Tuesday, January 24, 2017

MAALIM SEIF "NIMESHAMALIZANA NA JECHA"

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad 
  
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamada mesema ameshamalizana na mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha na haoni umuhimu wa kuzungumzia wala kumjibu, kwa sababu atampa sifa asizostahili.

Akihojiwa katika kipindi cha Funguka cha kituo cha televisheni cha Azam TV juzi, Jecha alisema hakumshirikisha Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein katika kufuta matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2015 visiwani humo.

Jecha alifuta matokeo hayo Oktoba 28, 2015, siku ambayo alitakiwa atangaze mshindi wa uchaguzi wa rais, huku ZEC ikiwa imeshatangaza matokeo ya majimbo 31 na mengine tisa yaliyosalia yakiwa yameshahakikiwa.

Alitangaza uchaguzi mpya Machi 20, 2016 ambao ulisusiwa na CUF na Dk Shein kuibuka mshindi.

DC AMSWEKA NDANI DIWANI WA CHADEMA

 
Mkuu wa Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, Joseph Chilongani amemweka rumande Diwani wa Bukundi, Joseph Masibuka (CHADEMA ) kwa tuhuma za kubomoa nyumba 20 za wananchi kwa madai ya kujengwa katika eneo lake.

Hata hivyo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Jonathan Shanna alisema jana kuwa wanachunguza madai hayo kubaini kama kuna kosa ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Shanna aliwapongeza wananchi kutojichukulia sheria mkononi wakati wa ubomoaji wa nyumba hizo wilayani hapa.

Kubomolewa kwa nyumba hizo na kampuni ya udalali, kumesababisha zaidi ya kaya 100 kukosa makazi.

Hata hivyo, Chilangoni aliwataka wananchi kurejea kwenye makazi yao na kwamba gharama za ujenzi zitafanywa na diwani huyo.

Baadhi ya wakazi hao walisema nyumba za nyasi na magodoro yalichomwa moto wakati wa ubomoaji.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...