Dar es Salaam. Serikali imeokoa zaidi ya Sh40 bilioni tangu ilipoanza kutumia mfumo mpya wa malipo kwa watumishi wake.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema
hayo jana, wakati akitoa ufafanuzi juu ya kuchelewa kwa malipo ya
wafanyakazi wa baadhi ya taasisi za Serikali kwa mwezi uliopita.
“Niliagiza kuanza kwa mfumo mpya wa malipo kwa
watumishi wote wa Serikali kuanzia mwaka huu wa fedha ili kubaini malipo
hewa yaliyokuwa yakifanywa na wahasibu wasio waadilifu. Tangu mfumo huo
uanze Julai, tayari tumeokoa zaidi ya Sh40 bilioni,” alisema Nchemba.
Serikali ilitangaza kuondokana na mfumo wa ‘malipo
ya dirishani’ ambao ulikuwa unatoa fursa ya wizi wa fedha za umma
kupitia mishahara iliyokuwa ikilipwa kwa wafanyakazi hewa wengi.
“Kuna mishahara mingi ilikuwa inalipwa kwa
marehemu au wafanyakazi wasiokuwepo ambayo ilikuwa inawaneemesha baadhi
ya watendaji wa idara. Tumeanza kwa kuziba mwanya huo ili kudhibiti
upotevu wa fedha,” alisema naibu waziri huyo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz