Monday, April 30, 2018

MCHUNGAJI KKKT ADAI KUNA UBABE KATIKA KANISA HILO

Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kigogo, Richard Hananja amedai kuna ubabe katika kanisa hilo.

Hata hivyo, amesema licha ya kanisa hilo kupitia mambo mengi anaamini litaendelea kusimama imara hasa katika kipindi hiki.

Mchungaji Hananja amesema hayo Aprili 29, 2018 alipozungumza na Mwananchi kuhusu baraza la maaskofu wa KKKT ‘kuwatenga’ maaskofu watatu kwa kutosoma waraka wa ujumbe wa Pasaka kwenye dayosisi zao.


Amedai kuna ukabila na makundi, huku watu wakichukuliwa hatua kibabe kwa mambo yanayotokea hata kama hawakuhusika.

“Kwenye haya makanisa kuna ubabe mkubwa, kuna ukabila na makundi. Ninyi wa nje hamuwezi kuona, sisi wengine tulishafukuzwa muda mrefu lakini bado tupo kwa sababu,” amedai.

Amesema kanisa ni taasisi inayohubiri amani na iwapo maaskofu wameona wamtenge mwenzao hilo ni la kwao.

“Yale unayomtendea mwenzio ndiyo utakayotendewa,” amesema Mchungaji Hananja.

Chanzo: Mwananchi

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...