Siku Moja baada ya kujiuzuri kwa Mwanasheria
mkuu Jaji Fredrick Werema, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kwa mara nyingine amejitokeza hadharani
na kutoa msimamo wake kwamba hana sababu ya kujiuzuru kwenye nafasi yake
kwa kuwa hakuhusika kwa namna yeyote kwenye sakata la uchotwaji wa
mabilioni kwenye akaunti ya Escrow.
Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi jijini
Dar es Salaam, Profesa Tibaijuka amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa
shinikizo la kutaka kujiuzuru, yeye binafsi ameona hana sababu ya
kufanya hivyo kwani kufanya hivyo ni kukubali kuwa amehusika moja kwa
moja kwenye kashfa hiyo jambo ambalo si la kweli.
Profesa Tibaijuka amekwenda mbali zaidi na kusema
kuwa uvumi unaoendelea kusambazwa mitaani ni ishara mbaya kwani
unawaaminisha wananchi kuwa amehusika katika sakata hilo wakati yeye
hajahusika na jambo lolote.
“Huu uvumi unatakiwa kuachwa, sioni sababu yeyote
ya mimi kujiuzuru kwa kuwa sijahusika kwa namna yeyote kwenye sakata
hili la Escrow” anasema Profesa Anna Tibaijuka. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.