Pichani chini baadhi ya Wafanyakazi
wenzake na Ufo Saro kutoka IPP pamoja waandishi wa habari wa vyombo
mbalimbali wakiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako Ufo Saro
ambaye mpaka sasa, yuko katika chumba cha upasuaji baada ya kupigwa
risasi na mchumba wake Anteri Mushi usiku wa kuamkia leo ambapo pia
alimpiga mama mzazi wa Ufo Saro Anastazia Peter Saro miaka 59
aliyefariki hapohapo na baadae kujipiga risasi mwenyewe na kufa
hapohapo, Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo huko Mbezi Luisi Wafanyakazi hao wakibadilishana mawazo hapa na pale katika hospitali ya Muhimbili leo hii Picha Kwa Hisani ya Fullshangwe Blog
Makalla
alitoa ufafanuzi huo muda mfupi baada ya Idara ya Habari-Maelezo kutoa
taarifa kwamba Serikali imesikitishwa na Gazeti la Mwananchi na gazeti
dada la Rai, Mtanzania kukiuka masharti ya adhabu walizopewa.
Septemba 27, mwaka huu Serikali iliyafungia Mwananchi kwa siku 14 na Mtanzania siku 90.
Wakati
likianza kutumikia adhabu yake, Mwananchi ambalo tayari limemaliza
kuitumikia, liliendelea kutoa taarifa kwenye tovuti yake wakati Kampuni
ya New Habari (2006) Ltd ambayo inamiliki Mtanzania ilianza kuchapisha
kila siku gazeti la Rai ambalo awali lilikuwa likichapishwa kila wiki.
Katika ufafanuzi wake alioutoa
jana
Makalla alisema: "Nimelazimika kueleza haya baada ya taarifa mpya ya
Idara ya Habari-Maelezo iliyohoji uhalali wa gazeti la Mwananchi kuwa
online (mtandaoni) na gazeti la Rai kutoka kila siku, badala ya mara
moja kwa wiki (Alhamisi)."