Tuesday, June 18, 2013

SIRI NZITO YA KIFO CHA MWANAMUZIKI LANGA

Na Mwandishi Wetu
MWILI wa mwanamuziki Langa Kileo jana (Jumatatu) ulipumzishwa kwenye nyumba ya milele katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar lakini nyuma ya kifo chake kuna siri ambayo rafiki yake wa karibu (jina linahifadhiwa) mkazi wa Mikocheni A jijini Dar ameamua kuiweka hadharani.
Akizungumza na Uwazi juzi, rafiki huyo wa marehemu alisema, siku chache kabla ya kifo chake alimfuata na kumwambia kuwa Israel mtoa roho anamtembelea usiku na anahisi siku si nyingi atamfuata mshikaji wake aliyetangulia mbele ya haki, Albert Mangweha ‘Ngwea’.
“Hii ni siri ambayo hata ndugu zake hawaijui lakini mshikaji alijua anakufa. Alijitahidi kukikwepa kifo lakini alishindwa. Siku chache kabla hajafa, usiku alikuja kwangu na kuniambia kule kwao kwenye geto lake analoishi ambalo liko ghorofani, anaona mauzauza na anahisi kifo kinamuita.
“Nilishangazwa sana na maneno yale. Akazidi kuniambia eti kwa jinsi mambo yanavyokwenda hawezi kuendelea kulala kwao na kuanzia siku ile angelala na mshikaji wetu mwingine pale Geza, Mikocheni A.
“Kweli siku hiyo alilala pale akiwa na hofu kubwa na asubuhi baadhi ya watu wakawa wanamshangaa akiwa ‘amezima’ nje ya lile geto la mshikaji wake. Alivyoondoka sikumuona tena mpaka nilipokuja kuambiwa yuko hoi kwa malaria na kesho yake nikasikia hatunaye, nimeumia sana,” alisema mtoa habari huyo.
Alipoulizwa juu ya uhusiano wa kifo cha Langa na matumizi ya madawa ya kulevya, rafiki huyo alisema: “Inaweza ikawa ngumu kwa ndugu wa marehemu kuhusisha kifo chake na madawa ya kulevya lakini mimi namjua Langa nje ndani, ukweli ni kwamba jamaa alikuwa akiendelea kula ‘mambo’.
“Alikuwa anakuja maskani tunakula mambo yetu na hata wakati anafanya kazi kwenye ile Kampuni ya Barrick hapa Dar, ilikuwa kabla hajaenda anapita kwanza huku uswahilini kisha ndiyo anaenda. Kwa maana hiyo malaria ndiyo iliyomuua lakini hata madawa yamechangia.” 
Langa alifariki dunia Juni 13, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Amini!
SORCE: Globalpublishers

JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WABUNGE 4 WA CHADEMA KWA KUSABABISHA VURUGU ARUSHA


Jeshi la polisi mkoani Arusha linawashikilia viongozi wanne wa CHADEMA na watu wengine huku likiendelea kuwatafuta wabunge wawili na watu wengine.

Jeshi la Polisi limesema limewatua nguvuni watu hao kwa makosa ya kuhutubia mkutano haramu wakati wa kuwaaga marehemu waliopoteza maisha kwenye mlipuko wa bomu uliotokea katika eneo la Soweto jijini humo mwishoni mwa wiki. Makosa mengine ni wanayotuhumiwa kwayo ni kufunga barabara na kuwashambulia askari polisi.



Amesema wataendelea kubaki korokoroni hadi uchunguzi utakapokamilika.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas amewataja Wabunge wanaoshikiliwa ni pamoja na Tundu Lissu na Mustapha Akunai.

Wanaotafutwa ni pamoja na Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambao waliponyoka mikono ya polisi.

ANGALIA PICHA ZAIDI ZA TUKIO LA MABOMU ARUSHA





MBOWE ADAI ANA USHAHIDI WA ALIYERUSHA BOMU, ARUSHA



MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amefichua siri kuhusu tukio la mlipuko wa bomu lililotokea jusi katika viwanja vya Soweto, jijini Arusha.

Katika kauli yake jana, Mbowe ameibua tuhuma nzito dhidi ya Jeshi la Polisi, ambapo alidai kuwa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) ndiye aliyerusha bomu hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa,baada ya kutembelea majeruhi katika Hospitali ya Selian, Mbowe alisema chama chake kina ushahidi wa kutosha juu ya askari huyo kurusha bomu.

Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni,alisema wamefanikiwa kupata ushahidi wa kutosha juu ya tukio hilo baya linalochafua taswira ya nchi.

VIDEO YA MSHIRIKI WA TANZANIA ( FEZA KESSY ) AKIMUOGESHA MSHIRIKI WA ZIMBABWE ( HAKEEM) NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER


Video hizi  hutolewa na big borther wenyewe kwa jamii kama sehemu ya shindano hilo....

Wahiriki wote wa big brother wanajua  ya  kwamba jumba hilo limezingirwa na kamera kila kona.Kwa hiyo, kama mtu ataamua kufanya ufuska au kukaa uchi basi ajue kamera zitamrekodi na kumwanika hadharani....

Masharti hayo hujuzwa mapema kabla ya kuanza kwa shindano hilo...

Hakeem
Huyu ni mshiriki toka zimbabwe aliyepata bahati ya kuoga na dada yetu Feza ndani ya bafu moja 

Feza
 Huyu ni mshiriki toka Tanzania....Yuko ndani ya afu moja akioga na mshiriki  wa Zimbabwe.....

Dakika chache baada ya kila mmoja kuoga kivyake,Hakeem anaamua kumuomba Feza amsugue mgongoni....

Video iko hapo chini....Kuitazama ni shart uwe mtu mzima na ni hiari pia. 

<<  VIDEO  IKO HAPA >>

CCM YASHINDA KATA 16 KATI YA 22 UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI,CHALAANI CHADEMA KUJITAFUTIA UMAARUFU MISIBANI

Itakumbukwa tarehe 16/06/2013 ilikuwa ni siku ya uchaguzi mdogo wa madiwani kwa baadhi ya kata nchini. Uchaguzi huo umefanyika kwenye kata ishirini na mbili (22)  kati ya kata ishirini na sita (26) zilizotangazwa kufanya uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi wazi.
                    Bw Nape Moses Nnauye

 Matokeo tuliyoyapata toka kwenye maeneo yaliyofanya uchaguzi yanaonyesha kuwa kati ya kata 22 zilizofanya uchaguzi CCM tumeshinda kata 16 sawa na asilimia 72.72% na wenzetu wamechukua kata 6 zilizobaki sawa na asilimia 27.28%.

 Tunawashukuru sana kote walikoonyesha imani yao kubwa kwa Chama chetu kwa kutupa dhamana ya kuendelea kuwatumikia. CCM inawaahidi utumishi uliotukuka.

Hata wale 27.28% walioamua kuwajaribu wenzetu, tunawatakia kila lakheri, kwani wametumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua wanaodhani watawasaidia kufikia malengo yao ya kimaendeleo. Uchaguzi kwenye kata hizi zote umeisha sasa tuwatumikie wananchi.
  Kata nne za jiji la Arusha hazikufanya uchaguzi baada ya kuahirishwa kufuatia tukio la kusikitisha la kulipuka kwa bomu kwenye mkutano wa kampeni wa Chadema mjini Arusha tarehe 15/06/2013.
 CCM tunalaani tukio hilo la mlipuko wa bomu na matukio yanayofanana na hayo katika nchi yetu.

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRI MUSHI AZIDI KUSOTA RUMANDE

 
Zanzibar. Mahakama Kuu ya Zanzibar, imekataa kumwachia kwa dhamana, mshtakiwa Omar Mussa Makame, anayekabiliwa na shtaka la kumuua Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki.Hatua hiyo ilifanywa jana na Jaji Mkuza Issac Sepetu, baada ya upande wa utetezi katika kesi hiyo ,kuiomba mahakama imwachie kwa dhamana mshtakiwa hadi hadi hapo upande wa mashtaka, utakapokamilisha upelelezi.Alisema mahakama itaendelea na kesi isiyokuwa na dhamana na ambayo upelelezi wake unaweza kuchukua hadi miezi tisa.
 
 Jaji huyo alisema mahakama haifanyi kazi zake kwa kuzingatia taarifa za watu au magazeti yaliyoko nje yake.“Mahakama hii haichukui vielelezo vya barua za nje ya chombo hiki. Mtu anayeweza kusema kila kitu ni mkurugenzi wa mashtaka, yeye ndiye mwenye dhamana ya kuondoa kesi mahakamani,” alisema Jaji Sepetu.
Baada ya msimamo huo, wakili Abdallah Juma anayemtetea mshtakiwa, aliiomba mahakama iuamuru upande wa mashtaka ,kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo.
Alisema ni vyema upande huo ukatoa muda maalum wa kukamilisha upelelezi huo.
Jaji aliipanga kesi hiyo kutajwa tena Julai 2 mwaka huu.
Omar ambaye ni mkazi wa Mwanakwerekwe, Mjini Magharibi, anadaiwa kumuua kwa kumpiga risasi Padri Mushi Februari 17 mwaka huu.
Mwananchi

BANANA ZORRO KURUDI KWENYE GAME KWA KISHINDO

 
Msanii na mmiliki wa Band ya B-band Banana Zorro amefunguka kuwa kimya kingi siku zote kina mshindo na kueleza kuwa alikuwa kimya kwa sababu alikuwa busy na kazi za Band lakini kwa sasa anatarajia kudodosha ngoma nyingine siku za karibuni kwa wale fans wake kaeni mkao wa kura. Banana amefunguka hayo leo alipokuwa katika Show ya Kikaangoni Live inayofanyika kila siku ya Ijumaa kupitia Accounts za Facebook za Eatv na East Africa Radio ambapo mashabiki wake wanapata nafasi ya kuuliza maswali na yeye kuwajibu. 
Moja ya shabiki aliuliza akitaka kujiunga katika B-band afanyaje na jibu lilikuwa anapaswa kufanya mazoezi ya kutosha na akiwa teyari awasiliane na meneja wake Allan Lucky na mambo yatakuwa poa.
Akizungumzia moja ya fanikio aliyopata katika Muziki ni pamoja na kumiliki Band yake mwenyewe ambayo ni B-band ambayo inaendelea kukuwa kila siku na kufanya vizuri pia.

CATHY WA BONGO MOVIE ALIA NA USHIRIKINA ULIPO NDANI YA TASNIA HIYO....AWATAKA WASANII WAMRUDIE MUNGU

Mwigizaji wa Bongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’  naye amenyanyua kinywa chake na kuonesha jinsi gani anakerwa na wasanii wanaoshinda kwa waganga ili kutafuta ustaa.
Akiongea na mwandishi  wetu hivi karibuni, Cathy alisema kuna baadhi ya wasanii (hakuwataja majina) wamekuwa na tabia za kuzunguka kwa waganga wakitafuta kuwa juu katika tasnia ya filamu suala ambalo halipendezi na kuwasihi wawe na hofu ya Mungu.

“Vifo vya wasanii vimetokea vingi sana, nilidhani kutokana na vifo hivyo wangepata hofu ya Mungu na kuacha mambo yasiyofaa vikiwemo vitendo vya kishirikina lakini hawakomi, wananikera sana. Ipo siku wataumbuka kwani Mungu siyo binadamu,” alisema Cathy.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 18, 2013

.
.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...