza kwa kuweka hoja mezani akitaka wabunge wa CCM kuchangia Sh.100,000 kila mmoja kwa ajili ya kuwezesha ushindi katika uchaguzi mdogo wa madiwani unaotarajiwa kufanyika katika kata 26 nchini.
Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge hao, lakini alisimama Mbunge wa Mwibara, Alphaxard Khangi Lugola, akihoji kulikoni wanaosaidiwa na chama wakawa madiwani ili hali wabunge walio na kesi mahakamani wakiachwa kugharamia kila kitu wenyewe.
“Si unajua nyoka wa shaba (Lugola), ana kesi mahakamani, sasa ndiyo maana akaamua kuhoji, iweje yeye hasaidiwi na chama wakati huo huo anaambiwa akisaidie chama,” alisema mmoja wa wabunge aliyekuwa ndani ya kikao hicho.
Subscribe to:
Posts (Atom)