INAWEZEKANA umekuwa ukisikia vitu vingi kuhusu lejendari wa
Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ lakini hukupata chansi ya kumsikia
mwenyewe akifunguka mwanzo mwisho juu ya kisanga kilichompata
alipojikuta kwenye janga la matumizi ya dawa za kulevya.
Ijumaa Wikienda limefanya naye mahojiano (exclusive interview) ambapo amekidhi kiu yako ya kujua chochote kinachomhusu. UNGANA NAYE…
KWA MTU ASIYEKUJUA, UMETOKEA WAPI?
“Nimezaliwa Mei 15, 1982 mkoani Iringa. Kabla ya kuingia kwenye muziki nilifanya kazi ya utangazaji. Watu wengi walinijua wakati nikiwa Radio Clouds FM. Albamu yangu ya kwanza ni Mapenzi Yangu niliyoitoa mwaka 2003. Kilichofuata ni kujipatia mashabiki wengi sana ndani na nje ya nchi. Baadaye niliachia Albamu ya pili ya Na Wewe Milele ya mwaka 2004.
Nilipata mialiko mingi nje ya nchi zote Afrika Mashariki, China, Uingereza na kwingineko. Kilichofuata ni singo kibao na tuzo hadi nilipopata matatizo mwaka jana. Unazikumbuka Mama Ntilie, Mahaba ya Dhati, Touch Me, Na Wewe Milele, Wanifuatia Nini na Nihurumie? Huyo ndiye Ray C mwenyewe.