Wednesday, November 27, 2013
SOMA MASHITAKA 11 YA MH. ZITTO NA DK. KITILA
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, akionyesha nakala ya kile
alichokieleza kuwa ndiyo mpango wa mabadiliko 2013 uliosababisha adhabu
ya kuvuliwa nyadhifa za aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho,
Zitto Kabwe, na Dk. Kitila Mkumbo, wakati akizungumza na waandishi wa
habari makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam jana.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Habari wa chama hicho, John Mnyika.
*****
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, alisema barua hizo, ambazo Zitto na Dk. Mkumbo, walitarajiwa kukabidhiwa jana, zinawataka wajieleze kwa nini wasichukuliwe hatua zaidi, ikiwamo kufukuzwa uanachama.
Alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana, siku mbili baada ya Zitto na Dk. Mkumbo, kuitisha mkutano na waandishi wa habari, Jumapili wiki iliyopita na kusema hadi siku hiyo walikuwa hawajapata barua hizo zaidi ya kusikia suala hilo kwenye vyombo vya habari.
CECAFA CHALLENGE CUP 2013 KUANZA RASMI LEO, STAR v ZAMBIA…TAKWIMU ZA TIMU ZOTE
Na Baraka Mbolembole
Timu ya Taifa ya Kenya ' Harambee Stars', leo itakata ' utepe' wa
michuano ya Mataifa ya ukanda wa CECAFA, kwa kucheza na timu ya Taifa ya Ethiopia. Wenyeji hao wa michuano ya sasa na makamu bingwa wa taji hilo, wanapewa nafasi kubwa ya kuvuka kundi A, mbele ya Ethiopia,
Zanzibar, na Sudan Kusini.
Mabingwa watetezi, Uganda wao wapo kundi C, pamoja na Rwanda, Sudan, na Eritrea katika kundi linalotarajiwa kuwa gumu zaidi katika michuano hiyo. Moi Kasarani na Nyayo Stadium, ni viwanja viwili vilivyopo
katika jiji la Nairobi, Kisumu Stadium, Mombasa, na Machakos ni idadi
ya viwanja vitano ambavyo vitazipokea timu 12. Mapema leo mchana wawakilishi wengine wa Tanzania, timu ya Zanzibar Heroes itacheza na Sudan Kusini katika mchezop wa kwanza kabisa mwaka huu.
KILIMANJARO STARS vs ZAMBIATimu
ya Taifa ya Tanzania Bara itaanza kibarua chake cha kwanza siku ya
kesho, Alhamis kwa kucheza na timu ' alikwa' ya Zambia katika mchezop
unaosubiliwa kwa hamu na wapenzi wa soka. Zambia, mabingwa wa michuano
ya Mataifa ya Ukanda wa Kusini mwa Afrika, COSAFA, iliifunga Kilimanjaro
Stars katika mchezo wa mwisho kukutana katika michuano hii,
walipoalikwa kwa michuano iliyofanyika, Dar es Salaam, 2010.
Mbele ya Rais wa Jamhurio ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, Stars ilipoteza kwa kulala bao 1-0 siku ya ufunguzi.
Mbele ya Rais wa Jamhurio ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, Stars ilipoteza kwa kulala bao 1-0 siku ya ufunguzi.
Subscribe to:
Posts (Atom)